Uhusiano wa uchawi na kuugua kichaa

xivii09

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2012
Posts
267
Reaction score
153
Ivi kwa nini idadi kubwa ya wachawi ni ni wanawake wengi hususani wazee na siyo wanaume kuna uhusiano gani hapa na je? Kwa nini vichaa wengi ni wanaume kuliko wanawake hili ni duniani kote?
 
Wanaume huwa na tabia ya kufikiria fikiria sana juu ya mbinu za kupata fedha na kutafuta maisha kushinda wanawake hali hii hupelekea kuchanganyikiwa.
 
Wanaume wengi huwa wanatunza siri nyingi moyoni bila kuzisema na ni wagumu kuomba ushauri pale wanapokutana na magumu kwa hiyo nayo hali hii hupelekea kuchanganyikiwa.
 
Mimi nimeshasema mara nyingi sana humu kuwa mambo ya kishirikina yanaendana na matatizo ya akili!
 
Hilo suala sheria za nchi haliamini !
Lakini pia kuna wanaotuhumiwa kuwa wachawi kwa kudhaniwa tu nainapokuja suala la kudhibitisha karibia watu wengi huwa gumu.

Wakati mwingi haya mambo ni kama hsdithi za mapokeo tu maana unaweza ambiwa fulani mchawi mbona unacheka nae ama akaogopwa na watu kizazi kwa kizazi hatA km hakuna ukweli.

Upande wa wachawi wengi kuwa wanawake mmmh ni suala gumu mno kusema ndiyo!

Hapa nilipo idadi kubwa ya vichaa ni wanaume sasa ukidodosa unaweza ambiwa tu mfano katembea na mke wa fulani labda alikatazwa akagoma,ama aliiba cha mtu n.k

Wajuzi waje sote tupate elimu dunia hii.
 
Gender ina determine thinking pattern ya mtu. Wanawake huwa wanazama zaidi kwenye mambo ya imani na wanaikazania....... iwe ya kidini au uchawi. Nenda makanisani uone wengi ni gender ipi?. Uliza waendao kwa waganga wa kienyeji wengi ni akina nani,. Walioenda kwa Mzee Mwasapila kwa kikombe kwa wingi ni wapi>

Kuhusu wanaume kuwa vichaa kwa wingi ni kuwa jamii yetu inawategemea wanaume wawe na solution of almost each and everything. Wanaposindwa si rahisi mwanamme kukubali kuwa umeshindwa. Na wakati mwingine jamii zetu zinatulazimisha kukomaa na matatizo kwa kusema "jikaze, wewe mwanamume". Tukishindwa kuhimili = Personality disintegration. Yaani unakuwa KICHAA.
 
Ivi kwa nini idadi kubwa ya wachawi ni ni wanawake wengi hususani wazee na siyo wanaume kuna uhusiano gani hapa na je? Kwa nini vichaa wengi ni wanaume kuliko wanawake hili ni duniani kote?

mbona equation ina balance hesabu ma witchdoctor wengi ni wanaume na kuna thin line btn witchdoctor na witch
 

kuna maswali mengi kuliko majibu
Je mwili unaweza kuruhusu madhara kwenye sever yake ?(conscious mind)
Je kuna connection gani au nguvu gani isiyoonekana inayounganisha mrogaji na mrogwaji ?
Je kama mrogwaji haamini katika uchawi atadhurika ?
Je nini hutokea kwenye conscious mind hata yatokee madhara yanayopelekea mtu kuwa chizi ?
Conscious mind iko very sophisticated na ni very powerful ina uwezo wa kujilinda na kujikinga na mashambulizi toka nje hasa inapokuwa pure bila kuwa contaminated na illusions za dunia hivyo basi yeyote awe mchawi mwanga nk ili aweze kupambana nayo inaabidi naye awe na conscious mind yenye kiwango sawa au zaidi cha vital energy kuweza kupambana na kudhuru the counterpart
Ni somo refu naomba radhi kwa kuchanganya mno lugha
 
