Uhusiano kati ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na vile vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi

Uhusiano kati ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na vile vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 (SARS Cov 2) na vile vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (HIV) vinafanana katika mifumo vinayoiathiri na pia tabia zake.

1. Virusi vya HIV vina Ribonucleic acid(RNA) halikadhalika virusi vya Corona vina RNA.
2. Vinaathiri mfumo wa kinga kwa kuathiri seli hai nyeupe (T-cells /lymphocytes) ambazo hutumika kama walinzi wa mwili wa mwanadamu.

Kwa majibu wa maelezo ya Dr Rogers Scheult ambaye ni mwanzilishi mshiriki wa MedCram.com virusi hivi yaani vinavyoeneza ugonjwa wa COVID-19 na vile vinavyoeneza ugonjwa wa Ukimwi vina uwezo wa kudhoofisha mfumo wa kinga wa mwanadamu (can affect immune system).

Tafiti hii inaonesha mawanda mapana zaidi yanayoathiriwa na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa COVID-19.Hii inatufanya kumaizi kuwa virusi hivi havivamii na kuathiri mfumo wa upumuaji tu ila pia vinaathiri T-cells, CD4 na pia CDA.

Tafiti zinaonesha kuwa virusi vinavyoeneza ugonjwa wa COVID-19 vinapovamia T-cells ndipo vinapojizalisha(replicate) maradufu.

Kulingana na maelezo ya Sadhguru(MOI) Virusi vinavyoeneza ugonjwa wa COVID-19 vinavamia T-cells kama vile vya Ukimwi (HIV) ila siyo katika muundo unaofanana, virusi hivi vinavamia mawanda mengine muhimu ya mfumo wa kinga ya mwanadamu.

Msisitizo anaoutoa Sadhguru ni wanadamu kuendelea kuimarisha mifumo yao ya kinga pamoja na kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu.

Sadhguru yaliendelea zaidi kusema kuwa wapo watu wanaojiamulia kutojali pamoja na maelekezo yanayotolewa ila aliunga jambo moja kuwaasa ambalo ni hili:

"USISEME MIMI SIJALI AU SIOGOPI KUFA NA KUKIUKA TARATIBU ZA KUJIKINGA KWANI UTAKUWA NI TATIZO UKIWA HAI NA HATA UKIFA NI TATIZO KWANI HATA MIILI YA WAATHIRIKA BADO INAWEZA IKAENDELEA KUENEZA UGONJWA HUU".

Msisitizo hapo niliouona ni kuwa kutojali kwa mtu mmoja kinaweza kuwa hasara kwa wengi hivyo tusipuuzie.

Huwa napenda sana kufuatilia hatuna za huyu Mystic figure of India (MoI) aitwaye Sadhguru na miongoni mwa mambo mengine aliyoyasema yananifanya niendelee kusoma zaidi ili kuelewa ni kuwa wanawake wapo sehemu nzuri zaidi kutokana na mfumo wao mzuri wa kinga ya mwili (well regulated immune system) na hivyo virusi hivi vinavyoeneza ugonjwa wa COVID-19 vinaonekana kuathiri na kuathiri zaidi wanaume (not accurate but it is largely men who are dying).

Aliendelea kusema kuwa kuna watu wengi ambao wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 na kutoonesha dalili yoyote ile ndani ya wiki tatu, watu hawa wakiachiwa kuendelea kutembea sehemu tofauti wanaweza kueneza kwa wengine wengi zaidi wakidhani wapo salama na kwa maana hiyo ni muhimu kukaa nyumbani na kuzingatia maelekezo ya kujikinga.
 
Si kweli SARS COV 2 vinafanana na HIV kwa mujibu wa maelezo yako, ufanano wao ulitakiwa kuishia kwenye RNA tu. Japo pia bado tofauti ni kubwa HIV ana RNA molecules mbili na zote ni positve sense RNA SARS COV 2 ana RNA molecule moja tu katika viral capsid yake.

HIV hana proofreading mechanism after its replication (A mechanism to correct any wrong added nitrogenious base) as the result of high mutation rate. Cov2 hana mutation rate kubwa kwa sababu anafanya molecular checks.

SARS COV2 has a significantly large genome compared to HIV and many other viruses, (34Kb) nucleic acid size.

According to viral tropism Cov2 hashambulii Immune cells, instead anashambulia lung cells, alveoli, na pia RBCs ambapo husababisha Iron ion dissosiation from the heme molecule ambayo husababisha oxidative stress reaction na baadae cytokine storm.

Point of correction.
Unaposema T cells dont mean lympocytes,
Lymphocytes ni white immune cells kama B cells, T helper cells, na Natural killer cells.

Ukisema CD4 dont mean it as a cell CD4 na CDA sio cells, hizi cell surface moleules (cluster of differention) /CD molecules ambazo hupatikana kwenye cells za kinga ikiwemo T helper cells, B cells, and antigen presenting cells (APCs) kama macrophages na dendritic cell.

Written by Modern scientist

For more information
Follow. IG. Scientist_melch
melchscience@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kweli ulichosema kuwa nimeandika HIV virus vinafanana na Virusi vya Corona.
Soma kichwa cha andiko vizuri kina neno " uhusiano"..
Halafu mbona sijasema popote CD4 na CDA ni seli?unayayolea wapi hayo?
I stand to be corrected
" Je hakuna huo uhusiano wa maeneo yanayoathiriwa na aina hizo mbili za virusi?"( Weka hili sawa ili mamlaka isitumike kukataa tafiti zilizopo"
Nimepitia tafiti kadhaa kabla ya kuandika andiko hili na tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaathiri mfumo wa kinga ya mwili na virusi vya Ukimwi navyo huathiri mfumo wa kinga ya mwili pia.
(Onesha upotofu wa tafiti hizo) nitakuja kukivuta hili andiko ikiwa linapotosha.
 
Back
Top Bottom