Uhusiano Kati ya Vyombo vya Habari na Intelijensia

Mkuu nashukuru kwa kuniita, nakubaliana na hoja yako , miaka ya nyuma baadhi ya magazeti yalikua yanafanya hivi hata TV km mfn uliotoa lkn kwa sasa mkuu wanaogopa kukutwa mabwepande au coco beach
 
Bado tuna safari ndefu sana kwenye hili... Bado hatuna vyombo vya habari vilivyo tayari kuwekeza kwenye uzugaji (camouflage) kuigiza ujuzi fulani kwa nia ya kuchimba na kupata habari... Mtu kujifanya KULI bandarini, mfagizi hospitali, karani ofisini, mfanyabiashara nknk kwa siku ama hata wiki kadha ili tu kupata undani wa habari kamili
 
 
Hahahaha, investigation journalist inahitaji mbinu na vifaa, mfn wako ni km yule Mtetema aliyefanya documentary ya VIUNGO VYA ALBINO ,sasa hao wa kwetu uwekezaji mdg

Ila kubwa zaidi historia kdg sio nzuri, hasa waandishi wa habari hizo ,mfn km yaliyowakuta akina Katabaro na scandal ya loliondo, Azory na Kibiti na wengineo

Kifupi habari za kichunguzi ukiingia deep sana unakua ktk wkt mgumu

Lakini pia ujue ,media house zetu nazo zina nyeti ila kuzitoa sasa, nimewahi kuwa ktk media house kadhaa hapo nyumbani najua kuna news nyingi hazitoki
 
Nafikiri media nyingi za Tanzania kimtazamo yakinifu zimekwama. Mfano mwepesi tujaribu kuangalia vipindi vya kwenye TV, ajabu kubwa utaiona! Kwa sababu takribani vituo vyote vya TV taarifa zao zinafanana, na hakuna vipindi vya maana.

Walichobaki nacho ni kuonyesha miziki, tamthilia, siasa na udaku. Ajabu zaidi hata vituo vipya vya runinga vikichomoza bado hawana jipya! Wanabeba tamaduni ileile ya TV kongwe.
 
Kwa mtazamo wangu, Tanzania tuna wapasha habari wa warsha, makongamano, ziara, nk. Wanahabari na wachambuzi wa taarifa ni wachache sana. Kwa nini? Nitawasilisha hoja tatu kwa sasa:

1. Elimu. "Waandishi" wengi walioko kwenye vyombo vya habari, elimu yao aidha siyo kwenye uandishi au ni ngazi ya cheti. Wanaomaliza ngazi za digrii/shahada wanaenda kwenye shughuli/tasnia nyingine. Hata elimu inayotolewa bado haijafikia viwango vinavyohitajika. Ukiangalia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, SJMC, asilimia kubwa ya mtaala wake ni nadharia, na kujifunza kwa vitendo ni asilimia ndogo sana. Tasnia ya habari inahitaji wabobezi wenye misingi ya tasnia nyingine kama uchumi, siasa, sayansi, usalama, saikolojia, nk. Ikibidi mwaka mzima wanajikita kwenye tasnia moja wapo na kisha miaka inayofuata wanajifunza kuwa wanahabari katika tasnia hizi.

2. Soko la habari: Habari za kiuchunguzi ni ghali kwa upande wa muda, rasilimali watu, fedha, nk. Vyombo vya habari vya Tanzania vinaangalia biashara (siwalaumu) na habari zitakazo waingizia fedha zaidi ili waendelee kujiendesha. Soko la habari linazidi kupata misukosuko ya kifedha kwa kuwa hadhira yake inazidi kushuka. Mtu kununua gazeti kusoma habari ambazo anaweza kupata bure kwenye mitandao ya kijamii, ni ngumu sana -- hasa ukiangalia uchumi wetu. Wenye vyombo vya habari kuwekeza kwenye habari za uchunguzi zitakazo wagharimu muda, watu, fedha, usalama wao wenyewe, nk., ni ngumu sana ukilinganisha na kutuma mwandishi kwenye warsha mbili au tatu kwa siku, na huko anaweza kupata 'bahasha ya khaki', analeta habari kama tatu kwa siku na husumbuki kufuatiliwa na kuhatarishwa maisha yako.

