Uhuru Jomo KENYATTA Ni Mandela Wa Pili Afrika

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,767
Reaction score
1,526
Ukiachilia Yoote aliyoyafanya Mandela na tukadhani hatuwezi kumpata atakaye fafana naye. Hakika Mungu katupa Mandela wa pili wa Afrika. Hakika UHURU JOMO KENYATTA NI MANDELA WA PILI. Baada ya maamuzi ya mahakama ameongea na kuwataka Wakenya wawe na Amani na kujua kuwa KENYA ipo hata kama yeye atakuwepo. Ujue kuwa kuna Jirani yako, ndugu yako hakika Uhuru nashindwa jinsi ya kumwelezea. Kikubwa ninachokuomba Rais wetu MAGUFULI badilika kwa kuona kuwa Wote sisi ni Watanzania na kila moja wetu anayo haki ya kusema na kushauri. Wapinzani wako wote ni WATANZANIA. Ondoa yale mawazo uliyonayo kuwa Tanzania ni CCM. Na bila CCM hakuna Tanzania. Jua kuwa tumejifunza mengi kutoka kwa jirani zetu Kenya. Usitupeleke tukaanza kuwaza kuwa mpaka watu/raia wafe ndio Amani ipatikane. Rais MAGUFULI tunaomba simamia na kuendeleza kupata katiba mpya. Utakumbukwa katika TANZANIA na dunia. Mabaya/ mazuri yote uliyoyafanya/unayofanya HAYATASAULIKA KATIKA VIZAZI VYOTE KAMA ILIVYO KWA Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nikuonye pia ukishikilia huu mwenendo wako wa sasa hivi wa kutokufuata sheria kufuata Uongozi wa Kagame au Museveni HAKIKA UTAISHIA PABAYA PAMOJA NA FAMILIA YAKO KATIKA UZEE WAKO. DUNIA IMEBADILIKA. Hakuna aliejua kuwa leo Kenya itakuwa hapo ilipo. UHURU JOMO KENYATTA alikuwa na madaraka yote kama uliyonayo wewe angeweza kutoa amri kuzuia hiyo mahakama kabla haijaanza na hata kuwaua lakini alichojali na kuweka mbele ni WAKENYA
 
Kwa sababu anajua alichokifanya kwenye uchaguzi halafu acha kafananisha Mandela na vitu vya kijinga Mandela hakuwahi kuuwa wala kutuhumiwa kwa mauaji tofauti na Uhuru ananuka damu
 
 
Kiukweli nimemkubali Uhuru kwa kile kinachoitwa kutenguliwa kwa matokeo ya uchaguz yaliyompa yeye ushindi wa kuwa Rais! Nimesikiliza hotuba yake kwakwel nimempenda sana kwa kuonesha uzalendo na utu maana angeweza hata kukataa maana alikuwa na mamlaka kamili kisheria kuwepo kwenye kiti hicho! Hakika yy ni shujaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakushukuriwa kwa Wakenya ni muungano wa Nasa kwani wamewapatia mwelekeo kumbuka pasipo wao kuelekeza nguvu zao mahakamani haya yaliyoamuliwa leo wasingeyapata


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani unamsifia mwizi wa kura kweli wewe ubongo wako una kutu!
 
tehe tehe tehe, mwizi anaposhikwa na ku surender anasifiwa, HII INATAKIWA IONYESHE JINSI GANI AFRICA IMEKOSA DEMOCRACY...
Mkuu samahani kidogo....,
Ulielewa msingi wa maamuzi ya kubatilisha matokeo au lugha ya malkia ilikuwa na ukakaso kidogo?
 
Mandela gani wakati analalamika watu sita tu kufuta matokeo? Mbona hamfuatilii mambo nyie? Kaonyesha waziwazi kabisa kuwa haafiki but katiba inamkaba hana ujanja. Wizi umemtokea puani. Angeitwa Mandela tu kama angepongeza uamuzi wa mahakama bila hisia hasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Nchi bado changa sana kwa hayo mambo mnayotaka yawe. Unafahamu maana halisi ya Demokrasia au unaropoka tu? Wazungu wamewaletea hii kitu wakifahamu kabisa nyinyi bado sana. Imagine Demokrasia hii hii umoe nchi Lissu, if any. Sijui kama unapata picha ya ninachojaribu kukuonyesha? Fikiria Libya, Iraq nk. Hata Syria pia. Hao nao wanapambana kupata demokrasia. Unaona walipo sasa? Acheni kucopy na kupaste haya mambo. Acha kwao wafanye ninyi mna tamaduni tofauti na wao. Wazungu hamwafahamu vizuri nyie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…