Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Irene alikutana na upinzani mkubwa kwenye hatua za awali za uamuzi wake huu kutoka kwa wazazi wake ambao hawakutaka ahamie huko, lakini kutokana na uwepo wa baadhi ya ndugu zake nchini Marekani, wazazi wake waliamua kumruhusu ili aende kupigania ndoto yake hii kubwa.
"Hakikisha unakunywa maziwa ya moto kisha pumzika" ni sentensi ya mwisho ya baba yake akizungumza na Irene february 24, 2022 akiwa Nairobi.
Baada ya hapo sauti ya Irene haijawahi kusikika tena.
Tukio hili lilianzaje?
Baada ya kuhamia Marekani, Irene Munga aliishi kwa kaka zake Chris Munga na Kennedy Wainaina kwenye mji wa Idaho city - Meridian.
Hapo ndipo alipokutana na Nathan Hightman (39) kisha kuwa wapenzi. Uhusiano wao ulianzia kwenye mtandao wa Craigslist unaohusika na matangazo ya ajira, nyumba pamoja na bidhaa zingine.
Wapenzi hawa walianza kuishi pamoja pasipo wazazi wake Irene kufahamu.
Mashaka yalianza kuibuka mwanzoni mwa mwezi wa pili baada ya wazazi wake kupokea jumbe kadhaa kupitia mtandao wa WhatsApp zikisema kuwa amekuwa hapatikani kwa sababu alidondosha simu yake kwenye maji, aidha ujumbe mwingine uliandikwa kuwa " Nataka tu mfahamu kuwa wewe (baba) na mama ninawapenda sana"
Kwanini tusizungumze kwa video ya WhatsApp kama tulivyo zoea? Baba yake aliwaza sana, hata hivyo hakupata majibu.
Kati ya Mwezi February hadi Machi, Hightman alihamisha zaidi ya Tsh 8.6M kutoka kwenye akaunti ya benki ya Irene kwenda kwenye akaunti yake binafsi. Pia alifanya manunuzi ya zaidi ya milioni 7.5 kwa kutumia kadi ya benki ya Irene kwenye supermarket moja, kwa mujibu wa ripoti ya polisi wanao fuatilia kisa hiki.
Nathan Hightman
Kesi hii itasikilizwa tena mwezi Novemba mwaka huu.
Jitihada kadhaa zimefanywa na ndugu zake ikiwemo kutembelea vyumba vya kuhifadhia maiti mahospitalini, kwenda kwenye maeneo ya ombaomba wasio na makazi, kufanya maandamano pamoja na kuanzisha tovuti maalumu yenye jina la whereisirene.com lakini vyote havijazaa matunda.
Hightman anatuhumiwa pia kubadilisha nywila za benki pamoja na kufuta Barua pepe ya Irene. Kwa mujibu wa polisi, mambo haya yote yalifanyika kupitia IP address zinazo husianishwa naye.
Wasiwasi unazidi kuwa mkubwa kwa kuwa binti huyu hakuwahi kumtambulisha Nathan kwa wazazi wake ambao kwa sasa hawajui wataanzia wapi kumtafuta.
Utetezi wa awali wa Nathan unaonesha kuwa yeye pia hafahamu aliko binti huyo, na kuhusu kuhamisha pesa kutoka benki amesema alifanya hivyo kama njia ya kumfanya arudi kuzichukua pesa zake ili waweze kuonana tena.
CNN