HAYATI OSCAR KAMBONA KATIKA KIELELEZO CHA UNYAMA WA NYERERE:
Ushetani wa dikteta huyo unatisha zaidi katika unyama aliomfanyia swahiba wake,hayati Oscar Kambona ambaye siyo tu ndiye aliyemwinua sana kisiasa,bali bali ndiye aliyeokoa hata uhai wake na utawala wake majeshi yalipotaka kimpindua mwaka 1964,ambapo nchi ilikwishakuwa mikononi mwa Kambona,kama angekuwa na uchu na roho ya ubinafsi kama ya Nyerere.
Oscar Kambona ndiye aliyemwokoa Nyerere hata alipokumbwa na ile kashfa ya rushwa ya nyumba ya Magomeni kutoka kwa Wahindi,alipokuwa Waziri Mkuu kwa miezi minne,kwa kumfundusha kama rafiki wa kweli kwamba ajiuzulu kabla ya hatua ya kamati ya TANU,kwa kisingizio kwamba anakwenda kuimarisha chama,ndipo dikteta huyo akapona na wadhifa akapewa Rashid Kawawa.
Tena ni Oscar Kambona aliyemfuata huyo rafika yake kwao Butiama mwaka 1958,alikokuwa anafanya Kazi mpya ya kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kizanaki baada ya kujiuzulu TANU ilipoishiwa pesa, Kambona akachangisha fedha ukanda wa ziwa alipotoka Uingereza kusoma,ndipo kwa sababu ya pesa rafiki yake akakubali kurudi TANU,na hatimaye akaupata na huo udikteta.
Isitoshe,Kambona ndiye aliyeasisi ukombozi wa kijeshi wa nchi za kusini mwa Afrika,baada ya kuwashawishi vizito watatu yaani Ahmed Sekou Toure,Kwame Nkuruma na Haile Selassie.Lakini sifa zote hatimaye akazibeba yeye Nyerere,ambaye kwa sababu wivu alimwondoa Kambona katika wizara ya mambo ya nje.
Kambona ndiye aliyekwenda China akaomba na kupata msaada wa ujenzi wa reli hii ya Uhuru,ambayo ilikuwa iwe katika Mtwara Corridor kwa sababu ya chuma Cha Liganga na mkaa wa Mchuchuma,mafuta na gesi vilivyopo kusini,na ukweli kwamba huko ndiko ambako kustawisha Taifa na Afrika kwa ujumla baadaye,lakini Nyerere akamtukana Kambona kwamba ni mkabila na kuihamishia reli hapo ilipo.Baada ya kutofautiana naye kifikra hasa juu ya ujamaa,Kambona alilazimika kutoroshea roho yake uhamishoni.
Kwa unyama wake dikteta huyo alisahau mema yote aliyotendewa na Oscar Kambona,akataifisha nyumba zake zote na kuamuru ukoo wote wa Kambona wasakwe na kuteswa.Mwanamke mmoja ambaye kwa kosa la kuwa na undugu na Kambona,akifanyiwa unyama wa kutisha mpaka kushindiliwa machupa na mawe sehemu zake za Siri na kubaki hana kizazi mpaka leo,pia ilibidi akimbilie Ulaya.
Kambona alifuatiliwa mpaka huko alikojificha akakoswa koswa mara nyingi kuuawa,hatimaye akauliwa mtoto wake wa kwanza aliyeitwa David Kambona kwa risasi.Nyerere aliuonyesha ukatilii wake kwa kuikimbia miili ya hayati Oscar Kambona na ndunguye Otini Kambon,siku ilipokuwa inawasili kutoka Uingereza.Hakutaka kabisa kuuona mwili wa mfadhili na mdhamini wake aliyemfanyia mema yote haya,akaukwepa pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam wakati anatorokea Butiama! Wala hatusemi kuhusu kiini Cha kifo chenyewe Cha hayati Oscar Kambona.Huu hauwezi kuitwa uwenyeheri.
