Ujasiriamali ni Ujenzi

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

UJASIRIAMALI NI UJENZI

Ujasiriamali huwa unaanzia mbali toka kwenye kuzaliwa kwa idea mpaka kuja kusimama. Siku zote ujenzi wa Msingi unaanziaga chini kwenda juu, hata ujasiriamali lazima uanzie chini kwenda juu, na kamwe huwezi anzia juu kuja chini mana huwezi ning'iniza matofali hewani. Kwenye ujenzi unaweka tofali moja baada ya jingine, unaangalia uimara wake, unaangalia usawa wake kama umenyooka wakati unaendelea kupanga jingine na kuweka cement, unaangalia kama unajenga kwa ufundi Stadi na ubunifu.

Kwenye Ujasiriamali ni hivyo hivyo utaiwaza Idea, utaweka Plan zitakazoendana na hiyo idea, utafanya survey kama hyo idea itafanikiwa, utaangalia malighafi za kusaidia kuizalisha au kuikamilisha hyo idea na utaangalia kama una ujuzi wa kuikamilisha. Kwenye ujasiriamali unaweza kuwa mwenyewe, unaweza kuwa na wasaidizi, unaweza kuwa fasta au taratibu, unaweza kuwa msafi au mchafu, lakini cha msingi ni Hakikisha unafanya kwa namna yoyote kufikia malengo yako. Mtu aliyewahi kujenga ukuta au mtu aliyewahi kusimamia ujenzi wa ukuta ni tofauti kabisa na mtu ambaye hajawahi kujenga wala kusimamia ujenzi wa ukuta.

Ni sawa na mtu ambaye amewahi kufanya shughuli za kiujasiriamali zikafanikiwa au ziikafeli na yule ambaye hajawahi kabisa kujaribu kufanya ujasiriamali, hawa ni watu wawili tofauti. Kuna mmoja anajua changamoto na ana uthubutu, kuna mwingine kila kitu "Mashikolo mageni". Sawa kwenu usukumani hamna nature ya Ujasiriamali ila umejifunza nini kwa jirani yako mchaga mjasiriamali? au ndo unasubir uuze ng'ombe uende kunywa tu Bia kwe Bar yake na kufanya shopping dukani kwake? Afu kesho ukifulia akakukopeshe kwa riba? Au ng'ombe wakiisha aanze kukuuzia ndizi?
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
Instagram Account Elimu_biashara
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…