ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Habari yako mwanajamii.
Kwa wasaa mwingine tena kuyajua haya :
Ujangili ni shughuli ya kiharamia ambayo hufanywa na baadhi ya watu katika kuwinda wanyamapori ambao pia ni rasilimali kubwa kwa taifa, na kama tunavyoelewa unapofanya uharamia au ujangiri ni uvunjifu na kinyume cha sheria za nchi.
Pia kwa vipindi tofauti kumekuwa na tuhuma mbalimbali zinazotokana na baadhi ya makosa ya watu wanaodhanika kuwa ni maharamia na pia kumekuwepo tetesi kwa miaka ya hivi karibuni kwamba moja kati ya sababu zinazodhaniwa kupunguza idadi ya watalii ni kwasababu ya upungufu wa wanyamapori wengi wanaliokuwa wakipatikana vipindi vya nyuma lakini hatimaye sasa idadi imepungua ikilinganishwa na mwanzo, ambapo nchi ilikuwa ikipokea idadi kubwa tofauti tofauti ya watalii na pia tukizingatia pia hata wanyamapori walikuwa wengi sana katika maeneo ya hifadhi ikiwa ni tofauti na hali ya hivi sasa.
Na tangu nipo shule ya msingi nilikuwa nikisikia habari ya kutoweka kwa wanyama mbalimbali ikiwa inachangiwa na sababu za mabadiliko ya tabia ya nchi lakini hasa ujangiri, naomba niulize je? Kama tangu kipindi nipo kipindi hicho miaka ya (2008) ikasemekana wanyama hao wapo kwenye hatari je? Vipi kufikia miaka ya hivi sasa watakuwa wamepotea wanyamapori wangapi, jambo linalotokana na uwepo wa majangiri katika aeneo ya hifadhi zetu za wanyamapori
Licha ya uwepo wa kitihada zinazofanywa na wizara zinazosimamia maliasili na wanyama pori bado kuna mianya na uwepo wa maharamia hao ambao huwashambulia kikatili kwa risasi wanyama mbalimbali hasa tembo na vifaru katika kuhakikisha wanawang'oa ndovu na pembe zao kwa malengo yao binafsi katika kujinufaisha kiuchumi kinyume na sheria za nchi yetu.
Pia nakumbumbuka kwamba nimewahi kujifunza kwamba kifaru na tembo ni moja kati ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi zetu za taifa
Majangiri huwinda wanyama hao kwa lengo la kujipatia pembe za ndovu na kuziuza nje ya nchi kinyume na sheria.
Kwa moyo mmoja tunaiomba Serikal izidi kuweka jitihada ili kuwanusuru viumbe hao muhimu kwa sifa bora kwa taifa letu halafu pia hii itasaidia kuchochea utalii ambao kwa kiasi kikubwa utaongeza pesa za kigeni na kuinua uchumi na pato la nchi na pia kulitangaza taifa vyema kimataifa katika swala zima la uhifadhi bora wa wanyampori.
Tukomeshe ujangiri Kwasababu wanyamapori ni rasilimali ya pekee sana kwetu na tunapaswa kujivunia
Tukomeshe ujangiri kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu sote
Tunategemea utanzaji bora wa wanyamapori na misitu kwa ujumla kwa sababu maisha yetu bora hutegemea wanyamapori hao licha ya kujipatia ongezeko la fedha za kigeni pia huchochea ubora wa mazingira yetu kuimarishwa zaidi.
Asante.

Upvote
1