Uhuru wa Kweli - Futa Uchawa

Uhuru wa Kweli - Futa Uchawa

Mejasoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
298
Reaction score
600
Ikiwa Leo tunatimiza miaka 63 tokea tupate uhuru wa Kisiasa mnamo tarehe 9. 12. 1961, na Bado Taifa Lina changamoto kubwa juu ya uhuru huo ikiwa imesalia miaka 37 tu kufikia karne Moja.
Kwa maono yangu uhuru wa siasa na bendera ulikua udanganyifu mkubwa na sio uhuru, ilikua mabadiliko ya sura za watawala tu na aina ya mamlaka ila utumwa ni ule ule,
Uhuru ule wa kisiasa uliua kabisa Taifa na kutengeneza makundi yanayohasimiana ndani ya nchi na hivyo kusababisha,
1) Utumwa wa kifikra
2) Ukosefu wa maarifa
3) Utegemezi wa kiuchumi
4) Fitna, unafiki na usaliti
5) Ubaguzi wa kichinichini
6) Uwizi, ubadhirifu, ufisadi wa rasilimali za nchi kwa mfumo wa kichawa
7) Umasikini wa Taifa
8) Kutamalaki kwa nishati hasi na nguvu za giza

Kwa hali hizo hapo Taifa haliwezi kuwa huru japo nchi inaonekana Ina bendera Moja ila Kuna mgawanyo mkubwa ndani ya Taifa na hivyo kuhatarisha usalama wa uhuru na umoja wa Taifa
Kingine tuna katiba na mfumo wa uongozi unaompa kiongozi mkubwa mamlaka ya kuwa dikteta (Ref: Alishashemaga Baba wa Taifa), kwa lugha hiyo tunachagua Rais anayefuata mapenzi yake na si ya Taifa.
Na hii katiba haikutengenezwa tu Bahati mbaya ila Chawa waliokuwepo kimfumo toka zamani za Mwalimu ndio waliohusika, Chawa hao ndio waliotaka Magufuli awe Raisi wa milele, na ndio hao hao wanaopiga kelele Mama anatosha Mitano tena.
Chawa ndio wanaendesha utekaji na mauaji
Chawa ndio washauri wabovu wa mfumo na viongozi wake
Chawa ndio maadui wa Taifa
Chawa ni wabinafsi mno
Jambo zuri ni kwamba
Chawa ni waoga, dhaifu sana, wanyonge mno, wakikosa mfumo wao,
ila wakibaki na mfumo unaowapa ustawi ni adui wa Taifa
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa sawa kutaja maadui watatu wa Taifa ila alikosea mno kusahau adui mkubwa kuliko wote ambaye ni Chawa/Uchawa
Huyu ndie anayeratibu Ujinga, Maradhi na Umasikini, fitna, majungu na orodha ni ndefu sana
Ubaya Chawa wamejikita sana kwenye CCM wakakiondoa kwenye hadhi ya kuwa chama Kiongozi enzi ya Nyerere, wakakishusha kuwa chama Tawala enzi za Mwinyi, Mkapa na Kikwete na ilipofika awamu ya Tano chini ya Magufuli Chawa wakapevuka na kujifanya chama kishuke hadhi kuwa chama Dola, kitu ambacho mwenyekiti wa mwisho wa Chama Tawala ( Jakaya Kikwete) alikikemea sana na kuwaonya makada wa CCM kufanya kazi ya kisiasa na sio kutegemea Dola na wafadhili ila kwa Bahati mbaya hawakusikia, ndipo chini ya Magufuli chama kikawa chama Dola haswa na kumfikiria kuwa na Raisi wa milele (Dikteta), Shukrani Mungu aliingilia Kati, lakini bado Kuna viashoria vile vile vya kurudi kule kule, kwa Sifa za mapambio zinazopazwa na Chawa sioni mama akiamua kupumzika karibuni, labda Mungu aingilie tena Kati.
Nyerere alikuwa na hekima ndio maana alielewa anatakiwa apumzike na Chawa ndio wanamponza akang'atuka,
Hivyo hiyo ilitakiwa Magufuli afanye hivyo,
Mama Samia anatakiwa afanye hivyo
kubwa zaidi kwa viongozi wa upinzani ambapo kwa bahati mbaya sana uchawa nao umejipenyeza huko wanatakiwa kufanya hivyo kama Nyerere, haswa Mbowe amabaye ndio kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani kwa sasa
kitu kikubwa waandae mfumo mzuri wa kiongozi na mapokezi ya hatamu za madaraka
Wahakikishe madaraka yanakuwa ni mamlaka ya kutimiza wajibu na majukumu na sio nguvu za kujinufaisha wao binafsi na watu wao wa karibu.
Uhuru wa ukweli ni kukataa Uchawa.
 
Kwanza kabla ya yote lazima tukubaliane kwamba iliyopata uhuru ni Tanganyika na sio Tanzania
 
Kwanza kabla ya yote lazima tukubaliane kwamba iliyopata uhuru ni Tanganyika na sio Tanzania
Ni kweli ila Chawa waliruhusu utokee Muungano usiokuwa na kichwa Wala miguu
 
Tanzania bila Chawa inawezekana?
 
Back
Top Bottom