Uhusiano wa Kamuzu Banda na Joyce Banda wa Malawi

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Hastings-Kamuzu-Banda-former-President-of-Malawi.jpg

Hastings Kamuzu Banda
Joyce Banda.jpg

Joyce Banda
Wiki iliyopita nilijaribu kuwapa historia fupi ya Rais wa kwanza wa Malawi Mh Kamuzu Banda. Leo ninataka niwapitishe kidogo kwenye historia ya Joyce Banda moja ya akina Mama waliowahi kutikisa Afrika na Dunia kwa ujumla na kujizolea umaarufu. Alijipatia umaarufu mkubwa kwa kupigania haki za Binadamu na alikuwa Mama msomi na mwanadiplomasia wa viwango vya juu. Kabla ya kuanza harakati alishawahi kuishi Nairobi nchini Kenya. Karibu uambatane nami katika makala hii inayohusu kuwa je, Joyce Banda na Kamuzu Banda ni ndugu?

Joyce Hilda Banda alizaliwa 12/4/1950 huko kijiji cha Malemia katika Wilayaya Zomba nchini Malawi. Baba yake alikuwa ni askari na moja ya wanamuziki wa brass band ya polisi huko Malawi. Pamoja na umaarufu mkubwa ambao Mh Joyce alijipatia lakini historia yake inasimulia kuwa alianza kusomea kwanza uhudumu/ secretary. Baadaye aliweza kusoma vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya Malawi huku akichukua shada tofauti. Aliweza kupata honory doctorate mwaka 2013 huko Jeonju University.

Joyce Banda baada ya kuwa Rais alijaribu kuiingiza Malawi na Tanzania katika vita ya maneno. Wajuzi wa mambo ya diplomasia wanasema vita hivi vya maneno vilichochewa na huyu mama mwanaharakati na mwanadplomasia pia. Taarifa zisizo rasmi wanasema Mh Kikwete akiwa Rais alisaidia sana Tanzania isiingie kwenye hiyo vita ambayo haikuwa na faida. Lakini wanadai kuwa Benard Membe akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanadiplomasia alikuwa tayari ameshapenyeza Watanzania Malawi kujua uhalisia wa mgogoro huu. Ninachokumbuka mimi kule kwetu Ileje mipaka yote ilikuwa imesimamiwa vizuri kuhakikisha kama kutakuwa na chokochoko zinazuiwa.

Kwa ufupi Mh Banda ana Shahada ya Sanaa katika Elimu ya Mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Columbus, na Diploma katika Usimamizi aliyopata nchini Italia. Katika umri wa miaka 25, alikuwa na watoto watatu na alikuwa akiishi mjini Nairobi, Kenya. Mwaka 1975, harakati za wanawake nchini Kenya zilimtia moyo Banda na aliwachukua watoto wake na kuachana na ndoa yake ya kwanza ya unyanyasaji. Mume wake wa kwanza alikuwa akiitwa Roy Kachale. Kati ya 1985 na 1997 Banda alianzisha biashara na makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ndekani Garments, (1985), Akajuwe Enterprises (1992), na Kalingidza Bakery (1995). Mafanikio yake yalimuongoza kuwasaidia wanawake wengine kufikia uhuru wa kifedha na kuvunja mizunguko ya kunyanyasika na umaskini.

Joyce Hilda Banda alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi kuanzia mwaka 2006 hadi 2009 na Makamu wa Rais wa Malawi kuanzia Mei 2009 kabla ya kuukwaa urais Aprili 7, 2012. Pia alikuwa Mbunge na Waziri wa Jinsia, Mambo ya Watoto na Huduma za Jamii. Kabla ya kushiriki kikamilifu katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Taasisi ya Joyce Banda (Joyce Banda Foundation), mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyabiashara Wanawake (NABW), Mtandao wa Viongozi Vijana Wanawake na Mradi Njaa. Alitajwa katika jarida la Forbes mwaka 2011 kama mwanamke wa tatu mwenye nguvu zaidi na ushawishi katika Afrika. Ni mwanzilishi na kiongozi wa Chama cha Watu (People's Party) kilichoundwa mwaka 2011, na kabla ya kifo cha Bingu wa Mutharika alionekana kuwa na uwezekano wa kugombea Urais wa Malawi katika uchaguzi mkuu wa 2014.

Joyce Banda alipata umaarufu zaidi kipindi cha Dikiteta Hastings Banda. Umaarufu huu ulitokana na Hastings Banda kwa kuwa alikuwa Rais wa Malawi huku Joyce Banda akiwa mwanaharakati wahaki za binadamu. Na umaarufu huo ulichagizwa hasa na majina ya mwisho kufanana hivyo ikatafsiriwa kuwa hawa ni ndugu.

Joyce Banda alikuwa mgombea mwenza wa urais wa chama cha Democratic Progressive (DPP) katika uchaguzi wa Rais Mei 2009, akigombea sambamba na Mutharika, mgombea urais wa DPP. Kwa mshangao ndani ya DPP, Joyce Banda na makamu wa pili wa rais, Khumbo Kachali, walifukuzwa kama makamu wa Rais wa DPP tarehe 12 Desemba 2010 kwa kile kilichojulikana 'kupambana na chama hicho’. Katika majaribio ya kumdhoofisha, Rais aliendelea kutoa majukumu ambayo awali yalikuwa chini ya Banda na kuyakabidhi kwa Callista Mutharika ambaye aliingizwa katika baraza la mawaziri mwezi Septemba 2011.

