Uhuru Kenyatta denies rift between Kenya and Tanzania

..chairman wa SADC troika ana dhamana ya kuelekeza operation za pamoja za majeshi ya SADC.

..Nimeshangaa Raisi hakwenda kwenye mkutano huo badala yake akawa nchini akihudhuria mkutano wa ma-engineer.

..waziri wa mambo ya nje alipaswa kumshawishi Raisi kwamba SADC Troika ni dhamana na heshima kubwa kuiongoza na Raisi wetu anapaswa kuhudhuria mkutano huo.

..mikutano ya ma-engineer Raisi ameshahudhuria mingi tu kwasababu alikuwa waziri wa ujenzi for 15+ yrs.

..SIASA ZETU ZA MAMBO YA NJE ZIMELEGALEGA.

Kafrican, kilam, MK254
 

Tuende mbele turudi nyuma, kwa kweli binafsi sioni tatizo hapo maana mfumo wa uongozi kwenye nchi yenu una cheo cha waziri mkuu mwenye mamlaka. Hivyo kwa yeye kumwakilisha rais, hapo naona ilikua sawa tu. Pia huyo waziri mkuu wenu nimemskliza mara nyingi, yupo sawa sana kwenye kujieleza na sio mkurupukaji. Yupo makini sana na anatumia hekima kila anapoongea.

Japo pia masuala yanayohusu kongomano la marais wa mataifa tofauti, yanahitaji rais mwenyewe ahudhurie maana pale ndipo kunakua na kitu tunata "peer to peer networking" na maamuzi yanafanyika mengi. Lakini hata hivyo nategemea waziri wenu mkuu aliwakilisha rais ipasavyo.

Halafu vipi JokaKuu mbona ngosha Magu ana mikwara sana siku hizi kwenye hotuba zake, kwani itakua mumemfikisha pasipo na lile lenu la UKUTA. Nimeona hotuba zake kweye Youtube, hadi anapiga mayowe ya vita hiiiiiiiiii!!! Katika hali hiyo itabidi wapinzani muwe wapole na kumbembeleza akubali katiba ifanyiwe marekebisho.

La sivyo naona kama upinzani utafutwa kabisa ndani ya Tanzania, ikizingatiwa Wabongo wengi hususan vijijini wanakipenda sana chama tawala. Siku moja nipo maeneo huko Bongo tunakunywa vinywaji na kuburudika na live band, halafu ghafla wale watumbuizaji wakaanza kuimba wimbo wa CCM yaenda mbele, aisei nilishangaa wateja wote walinyanyuka wote na kwenda kucheza tena kwa raha sana. Hivyo hicho chama bado kina umaarufu sana na hayo mambo ya UKUTA sidhani kama yanaweza kubadili chochote, muwe wapole na kuwa na mikakati mipya ya kujadiliana na rais kule ikulu moja kwa moja tena kwa ushirikiano ili mrekebishe katiba.
 
Ukali wa Magufuli ulikuwepo tokea alivyokuwa Waziri, watu walimchagua kutokana na ukali wake.
 

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania.

Akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana.

Alisema anaona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema.

Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili.

Alitaja kufunguliwa kwa njia inayojulikana kama “northern frontier” ambayo itaunganisha bandari ya Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, hadi Bujumbura, Burundi – njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka Bujumbura hadi Mombasa kwa kilomita 300 nzima.

“Afrika Mashariki haiko katika mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kenyatta. “Afrika Mashariki inashindana na dunia. Tunataka kujaliana (pale penye mapungufu). Tunataka tutumie nguvu zetu ili kukua, kuendeleza na kuinua uchumi wetu,” alisema.

Kutokuwepo kwa Rais John Magufuli wa Tanzania katika mkutano wa hivi karibuni wa kimataifa na Tokyo mjini Nairobi kulizusha uvumi kuhusu uhusiano wa nchi za eneo hilo.

Kiongozi huyo wa Tanzania ametembelea Uganda na Rwanda tu tangu achukue madaraka Oktoba mwaka jana ukilinganisha na rais aliyemtangulia Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisafiri sana nchi za nje.

Rais Magufuli pia hakuhudhuria mikutano karibu mitano ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mkutano wa shirika la biashara duniani na mikutano mikuu ya AU mjini Addis Ababa na ule wa Kigali Rwanda hivi karibuni.

======================

He asked the media to stop spreading ‘lies’, saying the region’s interests are to expand its horizons to other neighbouring countries such as Somalia and Ethiopia.

The absence of the Tanzanian leader John Magufuli during the Tokyo International Conference on African Development led to speculation on his commitment to regional integration.

However, Foreign Affairs Cabinet Secretary Amina Mohamed said the President Magufuli had sent a representative, Prime Minister Kassim Majaliwa.

“He is not the only one who didn’t attend. In fact, he was well represented so there is nothing to worry about. Tanzania and Kenya have excellent relations, so let us not dwell on the negatives,” she said in a phone interview.

The Tanzanian leader has only travelled to Uganda and Rwanda since assuming office last October unlike his predecessor Jakaya Kikwete who was known to make many foreign visits.

He has also skipped at least five international meetings, including the World Trade Organisation conference in Nairobi last December, the AU Summit in Addis Ababa in January, the United Nations Conference on Trade and Development in Nairobi last month as well as the AU meeting in Kigali.


Source: Daily Nation
 
Kenyatta amepotea Magufuli mshirika wake wa karibu ni Raila Odinga
 
Kumbe Rais uhuru naye anapitiapitia jf na kujionea porojo za BAVICHA? aisee.
 
As a president what did you expect him to say? He is diplomatic not aaaa like .....
 
Kenyatta amepotea Magufuli mshirika wake wa karibu ni Raila Odinga
Hapana siyo kweli, mahisiamo ya JPM na Raila ni ya kifamilia zaidi na mahusiano ya JPM na Uhuru Kenyatta ni mahusiano kati ya nchi na nchi. Hivyo ni kujitoa ufahamu kwamba Rais Kenyatta amepotea.
 
Yaani watu wanakesha kuaminisha watu rais ni mbaya, asante Kenyata kwa kuweka mambo wazi.
 
As a president what did you expect him to say? He is diplomatic not aaaa like .....
Tatizo lenu BAVICHA ndilo hilo, jambo linapokuwa Chanya mnaingiza porojo na linapokuwa HASI mnalikomalia. Aibu yenu.
 
Tatizo lenu BAVICHA ndilo hilo, jambo linapokuwa Chanya mnaingiza porojo na linapokuwa HASI mnalikomalia. Aibu yenu.
Hicho ndicho kilichobakia kwa BAVICHA, kila wanaposhika wanapigwa mweleka. Hawana jinsi zaidi ya kutapatapa na maneno mbofu mbofu.
 
Tatizo lenu BAVICHA ndilo hilo, jambo linapokuwa Chanya mnaingiza porojo na linapokuwa HASI mnalikomalia. Aibu yenu.
Ndo akili yako ilipo kila anayetoa hoja unadhani ni bavicha! Angalia content wewe
 
Ukisoma vizuri, hawajasema kwamba kuna rift. Wamesema the exact opposite - kwamba hakuna rift.

Kenyatta hana tatizo, wenye matatizo ni wapambe wake na baadhi ya raia wanao penda penda kukuza mambo - kwani Dk.Magufuli kuwakilishwa na wasaidizi wake kwenye mikutano kuna tatizo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…