Uhuru wa fikra na sanamu za shaba

Uhuru wa fikra na sanamu za shaba

Midnight

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
229
Reaction score
681
Mungu ibariki Afrika.

Heshima kwenu ndugu zangu katika Jamii forum, washiriki katika Jamii forum page Facebook, Telegram na search engine zote zenye unapata kuunganishwa na nyuzi zote makini kutoka JF.

Kwanza kabisa napenda kuupongeza uongozi wa JF kwa kuleta mabadiliko na elimu pana miongoni mwa Watanzania na Wana East Africa kwa ujumla wake. Pongezi nyingi sana kwenu nyote kwa kazi nzuri.

Acha niende moja kwa moja kwenye lengo langu kuu la kuanzisha nyuzi hii, huku likiwa sehemu ya jibu langu kama nilivyomwahidi mwanafamilia mwenzetu mmoja hapa ndani.

Kama ungepata nafasi ya kutembelea Marekani na ukapewa kazi ya kutembelea statues zote zilizopo USA ndani ya mwezi mmoja sijuia kama ungezimaliza. Hadi kufikia mwaka 2011 nchini Marekani kulikuwa na sanamu zaidi ya 5193 zilizosimikwa katika kona na maeneo mbali mbali ya kihistoria na makazi ya watu.

Tunaendelea...... Kuanzia vita za wenyewe kwa wenye, ukombozi hadi vita vya vietnam, michezo, ubunifu na viongozi, utumwa, na yote unayoyajua wewe kuhusu America yapo katika hali ya sanamu zilizo tengenezwa vyema kukumbushia matukio na kumbukumbu husika.

September 11 Wamarekani hawaikumbuki kwa maneno tu, Bali pale palipokuwa na majengo pacha yaliyoshambuliwa kuna statue na vipande vya vyuma vya majengo yale ambavyo vitatunzwa na kuwepo pale pale hadi kizazi chako cha tano.

Tukiangalia mfano huo mdogo tu wa Marekani jinsi wanavyo tunza kumbukumbu zao kwa njia ya sanamu hizo huku sisi tukiziona kama ibada na upotoshaji kiimani. Na wakati huo huo huko zilikoanzia hizi dini tunazozifuata ndipo penye mamia ama maelfu ya sanamu, mfano Roma Italia kuna mamia ya dazani za masanamu ambapo ukiachana na vile watanzania wengi mnaamini ovyo kuhusiana na maana halisi za sanamu ukweli ni kuwa kuna umuhimu sana kujua nini tunapaswa kufanya na nini hatupaswi. Tunaweka sanamu ya Steven Kanumba kwaajiri ya kumbukumbu ya ubora wake au tunamwabudu?

Watoto wetu wanapaswa kujifunza historia na matukio muhimu ya nchi zetu kupitia vitu vinavyoonekana kwa macho, vitu ambavyo vitaleta nguvu, wivu wa kujaribu, hamasa na uzarendo kwa nchi yetu pale kijana anapokaa chini ya sanamu ya Edward Sokoine na kusoma historia yake huku moyoni akijengwa hamasa na utayari wa kulitumikia taifa lake na siku moja na yeye picha yake isimame katika uwanja wa mashujaa milele huku ikitunzwa na kutembelewa na vizazi na vizazi.

Pia sioni kama kuna wajasiliamali dhabiti hapa Tanzania. Kama wapo basi waunge mkono wazo langu kisha Katika kuisaidia serikali Katika majukumu muhimu ya kutunza na kuhifadhi utajiri wa Tanzania 🇹🇿 watengeneze japo vituo mbali mbali ndani ya miji mikubwa hapa nchini, vituo ambavyo kutakuwa na statues za watanzania wenzetu walioipeperusha vyema bendera yetu tukufu.

Hata mjenge statue ya nembo yetu adhimu ya bibi na bwana na mkionyesha vyema yale maneno tukufu ya kuiheshimisha nchi yetu nasi tutafunga safari na kuja kuchangia fedha hapo na kupiga picha kisha kupost na wageni watatuuliza hapo ni wapi, tutaeajibu ni Tanzania 🇹🇿 nchi ya ardhi ya mlima kilimanjaro.

Niseme ukweli tu kwamba utajiri wa Tanzania 🇹🇿 Sio Simba, Nyati na twiga pekee, Sio mlima kilimanjaro, ziwa Victoria au mbuga maarufu ya Serengeti na wala sio uzuri wa visiwa vya zanzibar na harufu ya karafuu bali ni mimi na wewe, viumbe pekee wenye jukumu la kuilinda na kuitunza Tanzania, kulinda vilivyokuwepo na tulivyovipoteza.

Hakuna tena mtu kama mzee King Majuto popote pale duniani, hayopo tena Mtu kama Mzee Jengua, Steven Kanumba, Mwalimu Nyerere, John Pombe Magufuri , na wengine wengi ambao majina yao na mchango wao kwa taifa ni mkubwa mno.

