"Ujana Dume wako uko wapi?" Rais Samia ahoji maswali mazito watendaji wanaokalia kimya upotoshaji unaoendelea mtandaoni

"Ujana Dume wako uko wapi?" Rais Samia ahoji maswali mazito watendaji wanaokalia kimya upotoshaji unaoendelea mtandaoni

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Siku chache tangu zisambae picha mtandaoni kwamba kuna wagonjwa wanapelekwa hospitalini kwa kutumia matenga huko mkoani Ruvuma, Rais Samia jana ameamu kujibu mapigo.

Akiwa anahutubia jana huko mkoani Ruvuma Samia alisema kuwa anasikitishwa na baadhi ya watendaji wanaokaa kimya pindi taarifa za uongo zinaposambazwa mtandaoni kuhusu serikali na kuwataka watendaji wasisubiri Rais au mawaziri kuja kukanusha badala yake wawe wanakanusha wenyewe.

Samia alifananisha viongozi au watendaji wanaokaa kimya wakisubiri taarifa zinazochafua serikali zikanushwe na Rais au mawaziri kama wanaume wanaokimbia nyumba zao kwenda kwenye nyumba za wanaume kuomba msaada pindi wanapovamiwa na nyoka.

Hii ni sawa na mwanaume kaingia nyoka ndani ya nyumba yako, unatoka mbio unaenda kumuita mwanaume mwenzio, njoo unitolee nyoka nyumbani kwangu. Ujana dume uko wapi hapo?

Kwa kweli inafikirisha sana kuona viongozi wetu wanakerwa na mambo petty petty kama maoni ya watu wa mitandaoni.

Nawasilisha!

 
Alishakanusha watu hawauawi hadi wauaji walipofanya tukio live. Akapeleka fidia ya Tshs 5,000,0000 kwa familia ya marehemu ili kuwanyamazisha.

Yeye si ndiye anayetoa hela zote? Asikimbie lawama ya ubahili
 
Asilete drama huyu Chura kiziwi wa Kizimkazi!
 
Back
Top Bottom