"Ujanajike" Kitabu Kilichoshinda TUZO ya Fasihi

"Ujanajike" Kitabu Kilichoshinda TUZO ya Fasihi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
"UJANAJIKE" KITABU KILICHOSHINDA TUZO YA KISWAHILI YA CORNELL YA FASIHI

Mwandishi wa kitabu hiki Dotto Rangimoto kaniletea kitabu hiki nimekikuta nyumbani tena "autographed."

Bahati mbaya lau nilikiona na nikakifungua sikuona kuwa kilikuwa na jina langu na sababu ni kuwa nilikuwa nimetoka safari na nina mzigo wa kazi za kuandika.

Akili yangu yote kwenye kazi hii.

Nikachukulia kuwa hiki kitabu ni cha mtu mwingine hapa nyumbani nikarejea kwenye kazi zangu.

Ilikuwa pale nilipogutushwa ndiyo fikra zikarejea nikakifungua kitabu na kuona kuwa kimeletwa kwa ajili yangu na kina jina langu tena kwa kuadhimishwa.

Nasikitika kuwa sitaweza kukifanyia haki itakiwayo kitabu hiki kwa kuwa nina mkataba wa kazi ambayo umenifunga siwezi kupumua.

Juu ya haya yote nimefungua Mlango wa Kwanza wa kitabu.

Kimenichoma na kuniita simanzi.

Binti yuko kwenye kitanda chake cha mauti anahadithia mkasa wake uliomfikisha pale alipo.

Hawezi kushika kalamu kuandika.

Anatumia kinasa sauti akizungumza kwa sauti iliyochoka na inafifia.

Si bure kuwa kitabu hiki kimepata tuzo.
Ndugu yangu hutojuta kukisoma kitabu hiki.

1741466464019.png
 
Kumbe Dotto Rangimoto kajikita kwenye uandishi siku hizi! Simuoni kwenye majukwaa ya siasa kama nilivyomzoea siku za nyuma.
 
Back
Top Bottom