UINGEREZA: Mwanaume aambukizwa kisonono kisichotibika

UINGEREZA: Mwanaume aambukizwa kisonono kisichotibika

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Mwanamume mmoja nchini Uingereza amesemekana kuwa na kesi "mbaya zaidi" duniani ya ugonjwa wa Kisonono.

Alikuwa na mpenzi mmoja nchini Uingereza lakini alipata bakteria hiyo baada ya kujamiana na mwanamke mmoja kutoka Kusini Mashariki mwa Asia.

Madaktari wa afya huko Uingereza wamesema kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo hayawezi kutibika na dawa aina za 'antibiotics'

Maafisa hao sasa wanamtafuta mpenzi yeyote wa mwanamume huyo, ambaye bado hajulikani, kama njia ya kujaribu kuzuia usambazaji zaidi.

Mwanamume huyo alipatwa na mambukizi hayo mapema mwaka 2018.

Tiba halisi ya ugonjwa huo ni mchanganyiko wa dawa aina ya azithromycin na ceftriaxone lakini zimeshindwa kuutibu ugonjwa huo.

Dkt Gwenda Hughes, wa kituo cha afya cha Uingereza amesema: ''Hii ni mara ya kwanza kwa kesi kama hiyo kudhihirisha kiwango kikubwa cha kutosikia kwa dawa hizo mbili zinazotumika sana za antibiotics.

Majadiliano na Shirika la Afya Duniani(WHO) na kituo cha ulaya kinachodhibiti magonjwa wamekubaliana kwamba kisa hicho ndicho cha kwanza kutokea duniani.

Kisonono ni ugonjwa gani?
_100625120_79837975-ba2c-4f02-8df1-9e7d7733b26f.jpg

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kwa jina Neisseria gonorrhoeae.

Maambukizi hayo husambazwa na ukosefu wa kinga mtu anapofanya kitengo cha ngono.

Kwa wale walioambukizwa, mwanamume mmoja kati ya10 na zaidi ya robo tatu ya wanawake na mashoga dalili za ugonjwa huo hazibainiki kwa haraka.

Dalili za ugonjwa huo zinajumuisha;

  • Ute mzito wa rangi ya jani au manjano kutoka katika sehemu za siri,
  • Uchungu unapokojoa
  • Uvujaji damu wakati mwengine.
Maambukizi hayo wasipotibiwa yanaweza kusababisha mtu kukosa mtoto, kufura katika sehemu za siri na unaweza kusambazwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto aliyetumboni.

Utafiti wa mwanamume huyo unabaini kwamba 'antibiotic' ya mwisho inaweza kufanya kazi . Kwa hivi sasa anapokea matibabu na madaktari watapata matokea baada ya mwezi mmoja iwapo watafaulu.

Kwa hivi sasa hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa -hata mpenzi wake wa Uingereza amegunduliwa lakini uchunguzi bado unaendelea.

Dkt Hudhes aliongeza: ''Tunafuatilia kesi hii ili kuhakikisha kwamba maambukizi hayo yametibiwa vilivyo na mapendekezo mengine na hatari za maambukizi kwa siku zijazo kupunguzwaa.''

Dkt Olwen Williams, rais wa muungano wa Uingereza wa maswala ya afya ya ngono na virusi vya HIV: ''Kutokea kwa maambukizi hao ambayo hayasikii dawa ya kisonono ni jambo la kuzingatiwa na maendeleo makubwa.

''Tunawasiwasi kwamba shida hii inaweza kuongezeka kutokana na upungufu uliofanyiwa bajeti ya afya.

''La kusikitisha kabisa ni kwamba kesi hii imeiwacha huduma ya afya ya ngono katika nafasi ''mbaya'' huku kliniki zikifungwa katika wakati mgumu zaidi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Antibiotics nyingi zinatumika pasipo uhotaji wa matumizi yake mwisho wa siku zinaanza kutengeneza usugu.

Sasa kama huyo mgonjwa na huyo mpenzi wake hawatibiki,hakuna aliye salama.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Washaanza kuandaa watu kisaikolojia ili wauze dawa mpya
Yaani wazungu wanatuona mazoba kwelikweli waje huku afrika tuwape dawa za kienyeji ukinywa asubuhi mpaka jioni unakuwa uko safi kabisa
 
Jaman nimechanganyikiw nimenyonywa uume n mtu mwenye virusi vya ukimwi hapo si nitakua nimeukwaaa?
 
Inatisha sana aisee. Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari kulikuwa na kisegment kuhusiana na hawa bacteria sugu ambao hawatibiki. Nusu ya watu waliogua chanzo kikiwa hao bacteria sugu walikufa. Na kuna watu ambao wana hao bacteria lakini wao wako bomba ila wanaweza kuambukiza binadamu wenzao. Hawakusema lakini wanawezaje kuambukiza. Yaani kuhusu hawa bacteria wakati mwingine mahospitalini ndiyo maeneo yao ya kujidai. Inatisha sana aisee.

Antibiotics nyingi zinatumika pasipo uhotaji wa matumizi yake mwisho wa siku zinaanza kutengeneza usugu.

Sasa kama huyo mgonjwa na huyo mpenzi wake hawatibiki,hakuna aliye salama.
 
Mmh kwani mate yana virusi?...uko poa idriss mkuu usiwe na shaka kabisa
 
Back
Top Bottom