Uhusiano kati yake na Rais wa Malawi uliendelea kuwa wa wasiwasi kwa sababu ya Rais kujaribu kumpa nafasi ndugu yake, Peter Mutharika kama mwandamizi wa chama na Rais mtarajiwa. Ingawa Banda alitimuliwa kutoka nafasi ya Makamu wa Rais wa DPP pamoja na Makamu wa Rais wa pili Khumbo Kachali, aliendelea kuwa Makamu wa Rais wa Malawi kama ilivyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Malawi. Hatua hii ilisababisha wengi kujitoa DPP na kuunda mitandao ambayo ilimsaidia makamu wa Rais ili kusaidia ugombea wake wa urais wa Malawi katika uchaguzi mkuu wa 2014. DPP ilikanusha kujitoa kwa wengi na kusisitiza kwamba waliojitoa walikuwa wachache tu.

Baada ya kifo cha Mutharika, kulikuwa na hofu ya kugombea madaraka kufuatia taarifa ya Waziri wa Habari na Elimu ya Uraia, Patricia Kaliati, kuwa "mwenendo wa Joyce Banda ni katika kutengeneza chama chake cha upinzani kimsaidie katika kufanikiwa urais." Shirika la habari la Ufaransa lilitoa taarifa kuwa rais wa zamani wa Malawi, Bakili Muluzi, kusisitiza “utaratibu wa kufuata katiba,” akisema makamu wa rais lazima achukue madaraka moja kwa moja kwa mujibu wa katiba. “Natoa wito kufuata kikatiba, kwa ajili ya amani kuendelea na utaratibu.

Sheria za Malawi ziko wazi kabisa kuwa Makamu wa Rais anachukua madaraka” pale ambapo hayupo Rais. Tunatakiwa kuzuia hali ambapo kuna machafuko. Hebu tufuate katiba. Hatuna chaguo zaidi ya kufuata katiba. Ni muhimu sana kuwepo amani na utulivu,” alisema. Vikosi vya Usalama vya Malawi pia vilitaka katiba ifuatwe.

Chama cha wanasheria wa Malawi pia kilithibitisha kuwa chini ya kifungu cha 83 (4) cha katiba ya Malawi, Banda ndiye mrithi halali wa Urais. Aliapishwa kama rais mwanamke wa kwanza nchini humo Aprili 7, na kutoa wito kwa umoja wa kitaifa. Alipongezwa na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe .

Hoja yangu kubwa kwa leo ilikuwa ni kutaka kuwatoa wingu kubwa kichwani mwetu lililokuwa linataka kujua uhusiano wa Kamuzu Banda na Joyce Banda. Ninajua wengi hamjui, lakini ninataka nikujuze kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya Banda Rais wa kwanza wa Malawi na Joyce Banda. Hivyo si kweli kuwa Joyce umaarufu wake ulibebwa na Kamuzu Banda. Jina la Banda amepewa miaka ya baadae sana.

Majina yake halisi ni JOYCE HILDA NTILA, jina la Banda lilikuja baadae baada ya kuachana na mume wa kwanza. Kama ilivyo desturi ya watu wengi wakisha olewa huchuka majina ya waume zao. Joyce Hilda Ntila aliachana na mume wake wa kwanza mwaka 1981 na kuolewa na RICHARD BANDA aliyekuwa Ritired Chief Justice wa Malawi ambaye amefanikiwa kuzaa naye watoto wawili. Hivyo jina lake la Banda linatokana na mume wake wa pili na si Rais wa kwanza wa Malawi hayati Kamuzu Banda. Hata hivyo tunaona alishaanza mapambano hata kabla ya ndoa yake ya pili ambayo watu wamekuwa wakiusisha na harakati zake za kisiasa. Alianza mapambano hata kabla hajaolewa kwenye ukoo wa akina Banda.

Mwisho ijapo si kwa umhimu, baadaye baada ya kumaliza Urais alikamatwa kwa uhusishwa na mambo ya ubadhirifu. Lakii anahistoria ndefu, lakini kwa leo iliona nitoe tu majibu ya uusiano wake na Dikiteta Banda ili tuwe na uelea wa pamoja. Wiki ijayo nitakuletea uhusiano wa Peter Mutharika na Bingu Mutharika ambao wote wamekuwa Marais wa Malawi kwa vipindi tofauti.
 
Kuna siku nilikuwa karibu na ikulu ya Malawi kwa kazi maalum aise ilikuwa nusura nikamatwe
 
View attachment 1344936
Hastings Kamuzu Banda
View attachment 1344938

KUPATA VICHEKESHO KAMA HIVI ANDIKA BANDA KWENDA NAMBA 15667
 
ndio maana sa nyingione nawachukia wanaharakati huyu mama alisapoti ujinga wa ndoa ya jinsia moja
 
Back
Top Bottom