Sharo kwa kweli umeuliza swali la msingi sana tena sana,nakupongeza.Sasa ngoja nikumegee.Kwa kuwa unaingia humu JF na kuandika vitu vya maana ina maana wewe sio maimuna,una kaelimu kako na bila shaka una kashughuli ambako kanakuingizia kipato.Sasa nisikilize:
1.Kama ukijaliwa kupata ajira epuka tamaa.Wako vijana wengi hasa waliopata ajira kwenye mabenki,bandarini na TRA,kwa sababu ya tamaa ya kupata vitu kama blackberry na Nokia torch,toyota markX,kutanua Runaway na kwa JD,jeans za bei mbaya,kununua vidani vya dhahabu na matumizi mengine kama hayo,mara nyingi wamekwapua hela ofisini na matokeo yake wameishia lupango.Kesi kibao za fojare Kisutu zinahusu vijana,watch out,ishi kulingana na kipato chako , epuka tamaa.
2.Usiwasahau wazazi. Ni rahisi kupata kipato kizuri girlfried mzuri,apartment,gari na mwisho ukajiona umefika.Wazazi wako hata wawe matajiri vipi bado watafurahi ukiwakumbuka mara kwa mara hata kwa zawadi ndogo,baraka zao ni muhimu. Baba,Mama kama unaishi nao karibu siku moja moja watoe for a drink au hata nyama choma,usiwasahau.
3. Roho yako ikimdondokea msichana usikurupuke kumwoa,take your time maana majuto ni mjukuu na jihadhari usizae kabla hujaoa maana mwisho wake weza kuta una watoto kumi kwa wanawake kumi,tumeyaona haya na wala sio nadharia.
4. Fanya mazoezi,yatakusaidia uwe na afya nzuri lakini pia huwa yanapunguza muda wa vishawishi.
5. Jifunze mapema wakati ungali kijana umuhimu wa kutembelea wafiwa,wagonjwa,kuhudhuria harusi za watu etc hii itakusaidia siku za usoni siku yakikukuta.
6. Kujenga urafiki wa kweli ni kitu kigumu sana,ukimpata rafiki wa kweli mthamini,mtasaidiana kwa mengi huko mbeleni.
7. Kama wewe ni mkubwa kwenye familia,jitahidi uwe mfano mzuri kwa wadogo zako.
8. Endapo itatokea ukapata pesa nyingi usiwe na nyodo,maisha ni kupanda na kushuka.
9.Anza kuweka akiba ungali kijana,itakusaidia siku za usoni.
10.Wewe ni mtoto wa kiume,hata kama wazazi wako ni matajiri lakini wewe jitahidi ujenge kanyumba kako kwa pesa yako mwenyewe,utajivunia matokeo ya jasho lako.
Kwa leo naishia hapa ngoja na wana MMU wengine waendelee kukumwagia ushauri.Nakutakia maisha bora yenye fanaka tele!
Wako,
Bishanga Abashaija.