Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Rais Uhuru Kenyatta ameukashifu mrengo wa NASA kwa kutishia kutohudhuria kikao cha pamoja cha bunge la taifa na lile la seneti leo. Rais anasema uwezo wa kiidadi ulio nao mrengo wa Jubilee kwenye mabunge yote unauwezesha kupitisha miswada na hivyo atatoa hotuba yake ilivyopangwa.
Kinara mwenza wa NASA Moses Wetangula hata hivyo anasema kikao hicho kinafaa kuahirishwa hadi rais atakayechaguliwa kwenye marudio ya uchaguzi aapishwe na kwa sasa Rais hana mamlaka ya kufungua bunge. Pia Moses Wetangula amesema wataohudhuria wataadhibiwa.