Tuache chuki na wivu tuanze sasa kujenga statues za watanzania wenzetu walioipeperusha vyema bendera yetu tukufu na kuiheshimisha na watoto wetu watapata kujifunza kupitia kumbukumbu hizo.

Ahsanteni sana.
 
Kwa hiyo kila wanachofanya wamarekani lazima na sisi tufanye,wewe huoni kama huko ni kuiga utamaduni wa kigeni? mbona wao hawaigi vyakwetu?
 
Siyo kila kitu na cha kuiga...
Kama ni jambo zuri tutapaswa kuiga. Kama tumeacha kufuata baadhi ya mila mbovu na kuiga utamaduni mwingine mzuri toka ugenini, tutashindwaje kuiga na hili?
 
Kwa hiyo kila wanachofanya wamarekani lazima na sisi tufanye,wewe huoni kama huko ni kuiga utamaduni wa kigeni? mbona wao hawaigi vyakwetu?
Kuna vingi sana wameiga toka kwetu. Chunguza au Google ujionee..
 
Mungu ibariki Afrika.

Heshima kwenu ndugu zangu katika Jamii forum, washiriki katika Jamii forum page Facebook, Telegram na search engine zote zenye unapata kuunganishwa na nyuzi zote makini kutoka JF.
Umenena vyema midnight. Tujenge sanamu za kuwaenzi wenzetu walioweka mfano bora kwa Watanzania na binadamu wenzao. Sio kisiasa tu pia kwenye nyanja tofauti. Pia tuweke kumbukumbu kwa njia tofauti tofauti.

Kila mkoa utambue michango mbalimbali ya wananchi wake pia matukio. Mfano mkoa wa Kagera wekeni kumbukumbu za wasomi na wengine waliotoa mchango mkubwa katika nchi hii; Edward Barongo, Dr Mutahangarwa, Dr yule andiko lake la utafiti liliingia kwenye waliowania NOBEL PRICE miaka ya nyuma, waandishi mbalimbali km John Kihimbila, Dr Mutembei, Shekh Mustafa wa Katoro, Askofu J.Kibira, Prof Anna Tibaijuka na wengine wengi. Wasanii km Saida Karoli Chocho. Magwiji wa fikra km Ruge Mutahaba, Prof Mwesiga Baregu nk. Pia majanga kama janga la UKIMWI, TETEMEKO, KUZAMA KWA MV BUKOBA nk.
 
Shida ni gharama za miradi ya sanamu ukilinganisha na shida tulizonazo.
Hospitali zetu, shule zetu, barabara zetu na sehemu nyingine bado ni hoi, bajeti ya sanamu ingetosha kununua vitanda kwa ajili ya wajawazito, madawati shuleni au nyumba za walimu, kutengeneza madaraja vijijini n.k.
Huko Roma au USA kimiundombinu wametupiga gape, hivyo kujenga sanamu wakati kuna vitu vya msingi ni ukakasi.
 
Ukisha kuwa na sanamu ni hatua ya kwanza,hatua ya pili ni kuiabudu hiyo sanamu,kuiabudu hiyo sanamu inakuja automatically yaani mfano ni siku umeiangalia hiyo sanamu halafu siku hiyohiyo unalipwa yale malipo ya fedha yaliyokusumbua kulipwa kwa miaka mingi,basi utaanza kudhani hiyo sanamu imewezesha hayo malipo kufanikiwa na hapo ndo unakuwa mwanzo wako wa kuiabudu hiyo sanamu,huo mfano wa malipo yaliyokwama nifano mmoja tu,ipo nifano mingine mingi ambayo ina weza kulipelekea taifa kuwa la waabudu sanamu.
 
Una mawazo ya kilokole lokole sana. Kabla hata ya wakati huu tuliopo Tanzania ilishakuwa na utamaduni wa kuwa na masanamu ya waasisi wetu. Mfano nyelele square pale, hadi sanamu za masamaki maarufu waliopo Tz zipo.
Na ukizibrand vizuri unakuwa umetengeneza biashara na sehemu ya kuingizia kipato. Mfano pale Dodoma Nyerere square hapakauki watu, Mwanza kwenye picha ya samaki, nk, nk na watu wanapitia na kulipia hapo. Pia angalia pale ubungo kwenye sanamu ya mfano wa mlima kilimanjaro jinsi mwekezaji anavyopiga pesa za watu kutembelea pale na kupiga picha live na mlima.
Hayo mambo ya kuabudu sijui nini!! achana nayo hapa.
 
Kosa lako mtoa mada siyo kuongea kisicho cha maana. Kosa lako ni kumsifia jpm jamiiforums. Yaani adui mkubwa wa jf ni magufuri
 
Kosa lako mtoa mada siyo kuongea kisicho cha maana. Kosa lako ni kumsifia jpm jamiiforums. Yaani adui mkubwa wa jf ni magufuri
Mkuu Igombe, mimi ni mfanya biashara na kati ya watu walionienyesha kimaisha muongo huu ni huyo uliemtaja.
Lakini hapa nazungumzia kitaifa, na sio chama, au mtu mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom