Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

Jason Jr sasa ana miaka 36 kasoro wiki nane na nusu
Ameikomboa ile familia
Mungu ni mwema.

James Jason
Ohoo vizuri sana, ila mama yake alifariki akiwa na ndoto ya kuishi na wewe. Sipati picha alivyokuwa anaifeel hii ndoto, ninaolewa na kijana shabab, msomi, tajiri, anafanya kazi serikali tena anaishi dar es salaam.
 
Ohoo vizuri sana, ila mama yake alifariki akiwa na ndoto ya kuishi na wewe. Sipati picha alivyokuwa anaifeel hii ndoto, ninaolewa na kijana shabab, msomi, tajiri, anafanya kazi serikali tena anaishi dar es salaam.
Malizia, tena mtoto wa mzee Jason aliyefanya kazi na mzungu mishen, mjukuu wa mzee Bourne...

Ilikuwa ujiko! (Na fikra za kitumwa kiasi)

Kikubwa ilikuwa ni kuikomboa familia yake, walitarajia makubwa kutoka familia yetu.

Bahati nzuri wamepata na sasa wanafurahia maisha.

James Jason
 
harafu wewe mzee utakuwa ni ndugu yangu...kuna babu yangu ambaye ni pacha mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye ranch za taifa huko bukoba na mwingine alikuwa anafanya kazi wizara ya ujenzi...wote wamesha staafu...ila huyu aliyekuwa anafanya kazi wizara ya ujenzi nae alioa huko mbugani. bado anaishi na mke wake hadi leo...wapo kiomboi
 
Kigoma mkuu!
Tunatumia dawa mbalimbali kwa kutibu magonjwa mbalimbali. Kwa njia hiyo hiyo ya kuinama
Kwa ulivyouliza tuu nikajua una asili ya kigoma ,kuinama au kujiinika hakuishii kwa watoto pekee hii ni mpaka kwa watu wazima na ni njia mujaarabu kwa tiba
Kwani ina aminika magonjwa mengi huanzia kwenye tumbo hivyo kulipiga deki mara kwa mara huondoa uwezekano wa kupata magonjwa na kuimarisha afya
 
Kipande hiki cha hii hadithi ya kusisimua kina ladha ya tofauti sana upande mmoja unavunja moyo (Kifo cha Ruthi) aendelee kupumzika kwa amani, lakini upande mwingine maendeleo ya upande wa Hamida kukubaliwa kuolewa nawe yanatia faraja iliyo kuu, kuna mengi ya kujifunza hapa!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muda Mungu huwaumiza wengine ili kukupa furaha. Fikiria bila Ruth kufa huenda ndoa na Hamida isingelikuwepo hivyo Mungu akaona kuepusha shari, amtwae mmoja. Unaweza ukapanga kusafiri kwa usafiri fulani ila ikatokea unachelewa kuamka. Utalaumu weee halafu baadaye unasikia gari imepata ajali na abiria wote wamekufa. Ndio maana anasema mawazo yake sio sawa na ya mwanadamu, pale unaposhindwa ndipo anapoanzia. Na hakika kumtegemea yeye kuna faida na akianza kuleta baraka huwa ni mpaka kifo kikupate ndipo unaziacha. Sharti ni moja tu, kumtumainia yeye peke yake.
 
Kwanza pole kwa Ruthi, pili hongera kwa mtoto
Hakika Hamida alipangwa tangu awali awe wako.


Sent using Jamii Forums mobile app
Congrats bro
Congrats bro, its the best art writing i have ever ready in swahili.
 
Kigoma mkuu!
Tunatumia dawa mbalimbali kwa kutibu magonjwa mbalimbali. Kwa njia hiyo hiyo ya kuinama
Ulivyotumia neno KUINIKA nikahisi huyu atakuwa mtu wa Kigoma tu.

Mwaka 2015 nilienda Kasulu sasa tumbo lilinosumbua sana kule halafu kulikuwa na baridi sana hivyo wakahisi labda nina ngiri wakanifanyia hii tiba .

