Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Serikali ya Uingereza na Serikali ya Tanzania zitaendelea kushirikiana katika kukabiliana na makosa makubwa yanayovuka mipaka ili kuzidisha hali ya usalama na ustawi wa jamii wa nchi hizo.
Akizungumza katika ziara ya Maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Uhalifu Mkubwa wa kupanga na kupambana na makosa ya Ufisadi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bwana FELIX WOOD amesema kuwa, Serikali ya Uingereza imelenga kuzisaidia Taasisi za Tanzania zinazoshushughulika kuzuia makosa makubwa yanayovuka mipaka ili kuleta mafanikio katika kuzuia makosa hayo.
Nae Naibu Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP ZUBERI CHEMBERA amesema Kufuatia Ziara ya Maafisa Kutoka Ubalozi wa Uingereza, Jeshi la Polisi limeahidiwa kupatiwa vitendea kazi na taaluma hasa katika upelelezi wa uhalifu wa kimtandao.
Aidha, ameishukuru Serikali ya Uingereza pamoja na Wizara ya Sheria, Katiba, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar kwa kuwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kuwasogeza karibu na Taasisi wahisani katika Mapambano dhidi ya Uhalifu.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari
Makao Makuu ya Polisi
Kamisheni ya Zanzibar
Tarehe 20/01/2025