Uingereza yasema ATCL kufanya safari zake nchini humo ni fursa ya kiuchumi

Uingereza yasema ATCL kufanya safari zake nchini humo ni fursa ya kiuchumi

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552
1565171934290.png


Serikali ya Uingereza imesema Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanzisha safari za ndege kutoka nchini humo kwenda Uingereza ni fursa ya kiuchumi kwa nchi hizo mbili. Hivi Karibuni mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema mwishoni mwa mwaka 2020 shirika hilo litaanza safari zake kati ya Dar es Salaam, Tanzania na London, Uingereza na tayari limepata ratiba ya uwanja wa Gatwich .

Rosindell ambaye amesema Tanzania ina mambo mengi ya kuipa Uingereza kupitia safari hizo. "Kuna fursa kubwa ya kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji kama utalii kupitia ndege ya moja kwa moja.” “Kupitia safari hizo tutaimarisha urafiki wetu na mahusiano ya muda mrefu, nina imani jambo hili litakuwa la manufaa kwa pande zote," amesema Rosindell aliyeambatana na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke. Amesema lengo la ujumbe huo ni kusikia mipango, kueleza fursa, kushauri na kusaidia kufanikisha.

Mkurugenzi wa biashara wa ATCL, Patrick Ndekana ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuwaeleza fursa na nia ya kulisaidia shirika hilo kutimiza mipango yake, ameahidi kushirikiana nao ili kufanikisha jambo hilo. "ATCL imekuwa ikishiriki kutangaza fursa za biashara na utalii hapa nchini, hivi sasa tunataka kukuza soko la Ulaya. Kibiashara Jiji la London litatuunganisha na nchi nyingine za Ulaya na Amerika," amesema Ndekana

source: Mwananchi
 
Tatizo ni bei ya ATCL iko juu ukilinganisha na mashirika ya ndege mengine......
 
Kwa direct cargo plane to London ndio ingelipa saiv. Na itakuwa haina msimu kama za abiria hadi utalii tu
 
Ila mpaka mwishoni mwa 2020 ni mbali sana. Mashirika yenye codeshare na ATCL ni yapi?
 
Propaganda tamu sana ukiijua

Kuna siku utaskia ‘ British airways, Emirate na Qatar airways waingiwa hofu kwa kasi ya ATCL kwny baishara ya Usafiri wa Anga...’
 
Back
Top Bottom