Uhuru wa kifedha ni jambo la kufikirika kwa watanzania wengi na takwimu pia zinaonyesha ni asilimia ndogo sana yawatanzania walio na uhuru wa kifedha basi bila ata kufika mbali ata usalama wa kifedha nalo si jambo la kawaida.
Usalama wakifedha ni hali ya kutokuwa na wasiwasi wa fedha kwani una akiba ya kutosha kwa ajili ya matumizi, dharura, anasa na pia chanzo cha fedha kisichoweza kutetereka. Hili ni jambo ambalo watanzania wengi wa vipato vidogo na vikubwa hutakiwa kufikiria kwa sasa na kuanza safari yake.
Haya yote huanza na kubadilisha mfumo wa kufikiria kwenda na wakati na kuwa tayari kujifunza, kupata elimu ya fedha ambayo hujumuisha elimu na ujuzi wa kujiongezea kipato, kujilipa na kukuza mtaji kwa wafanyabiashara, kugawanya kipato kwa matumizi ya lazima ya kila siku mf chakula, matumizi ya awamu ya lazima mf bili za maji na umeme, matumizi ya kijamii, akiba ya mda mfupi kwajili ya malengo yamda mfupi na ya mda mrefu kwaajili ya ustaafu, dharura, urithi na namna ya kukuza mtaji kwa wote ikiwemo waajiriwa, waliojiajiri, vibarua, wanafunzi na watoto.
Umuhimu wa kuweka akiba hauni budi ya kuwekewa msisitizokwa kila mtanzania wakubwa na wadogo, hasa zaidi katika kipindi hiki ambacho gharama za maisha zimepanda nakuendelea kupanda na matumizi yanazidi kuongezeka.
Kuweka akiba na kukuza mtaji ni jambo gumu kwa makundi yote Yani wenye kipato na wasio na kipato kwa sababu mbalimbali zikiwemo kipato cha chini kulingana na matumizi yanayohitajika, matumizi makubwa kuzidi kipato na bila bajeti, kukosa elimu ya fedha hasa ya bajeti, akiba na kukuza mtaji napia upeo mdogo wa kujipanga kwaajili ya baadae. Hii hupelekea watanzania wengi kutokuwa na akiba ya kuwatosha angalau miezi sita bila kipato kama inavyoshauriwa na wataalamu wa fedha. Lakini pia njia zitumikazo kuweka akiba ni zilizopitwa na wakati ikiwemo vibubu, kutunziana, vikoba vya sanduku n.kambako hela haikui, haina usalama wa uhakika na ni rahisikuitoa na kupoteza malengo ya akiba.
Namna za kuweka akiba zimeongezeka na kuwa za kidigitali zaidi zinazorahisisha ufikiaji kwa kila mtu, usalama wa fedha, ukuaji wa mtaji na ukwasi. Kinachohitajika ni simu ya mkononi tu ya aina yoyote ilimradi nzima na elimu ya mifumo uo japo atakidogo kwa kuanzia.
Benki ni kati ya mifumo inayojulikana zaidi na inatoa namna nyingi yani akaunti tofauti kuendana na aina ya wateja kuanzia watoto, wanafunzi, wafanyabiashara, waajiriwa, wakulima, vikundi n.k na malengo ya wateja yawe ni ya mda mrefu au mfupi kwa faida. Benki pia hutoa mikopo ya aina tofauti pia kuendana na aina ya wateja na malengo ya wateja na namna pia za ulipaji zinazoweza kupunguza ugumuwake.
Elimu ya namna izi haijawafikia wengi na ivyo wengi huogopa benki na wengineo hutumia akaunti za kawaida yani savings account ambazo hazikuzi hela na hela hupungua kwa makato.
