Ukiachilia Yoote aliyoyafanya Mandela na tukadhani hatuwezi kumpata atakaye fafana naye. Hakika Mungu katupa Mandela wa pili wa Afrika. Hakika UHURU JOMO KENYATTA NI MANDELA WA PILI. Baada ya maamuzi ya mahakama ameongea na kuwataka Wakenya wawe na Amani na kujua kuwa KENYA ipo hata kama yeye atakuwepo. Ujue kuwa kuna Jirani yako, ndugu yako hakika Uhuru nashindwa jinsi ya kumwelezea. Kikubwa ninachokuomba Rais wetu MAGUFULI badilika kwa kuona kuwa Wote sisi ni Watanzania na kila moja wetu anayo haki ya kusema na kushauri. Wapinzani wako wote ni WATANZANIA. Ondoa yale mawazo uliyonayo kuwa Tanzania ni CCM. Na bila CCM hakuna Tanzania. Jua kuwa tumejifunza mengi kutoka kwa jirani zetu Kenya. Usitupeleke tukaanza kuwaza kuwa mpaka watu/raia wafe ndio Amani ipatikane. Rais MAGUFULI tunaomba simamia na kuendeleza kupata katiba mpya. Utakumbukwa katika TANZANIA na dunia. Mabaya/ mazuri yote uliyoyafanya/unayofanya HAYATASAULIKA KATIKA VIZAZI VYOTE KAMA ILIVYO KWA Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nikuonye pia ukishikilia huu mwenendo wako wa sasa hivi wa kutokufuata sheria kufuata Uongozi wa Kagame au Museveni HAKIKA UTAISHIA PABAYA PAMOJA NA FAMILIA YAKO KATIKA UZEE WAKO. DUNIA IMEBADILIKA. Hakuna aliejua kuwa leo Kenya itakuwa hapo ilipo. UHURU JOMO KENYATTA alikuwa na madaraka yote kama uliyonayo wewe angeweza kutoa amri kuzuia hiyo mahakama kabla haijaanza na hata kuwaua lakini alichojali na kuweka mbele ni WAKENYA