Last edited by a moderator:
Nimekulia vijiji vya mkoa wa Tanga ambako utajiri ni kumiliki uchawi na uchawi ni maisha ya kila siku kila nyanja
Nimetamani mno kujifunza uchawi kutokana na yale niliyiyaona nilitaka nipate ithibati za kisayansi kwenye ulimwengu wa roho ulimwengu wa maisha yasiyoonekana nimekutana na visa vingi sana ambavyo pasina shaka nimethibitisha uchawi upo na unafanya kazi
1: Kijiji cha mjimwema
Kiko njia ya kwenda kicheba ukitokea Muheza mjini kwenda kicheba misozwe mpaka kibaranga
ni kijiji kisafi mno lakini tatizo ni moja kila kitu kimevalishwa hirizi kuanzia wanadamu mimea mpaka wanyama kama paka pimbi na kuku nk
Kwa macho yangu nilishuhudia kifuu cha nazi kikirukaruka kama chura kilikuwa safarini
2: uwanja wa mpira kibaranga
Hapo ndipo ilikuwa airport na nilishawahi kwenda kwa kuiba na vijana wengine kuangalia wachawi wakiondoka kwa nyungo its very fantastic

3:kijijini mlingotini
nilishawahi kupewa chakula na bibi mmoja mchawi mkuu wa kijiji ilikuwa ni wali nyama sikula nikamwaga chooni bila yeyote kuniona lakini alijua na timbwili lake,sitakaa nisahau
Hapohapo mlingotini kijana mmoja anayesagisha alikataa kusagisha mahindi ya mzee mmoja akitaka binti afuate foleni
Haikuchukua nususaa yule kijana alivimba tumbo na likawa gumu kama jiwe alipelekwa kwa waganga wawili watatu wote wakasema ni shughuli ya mzed fulani. Aliwahishwa kwa yule mzee akaombewa msamaha akapona palepale lakini alikuwa hoi mno

Visa ni ni vingi mno vya kushuhudia mwenyewe natamani bado kujifunza hii kitu
 
Mimi nimeshasema mara nyingi sana humu kuwa mambo ya kishirikina yanaendana na matatizo ya akili!

Kuamini ushirikina ni matatizo ya akili tayari.

Na ili ushirikina ufanye kazi kwako, inabidi uwe controlled kiakili, which is a form of matatizo ya kiakili.
 
Kuamini ushirikina ni matatizo ya akili tayari.

Na ili ushirikina ufanye kazi kwako, inabidi uwe controlled kiakili, which is a form of matatizo ya kiakili.

Yup! Ndo mambo ya kuona vitu uvionavyo wewe mwenyewe tu au kusikia vitu uvisikiavyo wewe tu. Hallucinations come to mind.
 
Yup! Ndo mambo ya kuona vitu uvionavyo wewe mwenyewe tu au kusikia vitu uvisikiavyo wewe tu. Hallucinations come to mind.

Especially katika nchi ambayo the doctor to population ratio ni 1:40,000 . Na hapo average.imekuwa skewed na Dar, huko bush inaweza hata kuwa 1:60,000.

Na unaweza kuambiwa katika kila madaktari 20 kuna.mental health specialist mmoja tu.

Kirahisi unaweza kukuta ratio ya mental health specialist to population ni 1:800,000.

Makes you wanna ask, where is Dr. Kilonzo when you need him?
 
Kiukweli wachawi wengi ni wanaume...ila yawezekana wanadhaniwa na kusingiziwa uchawi ni wanawake kuliko wanaume.

Vipi Mtu anakua mchawi? sio shida ni kufanya kitu chochote kitakacho mkasirisha Mungu na shetani atakutimizia unalolita...Kwa mfano mtu anaweza kuamua kulala na mama yake...au mwanawe wa kumzaa...kutia kinyesi kisimani n.k. huu tayari ni uchawi na shetani hapa naweza kukufanyia lolote unalotaka...kwa sababu tayari umeweza kumkasirisha Muumba kupita viwango.....Nini hoja yangu? wanaume wengi wana roho ngumu zaidi kuliko wanawake na ndio maana wachawi wengi huwa ni wanaume....Kwa upande mwengine wanawake wao ni viumbe rahisi sana kuamini mambo ya uchawi....hata kama hapana uchawi...hii inatokana na wanawake ni watu woga zaidi ya wanaume....ndo kusema mwanamke anaweza kuumwa na malaria na akasema amrogwa...na vitu kama hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…