Uhusiano Kati ya Vyombo vya Habari na Intelijensia

Uhusiano Kati ya Vyombo vya Habari na Intelijensia

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Intelijensia inaelezwa kama taarifa za siri zinazokusanywa,kuchakatwa na kuchambuliwa ili kuwezesha serikali kuchukua maamuzi fulani ili kuongeza ufanisi. Umuhimu wa intelijensia haupimwi kwa uwezo wa wingi au usiri wa taarifa unaopatikana bali katika uwezo wa zile taarifa kupelekea maamuzi sahihi kufanyika. Kwahiyo kama taarifa nyingi na muhimu zikipatikana lakini maamuzi mabovu yakachukuliwa then intellijensia imefeli.

images (3).jpg

Tofauti ya Intelijensia na taarifa ni USIRI. Maana taarifa inawezwa kutafutwa kwa uwazi na kusambazwa kwa uwazi ila intelijensia inasakwa kwa usiri mkubwa na kusambazwa kwa usiri sana.

Vyombo vya habari kwa miaka mingi vinaonekana kama nyenzo tu ya taarifa ambazo zinapatikana kwa raia yeyote hivyo hazina madhara kwenye ujasusi. Lakini kitu ambacho wengi hawafahamu ni kwamba mataifa mengi yanatumia vyanzo vya habari kama maeneo ya kusaka taarifa za siri dhidi ya maadui wa nchi au viashiria vyenye hatari au faida kwa nchi hasa kiuchumi.

Moja ya mfano mkubwa kabisa ni shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) ambalo kwa miaka mingi sasa linatumika kama kiwanja cha kusaka taarifa za kijasusi ulimwengu mzima na kusukuma mbele propaganda za taifa lao kwa ajili ya maslahi mapana ya kiuchumi na kisiasa.

Kwenye vita ya pili ya dunia BBC ilitumika kama chanzo cha kusaka taarifa muhimu kutoka uwanja wa vita hasa kwa kunasa mawasiliano ya majeshi ya Axis (Germany,Japan na Italia) na kuzituma kwenye wizara ya ulinzi/Habari ili waweze kufanya maamuzi ya kijeshi.

Media za Tanzania hazipo kiutafiti bali kutoa taarifa tu na hapa ndio inanisukuma kuandika uzi huu. Ni mara chache sana unakuta media za Tanzania zinaleta habari za kiuchunguzi ukiachana na wachache kama enzi hizo Mama Terry au Jerry Muro,Kubenea,Jesse kwayu etc lakini TBC ambayo ndio inajukumu kuu kuwa media leader sababu ni chombo cha umma kinapwaya sana hapa. Habari nyingi unakuta ni za Warsha,makongamano,hotuba etc ila ni ngumu kukuta taarifa za kiuchunguzi kutoka kila kona ya dunia.

images (2).jpg

Angalau Media za Kenya mfano KTN na Citizen nimeona wamejitahidi katika eneo hili. Wanakua na habari za kiuchunguzi nyingi ambazo wanazileta kwenye kadamnasi na zingine kwa siri kusaidia vyombo vya ulinzi kuchukua hatua.

Nimewahi ona documentary moja kuhusu utesaji kwenye sober house (Eneo la kutibu kisaikolojia walioacha vilevi mbalimbali) yaani wamevaa kamera za siri na vinasa sauti na mwingine kujifanya teja yote ili wakusanye taarifa na mwisho wa makala wakapata taarifa muhimu ambazo baada ya documentary ile watu walitumbuliwa na serikali kuweka usimamizi mkali wa hizo sober house.


Investigative journalism juu ya kifo cha saitoti

Tukirudi Tanzania media nyingi sana zimekalia kutafuta habari za umbea,udaku,ngono etc ilihali nchi ina vivutio,taarifa za kutisha na kustaajabisha kabisa ambazo zingeletwa kwenye jicho la umma lingesaidia hatua nyingi kuchukuliwa. Lakini ukiingia youtube, channel 90% ni za udaku kuhusu video za menina!!, sasa kwa staili hii tutajuaje chanzo cha ukimwi kusambaa, Ajira kukosekana, Kilimo kukosa tija n.k ilihali vyombo vya habari haviingii ndani kuchimba kupata taarifa za kina.

