Uhusiano kati ya malengo yako na matendo yako

Uhusiano kati ya malengo yako na matendo yako

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;

Tunaishi hapa duniani na maisha lazima yaendelee.Leo nimeona nilete mjadala kidogo kuhusu maisha yetu.Mjadala huu unahusu uhusiano uliopo kati ya malengo yako na matendo yako.Wengi wetu hatujui ila moja kati ya chanzo kikuu cha mkwamo katika maisha ni mgogoro au kupishana kati ya malengo yetu na matendo yetu.Wengi wetu tunakuwa na matendo ambayo hayaakisi malengo yetu kimaisha,kifamilia na hata kibiashara.Hali inapelekea kila wakati tuna kuwa katika hali ya sintofahamu.

Malengo nini?

Malengo katika ujumla ni mambo ambayo mtu anakusudia kufikia katika kipindi fulani kwa kutegemea fursa na rasilimali alizonazo kwa wakati huo.Katika tafsiri hii ni muhimu kuzingatia kwamba suala la msingi sana ni muda,uwezo na rasilimali..Malengo katika maisha yapo katika makundi matatu na hii ni kwa kutegemea mtazamo wako na uelewa wako.Kuna malengo ya kiafya,Kuna malengo ya kiuchumi na kuna malengo ya kijamii.

Malengo ya Kiafya
Katika maisha Afya ndio msingi wa kila kitu.Unapoishi bila kuwa na malengo ya kiafya una hatari ya kujikuta unafanya maamuzi ambayo yanaathiri afya yako kwa wakti mfupi au kwa muda mrefu.Ninapozungumzia afya nazungumzia pande zote yaani afya ya kimwili,kiakili na kiroho.Mtindo wako wa maisha ni lazima uendane na malengo yako ya kiafya.Tabia yako ya ulaji,mapumziko aina ya watu unaojihusisha nao,mahusiano yako ya ngono na mengineyo..Unapokuwa na malengo ya kiafya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kusimamia kwa umakini afya yako na kuhakikisha kwamba kila unachofanya kinaakisi na kinakupeleka katika kufikia malengo yako ya kiafya.

Kwa mfano aina ya ulaji unaweza kukupelekea katika magonjwa kama sukari na hata BP na magonjwa haya yanaweza kuathiri maeneo mengine ya afya yako.Ngono zembe inaweza kukupelekea kupata magonjwa ya zinaa na hata VVU na hii inaweza kuathiri kabisa mpango wa maisha yako.Ni jambo lililo wazi kwamba afya ikitetereka inaweza kupelekea hata kifo chako ambacho ni mwisho wa ndoto zako.

Malengo ya kiuchumi
Malengo ya kiuchumi yanahusisha zaidi mahitaji ya kuweka hali inayoweza kukupa uhuru na uhakika wa kipato.Katika eneo hili ni muhimu kuzingatia kwamba uhuru wa kipato ndio msingi wa furaha katika maisha.Unapaswa uwe na mipango ya kiuchumi ya muda mfupi,wa kati na muda mrefu.Kwa kuzingatia nafasi yako ya sasa ni muhimu kabisa ukaanda mazingira ya kiuchumi ya baadae kwa kufanya uwekezaji,kuweka akiba,kuanzisha biashara,kutafuta fursa,kujiongezea maarifa na kutafuta fursa mpya za kupata kipato.

Malengo ya kijamii
Wewe ni sehemu ya jamii na Jamii ni shemu yako.jE UNA MALENGO GANI ambayo yanahusika na jamii yako kama vile majirani zako,watu mnaosali pamoja,familia yako na dugu zako wengine.Ni muhimu kuhakikisha kwamba kil jambo unalofanya kwa ajili ya kujenga mahusiano yako ya kijamii unalifanya ukiwa unatambua kwa kina lengo hili.Matendo yako lazima yaakisi lengo hili la kujenga aina ya jamii ambayo inakuhakikisha furaha amani na mazingira bora ya kuishi


Karibu tujadili zaidi jinsi namna matendo yetu yanavyoathiri malengo yetu katika maisha yetu.
 
Nikisika malengo moja kwa moja naelewa ni ya kiuchumi. Hayo mengine siyazingatii
 
Back
Top Bottom