Uhuru: Nitatumia siku 100 kutimiza ahadi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Ataanza kwa ahadi ya matibabu bure kwa wanawake wanaofuata huduma za uzazi
Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kwamba atatumia siku 100 tu kutekeleza ahadi zake zote ambazo ameziahidi kipindi cha kampeni.
Alisema kwanza atatumia miezi mitatu tu kuondoa kabisa malipo ya Afya ya uzazi kwa kina mama katika zahanati zote na hospitali za umma.
Alisema kwamba Serikali yake itatoa kiasi cha Sh6 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mfuko wa vijana na wanawake .
Pia alikumbushia ahadi ya kutoa ‘laptop’ kwa wanafunzi wote wa shule za msingi watakaojiunga na shule za serikali mwakani.
Uhuru alisema kwamba kutekeleza ahadi hizo ni katika suala la utekelezaji wa sera na misimamo wa Muungano wa Jubilee.
“Mimi nina fahari kubwa kuwajali wanyonge waliokubali kunipa nafasi hii ya uongozi na nimekubali kulivaa vazi hili la uongozi hivyo nitasimamia sera za Jubilee kama tulivyoahidi Wakenya wakati wa kampeni,’’ alisema Uhuru.
Aliongeza kwamba yupo kwa ajili ya Wakenya wote waliompigia kura na hata wale waliowapigia wapinzani wake.
Uhuru alisema atawasaidia Wakenya pamoja na taifa zima kuelekea katika mizizi imara ya kiutajiri kwa njia ya amani, hali ambayo alisema inawezekana ikafanikiwa kwa kiasi kikubwa baadaye.
Naye mtaalamu wa Uhusiano wa Kimataifa, Profesa Munene Machariaalipokuwa akifanya mahojiano na Kituo cha Habari cha Xinhua ,alisemakwamba kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta, kuna uwezekano mkubwa kubadilika kwa sera za kiuchumi.
Alisema kwamba Rais huyo ambaye awali alikuwa katika Baraza la Mawaziri la awamu iliyopita akiwa Waziri wa Fedha anatakiwa kujenga uhusiano wa karibu na mataifa ya nje ili aweze kubadili sera za kiuchumi.
Pia alimtaka waziri huyo kuangalia suala la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na nchi jirani za Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Macharia alisema baada ya kuitumikia Serikali ya Kibaki, Kenyatta ana uwezo mkubwa wa kudumisha sera hiyo ya kiuchumi.
“Lengo la msingi kwa Serikali ya Kenyatta inatakiwa kuimarisha mahusiano yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchi wanachama (EAC) Kama majirani wa karibu,” Macharia alibainisha.
Wakati huohuo Rais mstaafu Mwai Kibaki aliwahakikishia raia wa Wakenya kuwa, wapo katika mikono salama baada ya yeye kustaafu rasmi juzi.
Alisema kwamba yeye anaanza maisha yake ya kustaafu, hivyo raia wote wa nchi hiyo wanatakiwa kufahamu kwamba wanabaki katika mikono salama wasiwe hivyowasiwe na hofu yoyote ile.
CHANZO: MWANANCHI
 
Serikali zote almost za africa zikiamua kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kusimamia wizi na ugujaji wa rasilimali pamoja na ukusanyaji wa mapato, kuna mambo mengi sana ambayo yangewezekana. Hilo la matibabu ya uzazi kwa wanawake bure linawezekana sana. Next time aahidi kutibu na watoto pia. Kama waliweza kutoa elimu ya msingi bure, nothing is impossible.
Hapo kwenye laptop ndo maneno iko. Na hajasema level gani, ni praimare ama hadi vyuoni?
 
laptop ni kwa watoto wanaojiunga na darasa la kwanza which if u ask me doesnt make much sense.
 
laptop ni kwa watoto wanaojiunga na darasa la kwanza which if u ask me doesnt make much sense.
Inategemea ni aina gani ya laptop. I still think it does make sense hasa nikitizama mwanangu wa miaka minne tu "anavyomudu" kutumia hizi technologies - ni kizazi tofauti sana hiki!
 
laptop ni kwa watoto wanaojiunga na darasa la kwanza which if u ask me doesnt make much sense.

mkuu jana nilikuwa naangalia kutuo cha K24 tv ya kenya.walizionyesha hizo laptops. Zile ni toys jamani.ni laptop ambayo ukimwagia maji haiharibiki,wala ukidondosha haipasuki.tudogo kama toys za game au lunch box.hahahaha wajinga ndio watakubaliana nae.
 
Inategemea ni aina gani ya laptop. I still think it does make sense hasa nikitizama mwanangu wa miaka minne tu "anavyomudu" kutumia hizi technologies - ni kizazi tofauti sana hiki!

zile sio laptops kama uzijuavyo vile ni vijitoy(toy laptops)jana nimeviona k24.
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…