Ujanjaujanja wa Azam, hongera CAG na serikali kwa hili

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Nimefurahishwa na mabadiliko ya mfumo wa ufanyaji kazi baina ya serikali kupitia Temesa na azam marine kupitia bidhaa yao ya azam tax ferry.

Azam walipata dili la kuvusha watu pale ferry kwenda upande wa kigamboni kwa tender isiyo na uwazi baada ya vivuko vinavyomilikiwa na temesa kwenda kufanyiwa ukarabati.

Hata mara baada ya vivuko vya temesa kurudi bado azam waliendelea kuvusha watu huku kupitia ripoti ya CAG 2023/2024 tukajua kuwa azam walikuwa wakilipwa shilingi milioni tano kwa siku ambayo kwa mwezi mmoja ni milioni 150 tshs huku wao wakiwa hawalipi kodi wala ushuru wowote.

REJEA: Thread 'CAG Ripoti 22/23: TEMESA inailipa Kampuni ya AZAM Tsh. Milioni 5 kila siku kuendesha Vivuko' CAG Ripoti 22/23: TEMESA inailipa Kampuni ya AZAM Tsh. Milioni 5 kila siku kuendesha Vivuko

Hali iliendelea kuwa mbaya kwani kuna tetesi ya hujuma mpaka zilianzwa kufanywa ili azam aendelee kupewa tenda hujuma hizo ikiwa ni pamoja na vivuko vya temesa kuendeshwa taratibu na kikifika upande wa pili kinakaa muda mrefu kabla ya kurudi upande wa pili ili kwa makusudi watu wavizoee na kuvipenda vya azam huku ikiwamo tetesi za maboss watatu kula 10% ili azam waendelee kutoa huduma.

MABADILIKO
Baada ya ripoti ya CAG kuanika madudu yale mfumo wa uendeshaji wa sasa Azam anaingia kama muwekezaji na sio mzabuni.

Hivyo azam atatoa huduma kwa price anayoona yeye kuwa itamlipa na kisha atalipa kodi na malipo mengine yanayotakiwa kisheria.
Hivyo kwa sasa kuna watoa huduma wawili pale ferry
Temesa pamoja na azam marine.

Ombi
Tunaomba wawekezaji waongezwe tena bila ukiritimba wa kuchomekana kwa 10%

Tanesco,tazara pia watafutiwe washindani

Kazi iendelee
Lissu,samia mitano tena
 
Hapo Mwisho Mwisho Kabisa
 
Hiyo njia ya meli, huwezi kujaza makampuni mengi ya vivuko.

Uache wivu
 
Nasikia na yule marehemu mbunge wa pande zile sijui ndugu nani vile alihusika sana kuwavutia jamaa shavu upande wao.......jamaa walianza kuvuruga vivuko vya kawaida ili wapate sababu ya kuviingiza hivo vidude vya baharesa
 
Hata mara baada ya vivuko vya temesa kurudi bado azam waliendelea kuvusha watu huku kupitia ripoti ya CAG 2023/2024 tukajua kuwa azam walikuwa wakilipwa shilingi milioni tano kwa siku ambayo kwa mwezi mmoja ni milioni 150 tshs huku wao wakiwa hawalipi kodi wala ushuru wowote.
Unaweza ukaambiwa fedha inakwenda kuimarisha chama
 
Back
Top Bottom