Uhuru Kenyatta: Mabeberu watuheshimu na sisi tutawaheshimu

Uhuru Kenyatta: Mabeberu watuheshimu na sisi tutawaheshimu

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Chungu ya Mabeberu imemfikia Uhuru Kenyatta uzalendo umemshinda ayataka mataifa ya ulaya kuacha kuingilia maswala ya ndani ya nchi yao (Kenya)

'Mtuheshimu ndio tuwaheshimu', Rais Kenyatta aonya nchi za nje dhidi ya kuingilia masuala yake ya ndani

Chanzo: BBC SWAHILI.

MY TAKE; Uhuru Kenyatta hakujua kuwa Mabeberu hawana marafiki wa kudumu yeye kutanjwa tu kwa nchi yake kuwa sio sehemu salama ya kutembelea kwasababu ya COVID 19 tayari povu linamtoka alifikiri Magufuli ni mjinga anaye wapiga hawa watu kila siku.
 
Sasa asubiri matukio kutoka kwa wasomali. USA ndo hao wanakitoa. Alshababu watajitanua.Ila arudishe basi na pesa za Covid 19.
Tutaelewana tu
 
Tatizo viongozi hawa Waafrika hawawezi kuwaambia "mabeberu" uso kwa uso, wanaongea haya katika mikutano na wenyeji wakiwa katika kaunti , magavana , wawakilishi wa maendeleo wadogo au mikutano yao ya chama.

Hawathubutu kusema haya Beijing, New York , Washington D.C, Paris, Brussels , Geneva n.k wakikutana na wakubwa kabisa wa nchi za mabeberu au wakubwa wa WHO, IMF , World Bank , EU n.k.

 
Alifikiri anapendwa sana
Wakuu,

COVID-19 ilisambazwa kwa makusudi duniani ili kusababisha migogoro kati ya mtu na mtu, jamii kwa jamii, taifa kwa taifa, mataifa kwa mataifa kisha uhai na mauti. COVID-19 haina rafiki awe mweupe, mweusi, mwekundu, mrefu, mfupi, msomi, maamuma, tajiri au maskini wote wako sawa mbele ya kirusi hicho chenye uwezo wa kujenga chuki ndani ya mtu dhidi ya mwingine bila sababu za msingi ila ubinafsi tupu ndio lengo lake halisi.

Maadui ni rahisi sana kuchonganisha kati ya mtu na mtu , taifa kwa taifa kupitia athari za ugonjwa wa COVID-19 kwa hiyo unapochngamana na mtu, jamii, au taifa jitahidi kutunza siri za ndani ya chumba chako unacholala zisiende nje hata kama humo ulimo kuna fukuto, ukikurupuka kwa ulimbukeni wa kuchukua mfumo wa maisha wa Magharibi kwamba wewe ni mwanahakati wa kupigania haki, atakaye kupongeza ndiye atakuja kukutweza na hautaamini kitakachotokea.

Nafikiri kama kuna watu wana rangi ya bluu inawezekana wakawa na roho ya pekee lakini sio hawa walio juu ya uso wa dunia tunayoishi wanadamu wote tukionekana kwa macho na kugusika kwa kushika.

Bado athari zake zitakuja kusababisha vurugu kubwa sana Ulaya, Marekani na kwa sehemu Afrika kisha baadhi ya maeneo ya nchi husika kutamani kujitenga na kujitawala wenyewe.

Huko mbeleni watu, jamii, nchi na mataifa ambayo yaliungana kwa nia njema hapo kabla wataingiwa na kirusi kisichoonekana kwenye fikra zao na kufanya mtengamano wao kuwa tete; baadhi watatengana kwa uhakika ikiwemo USA ambayo state zake tatu zitasababisha mtikisiko usiotarajiwa katika taifa hilo kubwa
 
Naona lumumba mnajiliwaza na hiyo kauli ya Kenyatta, sioni ni kwa namna gani unaweza kulinganisha hali ya kisiasa kati ya Tanzania na Kenya kwa wakati huu, hali yetu ni mbaya zaidi hilo halina mjadala.

Na hii tabia yenu ya kishamba kuwaponda mabeberu kila wanapowaambia ukweli sijui mtaiacha lini, wakiwapa misaada yao mnawaita "marafiki wa maendeleo", wakiwalaani kwa ule uchaguzi wa maigizo mliofanya wanageuka mabeberu.

Kenyatta kuwazungumzia hivyo wazungu ana sababu zake tofauti ambazo kimsingi hazifanani kabisa na hizi za kwetu.

Ndio maana hata Kenyatta mwenyewe aliwashangaa kushindwa kwenu kukaa na wapinzani meza moja mpaka wanakimbia nchi yao waliyozaliwa, mnazalisha wakimbizi kwasababu za kishamba kabisa, halafu mnawalaumu mabeberu!.

Inawezekana hizo akili zenu zimeshikwa na hao mabeberu, amkeni usingizini mliokoe taifa, mkiendelea kukaa na hayo mawazo yenu mgando mtazidi kuliangamiza hili taifa, mnaiba kura kuongoza hamjui kila siku mnawalaumu mabeberu.
 
Chungu ya Mabeberu imemfikia Uhuru Kenyatta uzalendo umemshinda ayataka mataifa ya ulaya kuacha kuingilia maswala ya ndani ya nchi yao (Kenya)

'Mtuheshimu ndio tuwaheshimu', Rais Kenyatta aonya nchi za nje dhidi ya kuingilia masuala yake ya ndani

Chanzo: BBC SWAHILI.

MY TAKE; Uhuru Kenyatta hakujua kuwa Mabeberu hawana marafiki wa kudumu yeye kutanjwa tu kwa nchi yake kuwa sio sehemu salama ya kutembelea kwasababu ya COVID 19 tayari povu linamtoka alifikiri Magufuli ni mjinga anaye wapiga hawa watu kila siku.
Eeenh, nini kinamliza huyo 'lap dog'.

Trump, au baadae Biden hapo January, akifunua pochi tu, unasikia kisha kwenda mbio kwa hao anaowalalamikia.

Hakuna mtu mnafiki kama huyo bwana!
 
Back
Top Bottom