BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
Huyu mimi simfagilii, maana anafanya kama udaku................Kama ingekuwa anafanya hivyo baada ya kuombwa, basi isingekuwa ni jambo la kushangaza.................Lakini huyu anaangalia familia ambazo kipato kipo.........hasa kama mke anafanya kazi aua ni mjasiriamali, hapo anajua kuna dili.............lakini sisi ambao wake zetu ni wauza maandazi na chapati uswazi tumesalimika..............
Mpaka sasa simjui na hata hao wanaume ambao ndoa zao zimeingia kizungumkuti hawajamjua kidudu mtu huyo.............Mie mwenyewe amenidokeza mama Ngina baada ya kumegewa siri na shogake..............Nimemuonya katu asije akamtumia huyo shushushu kunifuatilia...........Atajuta.................LOLBiashara matangazo! Anachukua initiative ya kusaka wateja. It is allowed, kosa lake ni kuanza kukusanya data kabla ya initial contract na mteja (cheatwadi). Ila ni lazima afanye baseline survey anyway kujua kama kuna potential. Hehehee, umekamatika mwaka huu dingi, niunganishe nae nimuajiri kwenye kampuni,lol
Labda tumshauri awe anachunguza pande zote...........!
Huyu kijana amegeuka kuwa hatari hapa mtaani ninapoishi. Mpaka sasa kuna ndoa kama saba hivi ambazo inaonekana jahazi linaelekea kuzama kutokana na ushushushu wa huyu kijana anayedai eti amejiajiri ili kujikimu na maisha.
Anachofanya ni kumfuatilia mume wa mtu ambaye anamhisi ni mkware, akishagundua ana nyumba ndogo mahali atahakikisha anajuana na hiyo nyumba ndogo ili apate taarifa za jamaa na ikiwezekana anampiga picha huyo nyumba ndogo kisha anamfuata mke wa jamaa na kujenga naye urafiki na wakizoeana anamweleza kwamba anayo siri kubwa na anaomba ahakikishiwe usalama wake.
Akihakikishiwa usalama wake anamuuliza mke wa muhusika, kama akimpa taarifa kuwa mumewe anayo nyumba ndogo pamoja na ushahidi atamlipa kiasi gani……………Mke akikubali dili, anamwaga siri zote pamoja na picha na details nyingi tu alizokusanya ili mke aweze kumulika mwizi.
Akishakabidhi ushahidi anakunja mkwanja wake kisha anasepa na kuacha timbwili nyuma………………Wanawake hapa mtaani wanampenda kweli na wanapeana namba zake za simu. Sasa hivi huyu kijana anatengezeza mkwanja ile mbaya. Ila nimesikia wanaume wanamuwinda ili wamfanyie kitu mbaya……………………..
Kwamba itapunguza Ukware? hio ni kudanganyana HP.... Hio ndoa itavunjika.... ikiwezekana mwanaume ataoa tena na atacheat vile vile.... na kwa upande mwingine siamini kua ndoa zote ambazo anachonganisha kweli zavunjika. Ingekua anapeleleza wanawake na kupelekea waume zao sawa! Katka ndoa ambazo zipo hadi sasa ni aslimia zaidi ya 60 ambayo wake imewatokea kujua kua mume wake alichepuka/anachepuka nje ya ndoa.....
Labda tumshauri awe anachunguza pande zote...........!