NCCR wamechemsha maana 1963 Uhuru wenyewe nchi iliendeshwa na Sultan, (actually Uhuru halisi wa Zenj ulikuja baada ya Karume kufa - April 7th)(yes i kno wengine mtakasirika kusikia hiyo...)
Gozi fumu tafadhali fafanua zaidi hapa. Hii ndio transparency!!!! Tueleze .Hatukasiriki kwani siku hiyo kuna mtu alitimiza lengo lake na kuimeza Zanzibar kwa ujumla. Kabla ya tarehe hiyo kulikuwa na mtu aliekuwa ngangari na jitihada zilipotimu nchi akapewa Mtanganyika nae kama alivyosema mwenyewe 'mtu kwao' akaigawa Zanzibar.
Joka Kuu sijui anachukulia mantiki gani? Waafrika ( Ni Wakenya pamoja na Wasomali pamoja na Wasudani). Washirazi -kwa mintarafu ya Zanzibar- Ni watu ambao chimbuko lao limetokana na Washirazi. (Watu waliotoka Iran )eneo la Shiraz ambao walikuja na majahazi Zanzibar na kuoa wenyeji- kwa kule kwetu kabila la mtu linatokana na Baba- kwa hivyo wenyeji wakapoteza ukabila wao katika kizazi kipya na hivyo ndio maana ya kuchimbuka kwa Wa-Shiraz wa Kizanzibari. Sasa Wazanzibari Washirazi wapo tu tena ndio wengi katika visiwa hivyo. Hiyo ni historical and sociological aspect of the Zanzibaris.shukran Jokakuu, waafrika hawakuutambua Uhuru ndio wakapinduwa. Jee Washirazi hawamo ? Eeeee ndio maana karume akawataka wachukuwe jinsiya (Tajnisi), maanake si Waafrika! heheheheeee
Joka K. Tatizo lako hutaki kufahamu. Zanzibar ni kisiwa. Wameingia wengi tu. Waafrika (kutoka katika Bara kuu la Afrika-Tanganyika, Malawi, Msumbiji, Somali, Misri,Kenya, Uganda na kwengineko). Wameingia wahindi kutoka India, Pakistan, Wameiingia Wa-iran. Wa-Oman, Wa -China, Wazungu kwa sababu mbali mbali. Wote hao walioa wenyeji, na nkizazi kilichifuatia kikajinasibu kwa kabila la Baba (au sehemu anakotoka Baba). Lakini kimsingi kizazi kilichofuatia ni Mzanzibari. Sasa hakuna pale Zanzibar kitu kama Mwarabu au Mhindi au Mngazija au Mchina au Muafrika au Mshirazai bali kuna Mzanzibari tu.Sasa awe mweupe mwekundu hudhurungi- Ni Mzanzibari.Pakacha,Mtwike,
..waZanzibari mkiachana na kasumba yenu ya UALABU mtaishi maisha mazuri sana.
..kama ndani ya mioyo yenu na akili zenu mnajiona Washirazi au Waarabu basi jaribuni kurudi Iran au Oman na mdai haki zote kama raia wa nchi hizo.
...Sasa hakuna pale Zanzibar kitu kama Mwarabu au Mhindi au Mngazija au Mchina au Muafrika au Mshirazai bali kuna Mzanzibari tu.Sasa awe mweupe mwekundu hudhurungi- Ni Mzanzibari.
Nitayanukuu maneno ya Juma Duni
"SIKU YA UHURU IPO NA ITAENDELEA KUKUWEPO CCM WAKITAKA WASITAKE"
Utawala wa kisultan ulikuwa wa kidhalim?
na je wa Karume ulikuwa wa nini???
Huyo Duni ni mlevi wa Tende!
Naona mnababaishana Sultan alihamishia makao yake makuu Zanzibar kutoka Oman ndivyo inavyoeleweka ,Zanzibar ilipewa au ilijinyakulia Uhuru ikiwa na serikali yake kamili Sultani baada ya Uhuru alikuwa kama nembo ya Zanzibar , jambo ambalo hadi leo lipo Uingereza na baadhi ya nchi za Scandinavia au si kweli ?Mtwike,
..Sultani wa kwanza alitokea Oman na kujitwalia utawala ZNZ.
..baadae akaja Muingereza wakawa na makubaliano yao na Sultani.
..huo Uhuru wa 63 ulirudisha madaraka kwa Sultani.
..madaraka yalipaswa kurudishwa kwa Waafrika siyo Sultani. Kwa sababu hiyo basi Uhuru ule ulikuwa kiinimacho tu, na ndiyo sababu ya Waafrika kufanya Mapinduzi.
Mtwike,
..Sultani wa kwanza alitokea Oman na kujitwalia utawala ZNZ.
..baadae akaja Muingereza wakawa na makubaliano yao na Sultani.
..huo Uhuru wa 63 ulirudisha madaraka kwa Sultani.
..madaraka yalipaswa kurudishwa kwa Waafrika siyo Sultani. Kwa sababu hiyo basi Uhuru ule ulikuwa kiinimacho tu, na ndiyo sababu ya Waafrika kufanya Mapinduzi.