Kwahiyo niseme tu kuna uhusiano mkubwa kati ya Vyombo vya habari na intelijensia hivyo ningeshauri hasa TBC ijikite kwenye kutafuta taarifa za kina zenye tija kwa taifa kuliko kukamia kwenye propaganda za kisiasa.

Dunia ya sasa imehama kutoka vita za kisiasa kuelekea za kiuchumi na teknolojia. Sasa TBC ilipaswa ifanye propaganda za kiuchumi kwa kuiuza Tanzania kwa dunia kuhusu taarifa za kustaajabisha mfano kikombe cha babu enzi zile ili Tanzania angalu inufaike na utalii au wawekezaji n.k kuliko kudeal na habari za kisiasa tu zisizo leta faida yeyote kwa taifa. Wajifunze kwa BBC ambayo ni zaidi ya media ya kawaida.

Naomba kuwasilisha

images.jpg

Cc: Malcom Lumumba Kiranga Mshana Jr Chige Wick Daimler Richard lifecoded mtu chake mpite huku.
 
Kibongo bongo bado sana..duniani huko watu wanahamia kugather information through Artificial intelligence sisi huku hata hatuna wazo. Dunia inaelekea kwenye smart life, smart world wakati hata Analogy hatujaweza imudu!
 
Kwanza naomba nikuambie kuwa bbc wanafanikiwa kwa asilimia mia kwa sababu wao kila nchi au bara wana waandishi wa habari na wanaripoti kwa chochote kile kinachotokea ni tofauti na sisi kwetu wao wandishi wa habari wanakimbilia hapa hapa dar es saal am station zilipo na wamejitahidi sana ni mikoani na tena sio kila siku tunapata taarifa maana wengine hata vitendea kazi hawana ila wanajiita waandishi wa habari.

Kinachokwamisha kupata habari zaidi ni kuwa radio za kwetu hapa hazijajitanua zaidi kuweka watoa ripoti wao kutoka nchi za nje maulaya huko na hata wakizipata zile muhimu tuu tena kwa kipindi maalumu
 
Media za bongo zinakatisha tamaa kutazama/kusikiliza.
Tofauti kubwa sana hasa uangaliapo taarifa ya habari ya TV station za wenzetu Kenya na zile za TV zetu za hapa Bongo, ni aibu tupu !!
Tena kwenye "developing" stories sisi ndo zero %.....
 
Gatizo la media ni kubwa sana hapa BongolAnd.

1. Serikali kuminya uhuru wa habari.
2. Rushwa ni kubwa sana.Mtu akipata taarifa anahonga ili isiende mubashara na hivyo inaharibu
3. Waandishi wengi ni waoga.wanaogopa na hawana confidence.
4. Teknolojia kama vile kamera za siri kwa Tanzania hakuna au kuna upungufu na pia hawajui kuzitumia.
5. Watanzania wanaogopa kutoa ushirikiano kwa media.Yani mtu hataki ajulikane na aonekane mubashara. Hata hivyo kuna uwezekano wa kuweka kivuli kwenye sura kama mhusika hataki aonekane live.Niliiona hii kwenye realitymovie inaotwa bad grandpa.waigizaji wanakuja wanaleta vituko huku wanarekodi wote mliopo.Baadae wanawataarifu iliabaye hataki sura halisi ionekane anawekewa kivuli usoni.
 
Mkuu zitto junior nilishindwa kurejea jana mida yetu ile. Nilifanya ziara ya kukagua vilinge kuona athari za mvua chombo kikakwama mahali. Nimekwamuka alfajiri huwezi amini.

Turudi kwenye mada

Nimelisoma andiko lako kwa kutulia. Ni zuri na linafikirisha. Nina machache ya kuchangia. Nitachangia kwa weledi na katika uhalisia wake..
Kama taifa kuna mahali tumekengeuka na kupotoka. Tulifanya kosa kubwa sana pale tulipoacha ujuzi ufanye kazi na kuipa siasa thamani kubwa isiyostahili.

