Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wanasiasa wengi wa Tanzania hawana kitu kingine wanaweza kufanya nje ya mfumo wa siasa wakapata kipata kizuri na maisha yao yakaendelea vizuri.
Wengi wanaotoka vyuoni wakajiunga na siasa moja kwa moja hawana principles zozote wanazosimamia zaidi ya maslahi yao tu.
Wanaoacha ajira zao wakajiunga na siasa huwa hawawezi kurudi tena kwenye ajira zao na hivyo kuendelea kufanya kila namna ili wabaki katika mfumo wa siasa.Hao leo wanaweza kusema hivi kesho wakasema vile.
Wafanyabiashara wanasiasa huwa hawapendi kutoka kwenye siasa na biashara zao huyumba sana wanapotoka. Hiyo inawafanya wanang'ang'anie siasa maisha yao yote kulinda biashara zao.Huu ndio unaitwa ujasiriamali wa siasa.
Wanasiasa wetu wengi
1. Hawawezi kuandika vitabu wakauza wakapata kipato.
2. Hawaajiriki nje ya siasa
3. Hawawezi kuanzisha kampuni au biashara zikasimama wakiwa nje ya siasa.
Siasa kuwa sekta inayolipa vizuri nchi hii ni janga kwa ustawi wa Taifa.