Uhuru Kenyatta ahaadi kuachia nchi endapo upinzani watashinda

Aputwike

Senior Member
Joined
Aug 9, 2016
Posts
172
Reaction score
189


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amejinasibu kuachia madaraka kwa amani katika uchaguzi ujao endapo upinzani utashinda ili kuheshimu maamuzi ya wananchi.

Kenya ndio nchi pekee inayo heshimu misingi ya katiba, na demokrasia katika nchi za maziwa makuu, lakini zote zilizobaki zimekuwa vichaka vya maharamia wa ubakaji wa demokrasia, au madikteta, au manduli. Zipo tayari kuona watu wakipotea maadamu mkate wao upone.

Source: ITV
 
Ameshakomaa na kupevuka kisiasa, ngoja tuende mdogo mdogo na hawa wanasesere wetu!
 

Matamshi ya Mheshimiwa Raisi Uhuru Kenyata ni matakwa ya kikatiba na uongozi bora, na hayatakiwi wala kusifiwa. Kwa kutoa matamshi kama haya Uhuru Kenyata au kiongozi mwingine yoyote hatakiwi kupata credit kwani kimsingi anatekeleza wajibu wake
 
".......Nchi zingine zilizobaki zimekuwa vichaka vya maharamia wa ubakaji wa demokrasia......"
Hayo ni maneno YAKO ama ya ITV?
Sidhani ITV walisema hayo yote uliyoyaandika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…