Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, David Concar amesema kuanzia Novemba 01, 2021 Uingereza itatambua Vyeti vya Chanjo dhidi ya COVID-19 vilivyotolewa na Serikali ya Tanzania
Hatua hiyo itaruhusu waliopata Chanjo hapa Nchini kusafiri Uingereza bila kukaa Karantini au kulazimika kujitenga, ikiwa wamepata mojawapo ya Chanjo zinazotambulika katika Taifa hilo