Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

aisee, asante kwa simulizi nzuri yenye mwisho unaofurahisha.....
Shukrani

Imenibidi kuifupisha kwakuwa muda wa kuandika umekuwa mchache ukizingatia na huku nilipo halafu wafuatiliaji wanakuwa na hamu...

Kuna uzi mmoja wadau wameamua kumalizia wenyewe simulizi iliyoachwa kwa muda mrefu na aliyeileta. Hahahahah.

James Jason
 

kwa kweli bora umemaliza, tunashukuru kwa kutujali saana, Humu JF simulizi nying haziishagi,


ila sasa m naomba nijue watoto wako ni mashombeshombe eeh[emoji4]
 
vipi reaction ya kuzaa na ruthi
kwa hamida na familia yake
walilipokeaje??
Je watoto wenzie wanamchukuliaje??

Sent using Jamii Forums mobile app
Jason Junior alilelewa Usukumani kwa shangazi yake. Reaction ya Hamida na familia yake haikuwa mbaya, ilikuwa ni ya kujenga. Baada ya darasa la saba, Junior aliishi na wadogo zake hadi alipopata kazi.

Wadogo zake wanamuheshimu na wote wanaheshimiana.
Namshukuru mke wangu kwa kuwalea watoto wote kama wamezaliwa tumbo moja.

James Jason
 
kwa kweli bora umemaliza, tunashukuru kwa kutujali saana, Humu JF simulizi nying haziishagi,


ila sasa m naomba nijue watoto wako ni mashombeshombe eeh[emoji4]
Wakiume wana nywele za kipilipili, wa kike wote nywele zao ndefu. Rangi ni mchanganyiko, maji ya kunde baadhi na wengine shombe, damu ya kitaturu kali.

James Jason
 
Ahsante sana na Hongera kwa hadithi tamu.
 
Wakiume wana nywele za kipilipili, wa kike wote nywele zao ndefu. Rangi ni mchanganyiko, maji ya kunde baadhi na wengine shombe, damu ya kitaturu kali.

James Jason

mimejikuta nmewavutia picha[emoji39]
 
Hongera sana mzee wangu mana nahisi mm na mtoto wako wa kwanza hatujapishana saana

Embu niambie ktk swala sunna uliyoswali wewe ulikuwa imamu au kila mmoja aliswali kivyake na kuna sura maalum ktk hiyo swala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mzee wangu mana nahisi mm na mtoto wako wa kwanza hatujapishana saana

Embu niambie ktk swala sunna uliyoswali wewe ulikuwa imamu au kila mmoja aliswali kivyake na kuna sura maalum ktk hiyo swala

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika swala hiyo ya sunna, mimi nilikuwa imamu.

Nilimtangulia mbele kwa nchi tatu hivi kushoto kwake, miguu wangu wa kulia ukiwa umemgusa mguu wake wa kushoto (kidole changu kidogo cha mguu wa kulia kikiwa mbele inchi tatu hivi ya kidole gumba cha mguu wa kushoto wake)

Ingawaje kuna baadhi ya waumini wao huwa wanasimama mstari mmoja na wengine huwaacha kiasi cha nusu au robo hatua.

Sura za kusoma ya lazima ni al Fat'ha, kisha sura nyingine yoyote.
__

Katika swala za pamoja na mkeo iwe za fardhi (lazima) au sunna (hiyari) mume unakuwa imamu.

James Jason
 
Unaonaje hii iwe ndio special thread yako mkuu, kama kuna mada au story yoyote unaweka tu hapa hapa
 
Hongera Sana mzee wangu, na asante kwa kutushirikisha simulizi hii ya kusisimua na kuelimisha .
Kuna tofauti nyingi Sana nimeziona kati ya sisi vijana wa kisasa na vijana wa zamani, mfano.
1. Yawezekana wengi tumeoana na watu ambao hatukutarajia sababu ya kukata au kukatishwa tamaa na kushindwa kupigania mapenzi yetu. Hukukata tamaa kumpata umpendae pamoja na changamoto zote,Ulipambana.
2. Vijana wa sasa mara nyingi hatuwashirikishi wazee pale tunapotaka kufanya uamuzi muhimu maishani, Kama ulivyomshirikisha Katibu Kata. Hata kukaa tu kijiweni na kupiga soga na wazee au kunywa kahawa ni nadra sana kwa sasa, haswa tunapokua tunajiona tumesoma kidogo au tuna wadhifa fulani.
3. Wewe ulikua unazikabili changamoto, hukuzikimbia changamoto. Mfano vijana wa kisasa tukilala na binti mara moja halafu baada ya muda akasema ni mjamzito, ni wachache Sana watakubali kuwa ni wahusika. Nadhani ndio maana kwa sasa kuna watoto wengi Sana wa mitaani.
4. Una kumbukumbu kubwa Sana ya matukio ya nyuma na ulikua hupuuzii jambo.
Hongera Sana kwa kuwasaidia ndugu zako na wazazi.