Kusini mwa Tanganyika kumeathirika sana kimaendeleo tangu zamani hizo,kwa sababu ya kisasi Cha mwenyeheri huyo kwa Kambona.Wasomi na wanataaluma wengi wa huko wameishi nchini mwao kama ukimbizini,hata kama Mungu aliwapa vya kuibariki nchi yetu kama akina David Mattaka,Chiombola n.k waliofanya miujiza ya PPF nchini,lakini badala ya kupewa sifa na heshima waliyostahili,wakaangamia kama panya aliyethubutu kuinuka kutenda mema mbele ya paka,akidhani watamfurahuia na kumhesabu kuwa mwenzao.
Hayati Oscar Kambona alipotukanwa na dikteta huyo kwamba ni mkabila,kwa sababu ya kuipeleka reli ya uhuru kusini kwa ajili ya mapinduzi ya maendeleo ya Taifa letu na Afrika kwa ujumla,alimjibu kwa upole kwamba"Mimi unanionea,kwa sababu kama ni makosa aliyeyafanya ni Mungu mwenyewe"Alipoulizwa na Nyerere kwa ukali kwamba ana maana gani, Kambona alimjibu "kwa sababu Chuma Cha Liganga,mkaa wa mawe wa Mchuchuma,hazina za mawe ya thamani duniani,gesi na mafuta zilizoko kule kusini,kama Mungu angeviweka kule Musoma au Kilimanjaro bilashaka reli ingepita Kule,ila sasa alikosea na akaviweka Kusini."
Kisa hiki kilichangia kustawisha mbegu ya kisirani ndani ya dikteta huyo juu ya Kambona,ingawa urafiki wao usingedumu kwa muda mrefu kwa jinsi usivyoweza kuwepo umoja baina ya nuru na giza.Oscar Kambona alikuwa uzao wa ukuhani wa kikristo,wakati dikteta huyo mwenye Nyamurhunda ni wa mamlaka kuu ya kuzimu.
Kwa vile msingi wa utawala wa CCM ni ule ule wa kuzimu,mpaka leo nchi imo gizani kwa sehemu kubwa,kwa sababu mamlaka kuu ya giza kuzimu imezuia tusizalishe umeme wa mkaa wa mawe alioshauri Oscar Kambona,ambao ndio umeme wa uhakika unaoaminika (stable) kuliko wa maji ambao hupungua na hata kukauka kabisa ,au wa mafuta ambao ni ghali mno au wa nuclier ambao hata mataifa makubwa sasa wanauacha na kurudi ule wa uhakika na salama zaidi yaani wa mkaa wa mawe,kwa sababu ya hatari na athari zingine nyingi za nuclier.
Ni kweli kwamba umeme hauwezi kupelekwa vijijini kwa walalahoi ambao katika sehemu nyingine bado wanaenda uchi wa nyama na kuishi katika vibanda vya nyasi au tembe,miaka 60 baada ya uhuru,hali ambayo ni sura halisi ya utawala toka kuzimu!Lakini shangingi la mbunge baada ya kuiba Kura na mamilioni ya marupurupu yake yangetosha kugawa vile vimashine vya kutengeneza matofali ya udongo katika vijiji vya jimbo lake ,pamoja na vigae vya udongo,ili kila kijiji kikishajikamilisha kwa nyumba bora kwa wananchi wote kipelekewe umeme na kukomesha kabisa kugusa misitu,kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo.
Nyerere alimvika Oscar Kambona sura ya kuwa haini na msaliti mkuu wa Taifa kwa kupinga Azimio la Arusha au Ujamaa ambao alisema ni utu, na kupendelea ubepari ambao ni alitufundisha kwamba ni Unyama.Lakini unabii wa Oscar Kambona kwamba nchi ingeathirika vibaya sana kiuchumi,kijamii na kisiasa,na kurudi nyuma sana kimaendeleo na wananchi kuteseka sana ulitimia,na Nyerere akakiri kwamba "Tulifanya makosa".Kwahiyo kama dikteta huyo angekuwa na toba ya kweli kama mtu mwenye heri basi angeukiri unabii wa Oscar Kambona na kufanya naye suluhu,na kuyafanyia Kazi. Maono yake ya neema kwa nchi yetu,jambo ambalo Nyerere hakuweza kwa sababu ya roho yake chafu.Ndio maana haishangazi kutokuwepo nchini hata mtaa mmoja wenye jina la Shujaa Oscar Kambona licha ya mchango wake kwa uhuru na heshima ya nchi yetu na Afrika.