Uingereza yaondoa vikwazo vyote vya COVID-19

Uingereza yaondoa vikwazo vyote vya COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Uingereza imetangaza kuanzia leo kuondoa masharti yote ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona. Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na wanasayansi na vyama vya upinzani wakisema kuwa itaiweka nchi hatarini. Kuanzia saa sita ya usiku vilabu vya starehe vyote viliruhusiwa kufunguliwa tena.

Aidha hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kama kuvaa barakoa, kuweka umbali wa mita moja na nusu baina ya watu na kufanya kazi kutoka nyumbani zote zimefutwa. Waziri Mkuu Boris Johnson ameutetea uamuzi wa serikali yake na kusema:

"Ikiwa hatutafanya sasa, basi tutakuja kufunguwa miezi ya msimu wa baridi wakati virusi vitakapokuwa vinasambaa kwa kasi zaidi. Wakati huo huo tunapoteza muda wa mapumziko ambapo watoto wa shule pia wako likizo.

Tunapaswa kujiuliza kama sio sasa, tutafanya lini?" Licha ya kuondolewa vikwazo, Johnson amewataka wananchi wa Uingereza kuendelea kuwa waangalifu.
 
Wenyewe wanafungua sisi tunafunga...what a contradictory gut?
 
baada kushindwa kupata ufumbuzi wa uhakika waingereza wameamua kucopy Kwa Mr Pombe.....

bado utasikia tupige nyungu jamani.....
 
Tatizo wameturuhusu na wao wako kwenye house arrest
Yaani wengi bado wanavaa masks pamoja na kusema tuziache

Ila upande mwingine kwa kina dada mauzo ya lipstick [emoji168] yamepanda kwa 60%
 
Back
Top Bottom