Madhara yake ni ninini katika hili?
ujuzi unakuwa hauna maana tena. Siasa ndio inageuka ajira
Siasa ndio inageuka kufaulu
Siasa ndio inageuka kufanikiwa
Siasa ndio inageuka heshima
Siasa ndio inageuka mustakabali maono na mitazamo
Watu wanaacha ubunifu
Watu wanaacha ujuzi
Watu wanaacha weledi
Watu wanaacha maono
Kila mtu anakimbilia siasa kwakuwa siasa inalipa na siasa ni kila kitu

Inapofikia hapo huwezi kuwa na intelligence kwenye media
Huwezi kuwa na investigative journalism
Huwezi kuwa mwandishi jasusi na risk taker
Chochote utakachofanya ni kwa manufaa ya fualni na tumbo lako... Yani unasubiri kupenyezewa makombo ya habari toka pande zinazokinzana kugombea maslahi fulani ya kisiasa
Hakuna chombo cha habari kilicho tayari kuwekeza kwenye ujasusi wa habari wala kuajiri waandishi wenye weledi ujuzi na maarifa juu ya habari nyeti za usalama wa taifa kwa muktadha wake....

Habari zetu za kiuchunguzi na za usalama kwenye ujasusi zinachekesha na sometimes kutia kinyaa... Ni habari za kupenyezewa na makundi kinzani... Hazina mwendelezo hazina misingi... Mwandishi anaitwa anapewa kibunda na habari iliyokwisha pikwa kisha naye anaenda kuirusha kama habari ya kiuchunguzi
Nitarejea.....
 
Kenya alikupo yule jamaaa wa jicho pevu, bahatimbaya system imeshammeza na sasa kajikita kwenye siasa.

Bongo hii tumebakia na wapiga panda wa mfalme. Ni mwendo rais kasema, waziri kasema, ......
 
Kenya alikupo yule jamaaa wa jicho pevu, bahatimbaya system imeshammeza na sasa kajikita kwenye siasa.

Bongo hii tumebakia na wapiga panda wa mfalme. Ni mwendo rais kasema, waziri kasema
Ndio shida tuliyo nayo kwasasa. Intelijensia yetu haipo kwa ajili ya nchi bali ipo kwa ajili ya kaliba fulani ya watu
 
Mkuu Mshana Jr nimeelewa sana concept yako ya siasa kuvamia kila kitu ikiwemo media kumeua uweledi kwenye hizi taasisi na zimebaki kufanya propaganda za kisiasa. Sasa kwa ushauri wako unaona tunatokaje hapa tulipo ili tuwe na taasisi imara za habari zilizo huru,bila mrengo wa kisiasa na kuleta habari za kiuchunguzi kwa maslahi mapana zaidi ya kiuchumi na usalama wa taifa letu.

Nitangulize shukrani
 
Mkuu Mshana Jr nimeelewa sana concept yako ya siasa kuvamia kila kitu ikiwemo media kumeua uweledi kwenye hizi taasisi na zimebaki kufanya propaganda za kisiasa. Sasa kwa ushauri wako unaona tunatokaje hapa tulipo ili tuwe na taasisi imara za habari zilizo huru,bila mrengo wa kisiasa na kuleta habari za kiuchunguzi kwa maslahi mapana zaidi ya kiuchumi na usalama wa taifa letu.

Nitangulize shukrani
Asante zitto junior kwanza ni lazima tutambue dhima ya intelijensia ya nchi ninini. Je, ni kulinda mfumo ama taifa?

Lakini pia tunahitaji kuwekeza sasa kwenye vyuo vya habari vyenye ujuzi weledi na maarifa kuhusiana na intelijensia. Tuwe na wwnahabari walioenda shule wabunifu na walioshiba elimu.

Tunahitaji pia kama taifa kutenganisha siasa na ujuzi. Ifike mahali siasa iwe na mipaka. Ifike mahali inapoishia siasa ujuzi uchukue hatamu
 
Back
Top Bottom