Machakos360
New Member
- May 15, 2023
- 2
- 1
UJASIRIAMALI - SIRI YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI:
Ujasiriamali ni dhana ambayo inaelezwa kwa namna tofauti tofauti, wengi hufikiri kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara tu, lakini kiuhalisia ni kwamba?, ujasiriamali ni neno pana linalohusisha Ujuzi na maarifa ya mtu katika namna ya kutumia fursa zilizopo ,kwa namna nyingine ni kubadili Mawazo uliyonayo na kuwa vitendo. pia hujumuisha Ubunifu, kutengeneza kitu kipya Pamoja na kuwa tayari Kukabiliana na ugumu,Vilevile kuwa na uwezo wa kupanga na kuendeleza miradi Ili kufikia Malengo.
Ujasiriamali unaweza kueleza ni namna ya Kufikiri, kutafakari na kutenda Inayosababisha Utengenezaji, uimarishaji, utambuzi na ufanyaji mpya wa vitu Kwa maslahi ya jamii, mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu na jamii.
SIFA ZA MJASIRIAMALI:
Mjasiriamali ni dhahiri atambulike kutokana na sifa hizi, mjasiriamali lazima uwe na sifa hizi,hakika utafanikiwa;
Ujasiriamali ni mtazamo katika akili ya mtu katika kutafuta fursa,kuwa tayari Kukabiliana na ugumu na uwezo wa kutengeneza faida, kuanzisha Biashara mpya au kuongeza tija katika taasisi fulani,pia huwa tayari kukabiliana na hatari kwa lengo la kuzalisha ajira na usitawi kijamii na kiuchumi, nimesema Ujasiriamali sio kuanzisha Biashara tu Lakini pia kubadili utamaduni wa shirika au taasisi, mashine za kufulia au mashine za kuteketezea taulo za kike, simu za mkononi,huduma za usafirishaji na kadi za benki ni mifano ya Mawazo ya ujasiriamali yaliyobadilishwa kuwa bidhaa au huduma.
MITAJI (RASILIMALI) SITA (6) MUHIMU KWA AJILI YA KAZI/UJASIRIAMALI:
Tunatambua kuwa ili mjasiriamali ajikomboe kiuchumi anahitaji Mtaji,mtaji Ni rasilimali inayotumika kuanzisha na kuendesha biashara,tumekuwa tukijiaminisha kuwa PESA Ndiyo mtaji pekee anaohitaji mjasiriamali,huu ni ukweli kiasi tu; na siyo kweli kuwa PESA ni mtaji pekee,Ipo mitaji (rasilimali)sita muhimu sana ambayo MUNGU ametupa wanadamu kwaajili ya kufanyia kazi na kujipatia KIPATO.
1. MUDA
Tajiri na maskini, mrefu na mfupi,mnene na mwembamba,mwanamke na mwanaume, mzungu na mwafrika, wote wamepewa masaa 24 kwa siku, muda ni kitu cha thamani sana kuliko vitu vyote apa duniani na mara nyingi Umaskini au utajiri umo katika muda ambao mtu amepewa na Mungu, cha ajabu kuna mambo ya upuuzi wengi huyafanya na kupoteza muda, ambayo hayawapatii faida.
2. AKILI
Hiki ni moja kati ya vitu vinavyomtofautisha mwanadamu na mnyama, akili ndiyo inayokupa uwezo wa kutambua ,kila tunachokifanya ni matokeo halisi ya jinsi akili zetu zilivyo,kila mmoja anatakiwa kuzitumia akili zake ipasavyo hasa kufikiri.
3. AFYA
Kama kuna rasilimali muhimu kwa mjasiriamali yeyote basi ni Afya,huwezi kufanya lolote endapo afya yako itatetereka, hauwezi kufikiria kitu chenye tija kwa jamii kama ukiwa una afya mbovu, hivyo kila mjasiriamali anapaswa kuilinda AFYA yake,pasipo afya hakuna kazi itakayoweza kufanywa.
kama mjasiriamali Epuka vyakula na vinywaji ambavyo vitakuwa na madhara kwa afya yako.
4. NGUVU
Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe,tumia nguvu zako vizuri ungali bado unazo, nguvu tumepewa kwaajili ya kufanyia kazi ili kujipatia kipato.
5. ARDHI
Ardhi ni moja kati ya rasilimali muhimu sana katika dunia, hakuna kitu mjasiriamali atafanya pasipokuwa na ardhi. Ufungaji wa kuku,ng'ombe, kilimo au biashara yoyote inahitaji ardhi, watu wanaongezeka kila uchao lakini ardhi kamwe haitaongezeka.hebu kama wajasiriamali tujitahidi kuwekeza katika rasilimali hii muhimu kadiri inavyowezekana.
