Uhusiano ovu (unholly alliance) baina ya Alexander Mnyeti na wakili Mutalemwa Kishenyi

Uhusiano ovu (unholly alliance) baina ya Alexander Mnyeti na wakili Mutalemwa Kishenyi

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Moja ya matatizo ya serikali yetu ni kutokufuatilia kwa makini utendaji wa watumishi wa umma na inapofikia watumishi wakijipanga kwenye vikundi vyenye nia ovu na vinavyojiamini basi ofisi za umma zinakuwa sawa na madanguro ya kukusanya fedha na kuhujumu haki za wananchi.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye mkoa wa Manyara kipindi ambacho aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Alexander Mnyeti yeye alikuwa kwenye kundi la mkuu wa kaya basi yeye alifanya yake na watumishi chini yake walivyoona hivyo na wao wakaendelea kufanya yao.

Mmoja wa watumishi hao ni Mutalemwa Kishenyi wakili mwandamizi aliyekuwa kwenye ofisi ya mashtaka ushirikiano kati ya huyu wakili na Mnyeti pamoja na watumishi wengine kwenye ofisi ya mkoa ulifikia mahali ambapo wenye haki walishtakiwa na wenye pesa na utayari wa kutoa hongo wakosaji waliachiwa na ushirikiano huu ulitesa na kudhalilisha wananchi wengi sana.

Sio ajabu baada ya Mnyeti kuondoka kwenye nafasi yake ya ukuu wa mkoa haikuchukua muda wakili Kishenyi kukamatwa na Takukuru kwa kosa la kuchukua rushwa ya sh 5 milioni ili kumsaidia mtu aliyekwepa kodi nyingi za serikali.

Hakika kama jamaa yake angelikuwa mkuu wa mkoa Basi Wakili Kishenyi angelipangua kukamatwa huko kama hujaelewa hali hiyo ndio inaitwa nikune huku nikukune kule na hapa hatuna budi kuwapongeza TAKUKURU kwa hatua dhabiti ya kumnyaka mheshimiwa huyu mkware aliyetesa wananchi wengi kwa tamaa yake ya pesa watu kama hawa hawakutakiwa kuwa karibu na ofisi za umma.

Duru zinasema wakili huyu kabla ya kwenda Manyara kukutana na Mnyeti alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya mashtaka pale mahakamani Kisutu jijini Dar es salaam, kule tabia yake ya tamaa ya pesa, rushwa na hongo ilikwishadhihiri na inasemekana ili kusevu ngoma mkubwa mmoja alimhamisha na kumsukumia Manyara ambapo ndio balaa lilipomkuta ubia kati ya waheshimiwa hawa wawili ulikuwa balaa na kutesa wananchi wengi.

Imeelezwa kwamba yupo jangili aliyekubuhu aitwaye Gerald Joseph Kashiro ambaye baada ya kuondoka Mnyeti na Kishenyi kukamatwa yeye huyu alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kupatikana na nyara za serikali hivyo nachelea kusema kuwa kama miamba hii miwili ingekuwepo jamaa mida hii angekuwa huru huko Emboreet/Simanjiro akipiga bia na nyama za mishkaki ya twiga.

Shukrani nyingi na pongezi ziende kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa aliyekuja baada ya Mnyeti,Joseph Mkirikiti huyu alisaidia sana kukomesha vitendo vya ujangili vilivyokuwa vikiendelea mkoani Manyara huyu hakuwa na mchezo katika muda mfupi aliokaa madarakani alisimamia vyema rasiliamali za nchi na alichukia rushwa kwa vitendo.

Ushauri kwa wakili enenda madhabauni utubu dhambi zako mapema maana ulikamatwa bayana (red handed)na wanaokudanganya kwamba watakusaidia usiwasikilize maana wanakula pesa zako bure.

Pongezi kwa watumishi wa TAKUKURU kwa kukataa pendekezo lako la “tuyazungumze “maana tunaifuatilia kesi yako kwa ukaribu sana tunaujua utaratibu wa wanasheria kulindana kwenye mazingira hayo ila safari hii muhimu haki itendeke ili ipatikane funzo adhimu.

Tunawashauri Wanasheria/ Mawakili wengine kulinda heshima zao tuko hapo kwa pembeni tunafuatilia kwa umakini.

Nyooooo wewe si mtaalamu wa kupewa pesa kujinufaisha na kuwabambikia watu wema kesi za uhujumu uchumi? Laana hii haitakuacha salama jiulize nini kilikupeleka saa mbili za usiku kushobokea kupokea mlungula laana hiyo hiyo itakupeleka gerezani na wakati umefika ujitajirishe kunyea ndoo! dadeeeki.

Mwisho

E7D071DB-462C-4E82-9F9A-B15B54E8E4A5.jpeg


95C1853B-418E-4E1E-ADAD-4892AE76448F.jpeg


31E7CC12-EC10-4A99-ADAA-31B4CBBACA3E.jpeg
 
Hii Nchi ngumu sana hii tabia ya kulindana lindana na kupeana peana madaraka inaliangamiza na kuliuumiza sana Taifa hili adhimu.

Lazima tubadilike na kuleta katiba mpya itakayo toa muarobaini juu ya jambo hili vinginevyo itatuchukua miaka 100 kupata maendeleo.
 
Back
Top Bottom