Uhusiano wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993
Uhusiano wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu



Nini kinachofanya uume usimame?
Kwa haraka unaweza kujibu ni msisimko. Naam, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha msisimko huo. Bila hicho, msisimko hauwezi kutokea.

Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu sahihi la swali hili, ili atakapoona tatizo ajuwe pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madakatari pekee kama ilivyo dhana ya watu wengi.

Kutokuwa na chochpote kichwani kuhusu miili yetu ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.

Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ''Asilimia 94 ya damu ni maji''. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini na kama bado unasubiri kiu ndipo unywe maji na tena unakunywa maji ya baridi ya kwenye friji, POLE SANA.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika kusimama kwa uume wako. Kwanini?

Mzunguko wa damu ulio katika afya njema husambaza damu ya kutosha katika viungo vyako vyote vya mwili wako ikiwa ni pamoja na kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kwamba hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako inavyostahili. Tazama mtu aliyekufa, damu haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano wa juu zaidi.

Ina maana kwamba, chochote ambacho huzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa yako ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume. Hii ni kwa sababu uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba sababu ya mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume walio na umri zaidi ya miaka 60, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye ateriosclorisis (hali ya ugonjwa inayosababishwa na kukauka kwa vijiateri vya ateri), na wenye maradhi ya moyo.

Kwa watu wengi, sababu ya kuishiwa nguvu za kiume ni mlo wa mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inshauriwa pia kuepuka vyakula vilivyosindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya ateri ina nafasi kubwa sana kutokana na kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni jambo la busara sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujenga utaratibu wa kuwa unajichunguza mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kutopendelea kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe taabani, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini mwenyewe.

Kwa maswali yeyote niandikie: fadhilipaulo@gmail.com

Download notisi za somo hili hapa.
 

Attachments

  • 94255_f520.jpg
    29.6 KB · Views: 1,391
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…