Ndio kwa mara ya kwanza nilisikia hilo neno kuinika..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee itabidi ukishamaliza hizi simulizi ufungue nyuzi za kutoa darasa. Mapenzi ni starehe, vijana kwa kukosa mbinu muhimu za tendo, ndio maana mahusiano yetu hayadumu na hata ndoa nazo zimekuwa na changamoto.
 
Pole sana mkuu, ila sasa vipi asingetwaliwa, ungewaoa wawili? Maana inaonyesha ulishawapenda wote japo hamida Ni zaidi, hongera sana nasubiri niishuhudie ndoa yako
Nipe pole kisha nipe hongera
(Itanifanya nisihuzunike zaidi)

Nimeandika kwa tabu sana sehemu ya 16

Machozi yangu hayapo mbali

James Jason

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Licha ya huzuni juu ya kifo cha Ruth ambaye maisha yake yalitolewa sadaka kwa ajili ya kukuletea heshima na hatimaye kuitwa baba, nimejikuta nikicheka hapo ulipomfuata Betty na kumnyanyua kisha mkaanza cheza pasipo wimbo wowote kuimbwa sababu ya furaha uliyonayo. Ni asili yetu binadamu pindi jambo la furaha litutokeapo kujikuta tukiwa na furaha isiyo kifani na kitamani kila mmoja ajue furaha tuliyonayo.
 
Pole sana mkuu, ila sasa vipi asingetwaliwa, ungewaoa wawili? Maana inaonyesha ulishawapenda wote japo hamida Ni zaidi, hongera sana nasubiri niishuhudie ndoa yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ningewaoa wote

Uislamu (Kama nilivyofundishwa na Maalim Juma) unahimiza wanaume kuoa wake WAWILI, WATATU HADI WANNE, ila ukishindwa ndio uoe mke MMOJA.

Bila shaka Hamida angelikubaliana na hali, aidha kwa Ruth (R.I.P) mitala ni kawaida kimila.

James Jason
 
Furaha inaweza kukufanya ukafanya jambo usilotarajia.

James Jason
 
Kuna mahali katika simulizi Marry alitumia majivu (kulamba)kuzuia mimba.

Hivi Mzee kwa enzi zenu njia za uzazi wa mpango zilizokuwa mnazitumia na zinaaminika ni zipi?

Maana njia za kisasa hizi,Mimi binafsi sizipendi hasa kutokana na madhara yake japo hayasemwi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia za uzazi wa mpango za asili zipo nyingi. Kila Kabila wana njia zao na zinafanya kazi vizuri.

Lakini watu wengi sikuhizi wanapuuzia tamaduni (hata zenye manufaa!?)

Mwenyezi Mungu alitufundisha njia ya asili ya kwanza:-

Kwamba, wanawake wanyonyeshe watoto wao kwa miaka miwili.

Kwamba, wanaume waoe wanawake zaidi ya mmoja kama uwezo upo.

Darasa la kupanga uzazi kwa njia za asili linahitaji uzi maalum, maana kwa elimu ya juu juu inaweza kuleta madhara ama mimba kuendelea kuwepo na kudharau njia uliyotumia.

James Jason
 
Asante Mkuu,naamini ukipata muda baada ya kumaliza hii simulizi,utaanza kutuletea mada za kutuelimisha vijanaa wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo punje mzee baba wacha kabisa ukitafuna kana kautamu kidogo mwishoni koo mdomo huu elewi elewi kama kuflash kwenyewe ndio kule niliapa sitakuja kutumia abadani kisa cha kuchomoa utumbo nini na uombe uwe na choo cha kukaa uwe umepanga halafu choo cha tundu utakaa kwenye ndoo mbonaa
Nimeelewa

Kwenu wapi?

Sie tunakula mbegu fulani punje moja tu kisha shughuli inaaza (kuendesha)

James Jason

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…