Muda mfupi uliopita katika redio Wapo nimesikia ujambazi uliotokea "Commercial Bank of Africa" tawi la Nyerere RD-Jamana House. Majambazi 6 yalitumia vitambulisho vya benki hiyo na kutumia muda wa saa 2-3 na kufanikiwa kuchukuwa mamilioni ya fedha za Ki-Tz bila kutumia silaha. Kamanda Kova akihojiwa amesema wamewakamata watumishi 2 na mlinzi 1 wa Security Grp. Pia ameeleza kuanza kwa upelelezi mkali kwa kutumia Ma-CID kutoka Makao Makuu na Kanda Maalum.
Hakuna madhara mengine ambayo yamesababishwa na uvamizi wa majambazi hayo.