Uhuru Kenyatta abatilisha adhabu ya kunyongwa kuwa kifungo cha maisha

Uhuru Kenyatta abatilisha adhabu ya kunyongwa kuwa kifungo cha maisha

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta lro amebatilisha adhabu ya kunyongwa Kwa wafungwa zaidi ya 2000 kuwa kifungo cha maisha.Nchi ya Kenya haijawahi kunyonga RAIA wake Kwa miongo 3 sasa.

======

Waliohukumiwa kifo Kenya wabadilishiwa hukumu
_92068098_269ce51a-fa8a-41e7-aab9-7e1da3547445.jpg
Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametatilisha hukumu ya wafungwa zaidi ya elfu mbili ambao walikuwa wamehukumiwa kifo.

Rais amebadilisha hukumu hiyo na sasa wafungwa hao 2,747 watatumikia hukumu ya maisha jela.

Wahalifu wamekuwa wakihukumiwa kifo Kenya lakini hakuna aliyewahi kuuawa tangu miaka ya 1980.

Watetezi wa haki wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa hukumu hiyo.

Baadhi ya wafungwa hata hivyo wamekuwa wakilalamika kwamba hakuna tofauti ya hukumu ya kifo na maisha jela kwani mfungwa huwa anaishi jela hadi kifo chake.

Rais Kenyatta pia amewaachilia huru wafungwa 102 waliokuwa wakitumikia vifungo virefu.

Alhamisi wiki iliyopita, Rais Kenyatta alikuwa amewaachilia huru wafungwa takriban 7,000 wa makosa madogo madogo au waliokuwa wanakaribia kumaliza kutumikia vifungo vyao, na ambao walikuwa wameonyesha dalili za kubadilisha tabia.

Chanzo: BBC London.
 
Ni kawaida, katiba ya nchi inampa mamlaka ya kutotia saini kuthibitisha kunyongwa badala yake kutoa adhabu mbadala kama hiyo ya kifungo cha maisha.
 
Back
Top Bottom