Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Asubuhi ya Jumamosi Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa aliweka pandiko kwenye account yake ya Insta iliweka lebo kwenye gazeti la Nipashe "SIO KWELI (MISINFORMATION)" na kuongeza maelezo kuwa; PUUZENI UPOTOSHAJI HUU WA TAARIFA ZA DAWA ZA KUFUBAZA VIRUSI VYA UKIMWI (ARV). Dawa haziuzwi, tunazo za kutosha na zikipungua tutanunua zingine. Wananchi msiwe na hofu."
Baada ya hiyo, Wizara ya Afya Tanzania iliweka taarifa ya kusema kuwa uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ARV kuuzwa ni potofu, na kwamba dawa zipo za kutosha.
Nilipokutana na hiyo taarifa ya Msigwa niliagiza nitafutiwe gazeti nione kilichokuwa kimeandikwa... aisee boda walizunguka kote gazeti hamna, kuna sehemu moja akaambiwa gazeti halijatoka!
Ndio nikaelewa pini lilipigwa kabla magazeti hayajasambazwa kwenye vijiwe, na kama yalifika basi kote taarifa ilifika yasiuzwe.
Najiuliza, mpaka Nipashe wameandika ina maana walikuwa na ushahidi wa claims hizo. Badala ya kuzuia habari hiyo kuchapishwa na kushupasha shingo si wangetumia taarifa hiyo kuweka mambo sawa na kuuelewesha umma kuwa hakuna upungufu wa dawa hizo.
Maonyo 2 yametoka siku mmoja kwenye habari ambazo ukiangalia unashangaa kwanini inatokea hivi. Kadri tunavyosogea kwenye uchaguzi ndivyo vyombo vya habari vinavyozidi kuminywa.
Mkuu, mnataka kila mtu awe kasuku kurudia kile tu ambacho serikali inasema? Gerson Msigwa