Uhusiano wa Madai ya PSSSF na mfanyakazi kung'ang'ania kwenye nyumba ya Taasisi

Uhusiano wa Madai ya PSSSF na mfanyakazi kung'ang'ania kwenye nyumba ya Taasisi

DPMVTCn

New Member
Joined
Oct 11, 2022
Posts
3
Reaction score
6
Naombeni ushauri, kuna mfanyakazi alikuwa mtumishi wa serikali aliazimwa kutoka serikalini na kufanya kazi kwenye Chuo fulani cha Private alikuwa Mwalimu na alikuwa Mkuu wa Chuo.

Baadae uchumi ulianza kuyumba kwani kilikosa wanafunzi na hatimae kufungwa!. Mkuu huyo alikuwa anaishi kwenye nyumba ya Taasisi kwa kulipia( alikuwa akikatwa kwenye mshahara).

Baada ya Chuo kufungwa aliendelea kuishi kwenye lakini hakulipa pesa yoyote ya kodi, wakati wa utumishi wake Kuna miezi Kama 10 contributions za PSSSF hazikulipwa zote asilimia 20, ikumbukwe pia baada ya Chuo kufungwa aliomba kurudi serikalini kwani alikuwa ameazimwa na hivyo amesitaafu akiwa serikalini.

Sasa ameleta madai ya PSSSF yake ambayo haikulipwa na alipewa notisi ya kukumbushwa kulipa Kodi na baadae akapewa notisi ya kukabidhi lakini anadai hawezi kukabidhi nyumba mpaka alipwe madai yake ya PSSSF kwanza kwani kule Kuna Gaps.

Hii kisheria imekaaje?.

Najarbu kufikiria Uhusiano wa kung'ang'ania kwenye nyumba na madai ya PSSSF upo wapi?
 
Naombeni ushauri, kuna mfanyakazi alikuwa mtumishi wa serikali aliazimwa kutoka serikalini na kufanya kazi kwenye Chuo fulani cha Private alikuwa Mwalimu na alikuwa Mkuu wa Chuo. Baadae uchumi ulianza kuyumba kwani kilikosa wanafunzi na hatimae kufungwa!. Mkuu huyo alikuwa anaishi kwenye nyumba ya Taasisi kwa kulipia( alikuwa akikatwa kwenye mshahara). Baada ya Chuo kufungwa aliendelea kuishi kwenye lakini hakulipa pesa yoyote ya kodi, wakati wa utumishi wake Kuna miezi Kama 10 contributions za PSSSF hazikulipwa zote asilimia 20, ikumbukwe pia baada ya Chuo kufungwa aliomba kurudi serikalini kwani alikuwa ameazimwa na hivyo amesitaafu akiwa serikalini. Sasa ameleta madai ya PSSSF yake ambayo haikulipwa na alipewa notisi ya kukumbushwa kulipa Kodi na baadae akapewa notisi ya kukabidhi lakini anadai hawezi kukabidhi nyumba mpaka alipwe madai yake ya PSSSF kwanza kwani kule Kuna Gaps. Hii kisheria imekaaje?. Najarbu kufikiria Uhusiano wa kung'ang'ania kwenye nyumba na madai ya PSSSF upo wapi?
kwa mujibu wa maelezo yako,naweza sema kuwa suala la kodi ya nyumba halihusiani na kutokuingizwa kwa michango katika mfuko wa hifadhi ya jamii,fuata taratibuza kumtoa katika nyumba kwa kushindwa kulipa kodi,pia kama wewe ni muajiri hakikisha michango yake mnaingiza ila kama wewe siyo mwajiri wake mwambie aandike barua kwenda kwa utumishi kupitia PSSSF juu ya tatizo lake.

japo na maswali yafuatayo;
kwa nini hamkuchukua hatua mapema hadi anastaafu katika nyumba ya taasisi ambayo siyo mwajiri wake?
kwani kiasi cha kodi ya nyumba kina lingana na michango ambayo haikuingizwa katika mfuko wa hifadhi ya jamii?makubaliano ya ulipaji wa pango au kodi baada ya kazi kukoma ilikuwa ipi?na anadaiwa kwa miezi mingapi?
 
kwa mujibu wa maelezo yako,naweza sema kuwa suala la kodi ya nyumba halihusiani na kutokuingizwa kwa michango katika mfuko wa hifadhi ya jami...
Kodi ya nyumba haifikii michango ya PSSSF, kuna difference kama ya 1.7 M. Pia uongozi uliokuwepo ulijisahau kushughulikia tatzo hili, Lakini pia hakukuwa na makubaliano yoyote ya kulipa Kodi baada Ajira kukoma isipokuwa mwenye nyumba alielewa kuwa kwavile alikatwa kwenye mshahara na basi angellipa cash kwasababu mshahara haukuwepo, lakini pia mwajiri bado anadai hana fedha kwasasa kwasababu Taasisi ili collapse na huyu anayedai yeye alikuwa Mkuu wa hiyo Taasisi, sasa kabla ya kumulipa PSSSF yake mwajiri ana nguvu kisheria ya kumtoa kwenye nyumba? , na ikitokea akaendelea kukaa anaweza tumia technique gani? Kwasababu ni zaidi ya miezi 36 amekaa bila kufanya Malipo
 
nakumbuka mwanzo kabisa ulisema mlishampa Notisi ya kuhama katika nyumba ya taasi lakini alikaidi na kuhitaji kwanza alipwe pesa yake ya PSSSF(counterclaim)- "japo sijui aliwajibu kwa maandishi au mdomo?"nafikiri njia bora iliyopo ni kufungua kesi ya kuomba Amri ya mahakama/baraza la ardhi ya kumuondoka katika nyumba ya taasisi ,na hivyo amri hiyo itapelekea madalali wa mahakama au baraza la ardhi kumuondoa mhusika kwa kutumia taratibu za kisheria. Pia jitahidi kufungua kesi yako mapema kwa umebakiza miaka 3 tu ili kuweza kufungua kesi ya kumuondoa mpangaji na kurudhiwa au kulipwa pesa za kodi ambazo hazikulipwa katika vyombo vya sheria.
 
Naomba tuwasiliane WhatsApp 0763503995
 
Back
Top Bottom