Democracy999
JF-Expert Member
- May 26, 2012
- 945
- 189
Jana wameshambulia mahoteli mawili ya Kitalii katika Mkoa Kaskazini Unguja, na kila wiki hoteli japo moja ya Kitalii inaingiliwa kwa silaha.
jana waliteka watalii kwa kwenda na mwenye hoteli kuwagongea chumba hadi chumba.
Walichukua kila kitu mpaka mabegi yenye passport zao na documenti zao muhimu.
Mwanamke mtalii mmoja walimbaka.
Mwenye hoteli ya kwanza kuporwa mtaliano walimpiga risasi ya kichwa ila hajafa, mlinzi wake walimkata mkono.
Mwenye hoteli ya pili kushambuliwa Mtaliano nae kapigwa sana ili atoe ushirikiano.
Haya mambo yanaongezeka sana siku hadi siku.
Uporaji wa kutumia visu au bisibisi umeshamiri pia nyakati za usiku au hata mchana kwenye mitaa ya Mji wa Zanzibar na kwenye fukwe mbali mbali, na hili linawapata watalii na wazalendo pia.
Jamii haijajua bado ifanye nini, wangine wanasingizia siku zote Wabara japo sio kweli, ni kujaribu kujipotosha, wengine huwashangilia na kuwaita wanaume eti wamechukua chao.
Serikali imewaacha wawekezaji peke yao.
Jana mabalozi wamekuja wachukua raia wa nchi zao wakiwa hawana documenti yoyote.
Je????????? sehemu ndogo kama Zanzibar (unguja) upana kilomita kama 30 tu, urefu kama 80 hivi, yenye majeshi yake na ya Muungano, yenye tourist police force ambao kutwa huranda kuwaomba pesa mtu yeyote anaonekana na mzungu eti kuuliza kama wana vibali vya kufanya tourist guide eti wanalinda utalii, au wanadili na mateja kuwauzia wazungu madawa au bangi kisha wawakamate na kutishia kuwapeleka jela na wazungu hatoa pesa sana kwa woga, na mara nyingi huwapiga chabo watalii wanapokuwa beach ku enjoy mazingira wakiwa kwenye romantic way na huwasingizia kuwa wanafanya ngono hadharani na mchezo wa kuwatoa pesa kwa vitisho unaendela.
Jibu! Utalii unavunjika Zanzibar, kila mwekezaji sasahavi anajenga pwani ya Msumbiji kukimbia Zanzibar inayozamishwa na Wazanzibari wenyewe huku wakilaumu wengine tu kwa kila kitu (mfano katika kitongoji cha Mji Mkongwe kwa hapa eti ni jimbo, kina harufu ya kinyesi mitaani, juzi nimeshuhudia watalii na wazalendo wakipita huku wameshika pua kwa harufu na ndio mitaa ya Ismail Jussa na Mbunge Sanya) Zanzibar inazama jamani.