3. Matokeo (Consequences): Dhana kuu ya kuibua matatizo au maswala hatarishi kwenye jamii, ni ili vyombo/ watu husika vichukue/wachukue hatua. Pale mwandishi wa habari au mchambuzi wa taarifa anapowekeza rasilimali zake na kujitoa mhanga kuleta taarifa hizi kwenye uso wa jamii, halafu hakuna hatua stahiki zinazochuliwa, badala yake anawindwa kama mwizi, hukatisha tamaa. Lakini wakitoa habari za michezo, udaku na ngono, hawasumbiliwi na taarifa zao zinanunuliwa, wanaona bora waendelee na habari hizi. Mpaka leo magazeti yanayonunuliwa kwa wingi ni magazeti ya udaku na michezo. Hata humu jamvini, nyuzi zenye michango mingi ni kwenye majukwaa ya MMU na michezo.

Kiini na matokeo ya yote haya ni aina ya jamii tuliyonayo. It's a vicious cycle. Nilizungumzia hii dhana ya aina ya jamii tunayoijenga na matokeo ya uongozi, kwenye bandiko langu: Are we building demigods or future victims?
 
Sure Si Waafrica tunachangamoto sana kuna mtu nilimsikiaa anaongea anasema Tanzaniaa ni nchi ya 2 ikianza Marekan katika kutumiaa mtandao wa Instagram lakini kwa matumiz yasiyo sahihi ni kuchek umbea na porn basiiii
Kibongo bongo bado sana..duniani huko watu wanahamia kugather information through Artificial intelligence sisi huku hata hatuna wazo. Dunia inaelekea kwenye smart life, smart world wakati hata Analogy hatujaweza imudu!
 
Huyu jamaa yuko poaaa sana na anajuaa kuinvestigate ni balaa napenda sana makala zake na namfatiliaa sana
Kibongo bongo hakuna hii watu wanajiita wanaharakat lakin wamefichama mitandaoni
Huyu jamaa ni hatari sana yaani upelelezi wake unaweza dhani ni Afisa usalama wa taifa
 
Mkuu wewe ni great thinker..... Hoja yako hii nimeielewa sana. Kwa kutambua hili unaona suluhisho ni lipi kuvunja hii vicious cycle ya jamii yetu.
 
Nadhani mfumo tulio nao Tanzania ndio unaosababisha waandishi wetu kushughhulika na mambo yenye uzito mdogo na yasiyosaidia sana nchi kubaini uhalifu wa aina mbali mbali

huenda mfumo huu unajenga hofu ya wanahabari kuchimba maovu yaliyofichika,kwa hofu ya kukosa ulinzi kama ikitokea labda wamechimbua habari Fulani hatari

Labda ifike mahali waandishi wapewe kipaumbele na waachwe wafanye kazi yao kwa uhuru lakini pia wawe motivated kwa kupewa ulinzi wa hali ya juu,wahakikishiwe usalama wao,huenda hiyo ikasaidia kupata habari zenye uzito na kusaidia nchi katika kutokomeza baadhi ya maovu yanayoweza kutokomezwa ikiwa yataanikwa hadharani.
 
Ukiangalia media za nje mbali na taarifa za kiutafiti ila n kama propaganda war machines.....angalia jinsi aljazira inavyoreport juu ya north Africa ,au arabs world achilia mbali inavo weaponise taarifa dhid ya Israel.....utaelewa nn media kaz zake....
Lakin saa ivi angalia how China media vs Western ...jinsi China inavotumia media kulinda heshima, kuinfluence na propaganda nyingine....


Yaan mkuu hapa naungana naww100%
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…