6. WATU
limwenguni kimeanzishwa kitengo katika idara na taasisi mbalimbali kiitwacho kitengo cha Rasilimali watu.kama mjasiriamali,ni lazima utambue kuwa biashara au mradi wako wowote ule unahitaji Watu ili kufanikiwa,watu ni mtaji muhimu sana,hakuna jambo utakalolifanya ambalo halihitaji watu, hivyo Jifunze kuwaheshimu watu wote bila kujali mionekano yao hadhi zao Elimu wala kitu chochote, jifunze kuzungumza na kila mtu, Tengeneza mtandao wa kibiashara na watu mbalimbali na biashara yako itasonga mbele.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KAZI /UJASIRIAMALI:
Kama mjasiriamali ni lazima uzingatie mambo haya;
Kuwa mbunifu
Mjasiriamali ni lazima uwe mbunifu ili uweze kufanikiwa, ubunifu unahusisha kuzitambua,kuziona na kuzitumia fursa. Tumia akili, umiza kichwa, boresha biashara au mradi wako, Epuka kufanya mambo kwa kufuata mkumbo na mazoea fulani, Tafuta Namna ya kuwavutia wateja wako ili waendelee kuja kwako na kukuletea wengine zaidi.
Kuwa na mipango
Ili uweze kufanikiwa na kufikia Malengo, mfano unataka kufika wapi? Siku zote mtu ambaye hajui aendako, hawezi kamwe kujua kama amefika au amepotea, hii ndiyo changamoto ya kutokuwa na mipango.
Penda kazi yako
Siri nyingine ni kuipenda kazi yako kwasababu ukiipenda kazi yako utaifanya kwa furaha, bila hofu na hata Ufanisi utaongezeka.ifurahie kazi yako, ifanye kwa nguvu,moyo, akili na roho yako yote.hii ni siri ya mafanikio katika ujasiriamali.
Usiogope kuchekwa wala kukosolewa
Moja kati ya mbinu anazotumia shetani kuvunja watu moyo ni Ukosoaji,nani umewahi kumwona anafanya hicho unachokifanya wewe? Hutafika popote, na mengine mengi. Haya maneno yamekuwa sumu kali inayoua na kuangamiza dhamira za watu za kutaka kuthubutu, lakini unatakiwa kutambua kuwa upo ukosoaji wa namna mbili, wapo wanaotaka Kujenga na wale Wanaokosoa Kwa lengo la kukatisha tamaa. Kikubwa ni kumwelewa mkosoaji wako haitakusumbua.
Kujitoa/kufanya kwa Imani
Kila linalofanyika hapa duniani, hufanyika kwa kujitoa mhanga, Epuka kuwa kikwazo chako mwenyewe. Mfano, Lima nyanya mtu anasema Zikioza? Fungua kibanda, anasema wakivunja Wakaiba? Ndugu acha kujiweka vigingi! Fanya kwa imani.
Usikubali kukata wala kukatishwa tamaa
Ulimwengu umejaa watu wakukatisha tamaa, lakini unatakiwa kutambua kuwa watu watafanikiwa kukatisha tamaa Endapo utawaruhusu.hakuna mtu aliyewahi kukata tamaa isipokuwa yule aliyekubali kukatishwa tamaa, hivyo mjasiriamali usikubali kukatishwa au kujikatisha tamaa mwenyewe SONGA MBELE!
Anza na ulichonacho
Watu wanajiuliza nitaanza na nini huku tayari ana Akili, Afya, Nguvu, watu na vingine, anza na hivyo usisubiri.
*Mengine ya kuzingatia
1. Kuwa makini na mikopo.
2. Kuwa na nidhamu ya PESA.
3. Badilika kulingana MUDA.
4. Kuwa mtu wa mtazamo chanya.
5. Kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Ujasiriamali ni dhana ambayo inaelezwa kwa namna tofauti tofauti, wengi hufikiri kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara tu, lakini kiuhalisia ni kwamba?, ujasiriamali ni neno pana linalohusisha Ujuzi na maarifa ya mtu katika namna ya kutumia fursa zilizopo ,kwa namna nyingine ni kubadili Mawazo uliyonayo na kuwa vitendo. pia hujumuisha Ubunifu, kutengeneza kitu kipya Pamoja na kuwa tayari Kukabiliana na ugumu,Vilevile kuwa na uwezo wa kupanga na kuendeleza miradi Ili kufikia Malengo.
Ujasiriamali unaweza kueleza ni namna ya Kufikiri, kutafakari na kutenda Inayosababisha Utengenezaji, uimarishaji, utambuzi na ufanyaji mpya wa vitu Kwa maslahi ya jamii, mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu na jamii.
SIFA ZA MJASIRIAMALI:
Mjasiriamali ni dhahiri atambulike kutokana na sifa hizi, mjasiriamali lazima uwe na sifa hizi,hakika utafanikiwa;
- Mwenye kutumia fursa zilizopo.
- Mwenye kuleta tija.
- Mbunifu.
- Mvumbuzi.
- Mwenye kuwa tayari kupambana na hatari yoyote.
- Huchukua uamuzi mapema bila kusubiri tatizo kukua.
- Mwenye kufikia Malengo yake.

Upvote
4