JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
SELIMUNDU (sickle cell) ni ugonjwa unaorithiwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine, hutokana na tatizo kwenye chembechembe nyekundu za damu.
Ugonjwa huu unaendelea kuongezeka hapa nchini kutokana na wazazi wa pande zote mbili kushindwa kupima vinasaba (DNA) kabla ya kuoana au kuzaa.
Ikiwa wazazi wote wawili wanachembechembe za sickle cell wanaweza kumzaa mtoto mwenye ugonjwa huo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa, zaidi ya watoto 1,000 duniani huzaliwa wakiwa na selimundu kila siku.
Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa Nchini Tanzania watoto takribani 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa sickle cell kila mwaka, ambao ni sawa na watoto nane kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa.
Takwimu hizo zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya nne duniani kwa kuwa na wagonjwa wengi wa sickle cell huku nchi inayoongoza Duniani ikiwa ni Nigeria.
Nchi humo, watoto 20 hadi 30 kati ya 1,000 huzaliwa na tatizo hilo, nchi inayofuata ni India ambayo inaonyesha kuwa watoto 14 kati ya 1,000 wanaozaliwa na selimundu na nchi ya tatu ni DRC Kongo ambapo watoto 13 kati ya 1,000 huzaliwa na ugonjwa kila mwaka.
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa sasa Tanzania ina wagonjwa zaidi ya 200,000 wenye sickle cell, takribani watoto saba kati ya 100 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufariki nchini kutokana na tatizo hilo.
Asilimia 15 hadi 20 ya Watanzania 100 wana vinasaba vya ugonjwa huu, yaani wana uwezekano wa kupata watoto wenye ugonjwa huo iwapo watakuwa na wenza wenye vinasaba vya selimundu,” anasema.
CHANGAMOTO WAGONJWA WA SELIMUNDU
Zipo changamoto kadhaa zinazowakabili wagonjwa wa selimundu kulingana na mazingira wanayoishi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wagonjwa wa Selimundu, Arafa Said, anataja changamoto kubwa kuwa ni gharama za matibabu ambazo wengine wanashindwa kuzimudu.
“Kuna gharama za matibabu kutokana na ada ya kumwona daktari kliniki na dawa muhimu za selimundu hii inawafanya wengine kukosa matibabu kwa kipindi kirefu na kurudisha nyuma mahudhurio ya kliniki kwa wale wasio na bima.
“Kingine kuna uchache wa wataalamu kwa mfano ni hospitali chache ukienda unamkuta mtaalamu ambaye mgonjwa anapaswa kumwona hivyo, kupata matatizo mengi kama kuharibika kwa viungo, shida ya kifua kubana, maambukizi ya bakteria na mengineyo,” anabainisha Arafa.
Anasema changamoto nyingine ni vifurushi vya bima ya afya kuwa vya bei ghali na kuwa na kikomo hivyo kushindwa kulipa baadhi ya huduma.
“Pia kuna changamoto ya vipimo, wagonjwa wengi wanalalamika kupimwa damu tu wanapohudhuria kliniki, ukosefu za vipimo vya moyo pia ni changamoto.
“Wapo wagonjwa wanaoshindwa kwenda Muhimbili kutokana na gharama za usafiri,” anafafanua Arafa.
Arafa anasema wanaendelea kusisitiza uboreshaji wa huduma za selimundu kama uwapo wa vifaa, kuongezwa kwa wataalamu wenye ujuzi na kukuza uelewa wa selimundu.
“Kingine ni uwapo wa vipimo vya awali kwa wajawazito na watoto, kuboreshwa kwa bima za watu wenye selimundu na uongezwaji wa huduma maeneo ya vijijini
ili kila mmoja aweze kujua vinasaba vyake tuweze kuvunja mnyororo wa selimundu,” anashauri.
UHUSIANO SELIMUNDU NA MAGONJWA YA MOYO
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi, anasema ugonjwa wa selimundu unaweza kusababisha matatizo ya moyo.
Anasema hali ya kuwa na selimundu huweza kufanya moyo kuwa mkubwa baada ya damu kuwa kidogo.
“Pia upo wezekano wa kuharibika kwa valvu za moyo na kunapokuwa na damu chache inabidi moyo uende kasi zaidi ili uweze kuzungusha damu iliyopo hali hii huleta madhara.
“Lakini lingine ni aina ya chembechembe za damu kuwa hazipo kwenye umbo la kawaida inaweza kugandisha damu na ikiingia kwenye moyo na kuziba unaweza kupata tatizo, kwahiyo changamoto zinazotokea kwenye damu huweza kuleta athari kwa moyo.
“Zile changamoto zinazotokea kwenye damu ndio zinaleta athari kwenye moyo kwahiyo sickle cell husababisha ugonjwa wa moyo, lakini moyo wenyewe hauwezi kusababisha tatizo hilo,” anabainisha Profesa Janabi.
Anaeleza kuwa sio wagonjwa wote wa selimundu wanapata magonjwa ya moyo,bali wapo wanaoweza kupata.
“Karibia kila siku tunaona mgonjwa wa sickle cell kwenye kliniki ya magonjwa ya moyo,” anasema.
Chanzo: Mtanzania