Ujanja ujanja na utengenezaji wa mazingira ya kibiashara Ofisi za Serikali

Ujanja ujanja na utengenezaji wa mazingira ya kibiashara Ofisi za Serikali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam ndugu zangu,

Natumai wote mu wazima. Leo najaribu kugusia na kudokeza baadhi ya tabia za ujanja ujanja zinazofanyika nje ya Ofisi nyingi za umma.

Walinzi au watu wa mapokezi wa sehemu hizi wamekuwa chambo Cha kufanya biashara ndogo ndogo wakitumia chambo Cha wananchi kusaka huduma nitatoa mifano kadhaa.

Ukienda Ofisi za NSSF kupata huduma kama hujui mazingira vyema walinzi watakutaka ununue barakoa kwao Ili wakuoneshe na wakuruhusu kuingia ofisini.

Ofisi za Uhamiaji hawaruhusu kuingia na begi lolote kwa hiyo watu wa mapokezi watakulazimu uende nje ambako utakutana na watu wanahifadhi mabegi kwa Shilingi 1000.

Kiukweli hizi pesa ni ndogondogo sana wanatoza watu lakini ukiwaza kwamba Kuna watu wanaweza wasiwenazo kwahiyo wanaweza kukosa huduma kwa sababu ya wizi huu.

Serikali na Mamlaka husika katika Ofisi za umma najua mnayafahamu haya tafadhali yaangalieni na yashughulikieni.
 
Mara nyingine wanasaidia sana, kama pale Ardhi Magogoni wale vijana wa Jkt walinisaidia sana kwa ujira mdogo.

Laa sivyo ule msululu.
 
Back
Top Bottom