Zipo pia taasisi za serikali kama vile UTTAMIS ambayo inatoa huduma ya usimamizi wa fedha kukidhi mahitaji maalumu kwa wawekezaji binafsi wa vipato tofauti na taasisi. Uwekezaji binafsi ni jambo lisilo rahisi na linaleta uoga kwa wengi wetu na hapa ndipo tunapoona umuhimu wa taasisi kama hii wanaosimamia fedha yako na kukupatia faida. Wana mifuko mbalimbali ambayo inamfaa kila mtu kwa uwezo na malengo yake na hivyo kuwa ni msaada mkubwa kwa uhifadhi wa fedha, kukuza mtaji, ukwasi wa fedha yako na pia faida nyingine kama bima ya maisha ambayo husaidia katika vifo, ulemavu wakudumu n.k.
Mfuko huu umerahisishwa kuwafikia wananchi kwani wanahitaji simu ya mkononi tu na huweza kufikia menyu yake kufungua akaunti, kuchangia na huduma mbalimbali. Elimu yake hutolewa kwa mitandao yao ya kijamii, ofisi zao ambapo wanaandaa madarasa lakini pia inapaswa kuwafikia wengi zaidi na kwa namna rahisi inayoeleweka.
Mitandao ya simu nayo imekuja na mifumo mizuri na iliyorahisishwa ya kuweka akiba kwa mfano Timiza ya airtel na M-pawa ya Vodacom ambazo pia hutoa faida kwa akiba uliyoweka kwa kila mwezi, hurahisisha upatikanaji wa hela yako mda wowote na upatikanaji wa mkopo. Vikundi pia vinaweza kufungua akaunti kama vile M-koba kutoka Vodacom kwaajili ya vikoba ambapo hurahisisha ukusanyaji wa fedha, utoaji wa mikopo na uwazi kwenye mapato ya kikundi.
Hizi zote na nyingine zaidi ambazo tunaweza kujifunza kupitia mitandao yao ya kijamii, meseji za matangazo na huduma kwa wateja humuwezesha mtu kuweka akiba kwa malengo kuanzia hela ndogo muda wowote, kwa usalama, kwa faida na urahisi.
Kujiwekeza kwaajili ya ustaafu na ulemavu ni muhimu sana kuepusha umaskini na utegemezi. Waajiriwa wana faida ya kuwa na michango ya lazima yani pensheni ambayo huwasaidia katika ustaafu, kifo na ulemavu lakini pia mifuko hii ya pensheni kama PSPF inawafikia na wasioajiriwa pia ambapo wanaweza kujiunga na kuchangia kupata faida hizo pia apo baadae.
Hili ni jambo zuri hasa kwa wale ambao kazi na vipato vyao hutegemea nguvu huwaletea faida pale wanapokuwa hawana nguvu na hivyo hawana kipato. Pia kwa wale wenye vipato vidogo na kushindwa kujiwekea akiba ya kutosha pale ambapo wanakuwa hawana tena chanzo cha kipato. Mifuko hii ya pensheni pia ina namna za kuchangia ili kupata faida kama elimu ya watoto na faida kwa familia baada ya kifo.
Elimu ya kodi pia kwa wafanyabiashara na waliojiajiri ni ya muhimu sana kwani kulipa kodi huwasaidia kufuatilia vizuri nakujua mapato na maendeleo ya biashara zao na namna wanavyojilipa kutokana na biashara zao kwani wengi sasahivi huona kodi ni mzigo na wengine huikwepa ambapo ina madhara zaidi baadae kwao na kwa biashara zao ata baadae kwa vizazi vyao.
Ni jukumu la serikali, taasisi binafsi na watu binafsi kuelimishana namna hizi na nyingine zaidi kama ununuaji wa hisa, zitakazotusaidia kumudu maisha yetu katika hali zote za uchumi yani kuwa na usalama wa kifedha na pia kutengeneza uhuru wa kifedha, kuwakuza watoto kwa elimu hii majumbani na mashuleni ili iwasaidie na pia kusaidia watu kujikwamua nakuepukana na umaskini na madeni sugu hasa kwa taasisi zinazokopesha watu wa kipato cha chini kwa riba kubwa sana.
Upeo wetu wa kujipanga na baadae na kutengenezea vizazi vyetu vijao unapaswa kupanuka kwa kupata elimu zaidi yakifedha na kujifunza zaidi.

Upvote
5