Ujasiriamali: Biashara ya kuuza maji inalipa?

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Wadau Heshima kwenu,

Nina kisima chenye urefu wa ft 56 na kina maji mengi tu ya kutosha kwa matumizi yangu na hata kuwa na ziada.Kisima kimechimbwa mwaka 1999 mwishoni (November). Tangu kilipochimbwa hakijawahi kukauka na maji yake ni mazuri hayana chumvi.

Nafikiria kukijengea na kufunga pampu na kuanza kuuza maji ya ziada, lengo langu ni kuuza maji katika chupa na kuwa na nembo yangu ya biashara. Najua humu kuna watundu wengi tu wanaoweza kujua maji kama ya Kilimanjaro kwa mfano huwa yanapitia hatua zipi hadi kujazwa kwenye chupa na kuingizwa sokoni?

Ni mashine gani zinahitajika kufanya uzalishaji wa maji? Ni materials gani natakiwa kuwa nayo ili kufanikisha uzalishaji huo, Ni vibali gani nahitajika kuwa navyo kabla ya kuanza kuzalisha na kuuza maji kutoka katika kisima changu kwa nembo yangu?

Kwa yeyote mwenye kujua kitu naomba anijuze. Mafanikio yoyote ni yetu sote!!.

Naomba kuwasilisha hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…