Mungu azidi kuwadumisha pamoja katika Upendo,mpendane daima. Binafsi nimebahatika kumuoa binti ambae niliamini na ninaamini ndie alistahili kuwa mke wangu, sikukata tamaa, tulipambania penzi letu.

Msalimie Sana Mama (Hamida) mwambie asante kwa kukuruhusu kutusimulia.

Naamini baada ya kumpata Hamida hukuendelea kupasha viporo baharia mstaafu 😂😂😂😂
 
Nimefuatilia kwa ukaribu hii simulizi yako mwanzo mpaka mwisho kwa sababu kuu tatu;

1.Ni hadithi yenye uhalisia(ya kweli) iliyisimuliwa kwa ustadi wa lugha ya kuvutia na matukio

2.Ni hadithi yenye mambo mengi ya kujifunza hasa kwetu sisi vijana

3. Ni simulizi ambayo kwa asilimia kubwa mikasa yake inafanana na historia ya maisha yangu ya ndoa kama vile;

[emoji818]Jina la mkeo (Hamida),herufi mbili za mwisho 'DA' zinafanana na jina la mke wangu(sitalitaja hapa)

[emoji818]Nimeoa chotara kiarabu(mwafrika na mwarabu) wenye asili ya Yemeni

[emoji818]Nikiwa kwenye mipango ya kumuoa alikuwa tayari keshatafutiwa mchumba Oman na posa ilishaletwa

[emoji818]Familia ya mke wangu ni waislamu na Mimi nilikuwa mkristo

[emoji818]Nilikataliwa kuoa kwa hofu ya 'kuharibu' hasa kwa upande wa imani

[emoji419]Tofauti ni kwamba Mimi na binti tulishakubaliana kuwa yenye ndiye atabadili dini ili kuwa mkristo,hapa nilishikilia msimamo.

Baada ya misukosuko mikali Namshukuru Mungu tulifunga ndoa ambayo ilianzia bomani(Serikalini) halafu baadae kanisani kwa ajili ya kubariki.

Nilichojifunza ni kwamba unapoamua kusimamia jambo ambalo unaliamini, uwe tayari kulipigania kwa gharama kwakuwa si Mara zote utafanikiwa kirahisi.

Onyo;

Katika mazingira kama haya ambayo wazazi au ndugu wanakuwa na wasiwasi wa kukukabidhi binti kwa sababu zozote zile,inapotokea umefanikiwa kumuoa kwa namna yoyote ile,(kwa ridhaa yake) basi huna budi kuhakikisha binti hajutii uamuzi wake,au wazazi hawajutii uamuzi wao.

Najaribu kufikiri kama Mzee Jamaal baada ya kuoa angerudia 'ukipanga' wake na kuanza kumtesa huyu binti(Hamida),au angerudia dini yake ya zamani(ukristo),hii kwanza ingemfanya Hamida ajute kwa kujitoa kwake,pia ingempoteza sana kiimani.

Lakini kikubwa zaidi ingewapa sababu (Mzee Burhani na mkewe)za kuamini kwamba walikuwa sahihi kukataa kumkabidhi binti yao kwa Jamaal kabla ya kushawishiwa na kukubali.

Mwisho,nakupongeza kwa sababu mpaka hapo umeweka viwango vya juu sana,kwa kuvunja ile hofu ya wazazi na ndugu na pia kufanya Hamida ayaishi maisha ya upendo aliyoyotarajia kutoka kwako.

Kauli iliyonivutia katika simulizi;

"Nilibadilika na kuwa mume mwema sana".

Ahsante.











Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…