Uhuru ni nadharia iliyokuwepo

Uhuru ni nadharia iliyokuwepo

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Uhuru ni hali ya kutofungamana na kitu chochote pamoja kufanya maamuzi yanayoweza kukupa furaha na amani.

Dhana potovu ya uhuru imekuwapo kwa muda mrefu huku tukiendelea kukaririshwa kuwa binadamu yupo huru na anahitaji uhuru au nchi ipo huru lakini nadharia hizi ni za uongo na zakupingwa.

Nadharia za sayansi ya jamii kama vile state of nature ya John Locke na Thomas hobbies zinaweza kutupa jibu sahihi kuwa binadamu hayupo huru pia uhuru wa binadamu unakuwa unamipaka kutokana na hali au cheo cha binadamu au nchi.

Zipo taasisi mbalimbali ambazo zinajinasibu kuwa binadamu anahitaji uhuru ili kuweza kutimiza malengo yake lakini aghalabu kwa taasisi zenyewe kuwa huru,tambua kuwa uhuru ni kitu ambacho hakipo na hakitokuwepo katika dunia hii.

Watu waliosoma elimu ya saikolojia au filosofia wanaweza kujua kitu gani nachoomaanisha nikiwatajia neno "consciences" kuwa ndiyo kitu pekee kinachoweza kumpa mtu uhuru wa kufanya maamuzi binafsi.

NB:

Unadai uhuru wakati bado haipo katika nafasi yeyote katika chama au nchi tambua na ujue kuwa wewe ni mtaji au daraja la mafanikio kwa wengine.
 
Uko sahihi kabisa ukiangalia mambo kama tamaduni, Mila na desturi, Dini zetu, asili yako. Fikra nk. Hivi vinaweza ku influence uhuru. .
 
Back
Top Bottom