UHURU Kenyatta : Niko tayari kuondoka ofisini iwapo nitashindwa uchaguzi ujao

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais Uhuru Kenyatta, amesema yuko tayari kuacha madaraka pindi tu atakaposhindwa kwenye Uchaguzi Mkuu ujao

Kenyatta amesema ataheshimu uamuzi wa wakenya pamoja na katiba ya taifa na kuondoka uongozini atakaposhindwa

Ameyasema hayo baada ya kuulizwa suali na wanahabari huko Nyeri, iwapo yuko tayari kuondoka ofisini pindi tu atakaposhindwa Visa vya Marais kudinda kubanduka uongozini vinazidi kushuhudiwa barani Afrika, ikiwa kisa cha hivi punde kwa aliyekuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh

Jammeh alikuwa amedinda kubanduka ofisini baada ya kushindwa na Adama Barrow, lakini hatimaye kusalimu amri na kuamua kuacha madaraka na kwenda uhamishoni nchini Equatorial Guinea baada ya Jumuiya ya Ecowas kuingilia kati.

Chanzo : Radio Rahma
 
Hayo ni maneno ya viongozi wote wa kiafrika lakini kichwani kwake anajua atakachokifanya mpaka ashinde huo uchaguzi.Waafrika sio wa kisport sport.......
 
Uhuru is among the brilliant people Africa to have.

Impossible to level him with our sociopath statue like a man.
 
Angekua juma ponda mali sasa....
 
Ingekuwa kunauwezekano tukabadilisha tukamchukua uyu raisi mwenye akili akawa wetu.
 
Itakuwa ni ngumu mkikuyu amuachie nchi mjaluo haaaa utani wa mawe huo labda waweke mnandi na si hawa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…