SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,027
- 5,344
Habari wana JF.
Ndio. Uingereza ni mji wa Marekani.
Jinsi nilivyoanza unaweza kusema kwanini hili sikupeleka jukwaa la Utani. La bali ni masikitiko yangu tu hasa katika swala la Elimu hapa kwetu Tanzania.
Nilikuwa na kijana mmoja tumetulia sehemu mmoja hivi tukisikiliza muziki radioni na ilipofika muda wa habari ilibidi ni badilishe kituo kingine cha radio. Yule kijana akahamaki kwanini nabadilisha wakati muziki ulikuwa mzuri. Nikamjibu tusikilize habari tujue nini kinaendelea duniani.
Katika habari hiyo Uingereza na Marekani zilitajwa.
Baada ya kutajwa huko yule kijana ambaye alimaliza kidato cha 4 mwaka 2012 akauliza mbona mie hapo sielewi kuhusu Uingereza na Marekani. Huelewi nini? nilimuuliza. Akasema "Uingereza na Marekani mbona ni nchi moja yani kama Dar es Salam na Tanzania, Uingereza ni mji na Marekani ni nchi na zipo bara la Ulaya"
Nilifikiria mengi nikajua hiki ndio kizazi cha BONGO FLAVA & MOVIE. Nilichofanya nilimfafanulia akawa kaelewa.
Baada ya hapo nikawa najiuliza juu ya vijana wetu na nikasema hebu nifanye uchunguzi kwa vijana kumi tu ambao wamemaliza kidato cha 4 mwaka jana na juzi na swali lilikuwa hilohilo moja juu ya Uingereza na Marekani.
Vijana na majibu yao:
1. Marekani ipo Uingreza na zipo Bara la Asia
2. Hiyo ni Nchi moja ya Marekani sema Uingereza ni mji wao ndio ambao unaongea sana Kiingereza na Marekani wote wakawa wanaongea hiyo Lugha.
3. Achana na mimi bwana hiyo nchi itanisaidia nini mie sijui lolote niache kusaka maisha tena unanirudisha shule.
4. Marekani ndio nchi na uingereza ni mji wake na ndio maana sijawahi kusikia RAIS wa Uingereza bali huwa nasikia RAIS wa Marekani.
5. Kwakweli mie sijui chochote.
6. Zote ni nchi na zote zipo Bara la ULAYA.
7. Kamuulize Kikwete ndio huwa anasafiri sana kwenda huko Marekani.
8. Mie ninachojua Uingereza ipo Ulaya na Marekani ipo America ya kusini.
9. Umenidharau kaka mpaka unaniuliza hivyo. Marekani ni nchi na Uingereza ni nchi. Uingereza ipo Ulaya na Marekani ipo Marekani ya Kaskazini. Marekani ina Rais kwakuwa inatumia serikali ya kidemokrasia na uingereza serikali ya kifalme na ndio maana ina Malkia Elizabeth.
Hahaaa unanidharau hebu nipe tano bro.
Nikawa nimemaliza kwa hao 9 ukijumlisha na yule mwingine akawa wa 10.
Kiukweli binafsi niliwaza mengi sana juu ya vijana wetu wengi hata ule uelewa tu wa kawaida hawana hususani wale waliomaliza kidato cha 4. Ukianglia hapo asilimia 90% hawaelewi chochote. Mie shule ya msingi niliyo soma miaka hiyo kulikuwa na ATLAS ambacho kilikuwa kitabu kizuri sana cha kuonyeha ramani za nchi mbalimbali na Tabia za Nchi. Hapa suala kuu siyo kujua sehemu ila uelewa.
Wanafunzi, Serikali na Walimu Wake, Wazazi na Wadau mbalimbali TUAMKE jamani elimu ipo pabaya sana.
Asanteni.