Ujasiriamali: Wazo lako la uchumi imara wa nyumbani :Self sufficient home based business idea

Ujasiriamali: Wazo lako la uchumi imara wa nyumbani :Self sufficient home based business idea

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Hii idea imenikaa kwa muda sasa na baada ya kufuatilia uzi wa Ni machine gani ambayo ukiipata itafungua njia zako za kibiashara? nimeipa tafakuri zaidi.

Lakini sio hilo tu fikiria hata masuala ya vita yanayoendelea sasa hivi, kama Russia ingekuwa sio self sufficient country isingewezekana kuendelea kudunda pamoja na vikwazo vya hapa na pale. Sasa kama kitu ni cha kweli kwa taifa, basi ni kweli pia kwa mkoa, ni kweli pia kwa wilaya, miji na hata familia mojamoja. Imagine kukatokea janga/mafuriko/daraja kubomoka sio lazima vita ingefaa kila kaeneo kajitosheleze mahitaji madogo madogo.

Mtanielewa tu, hapa niko nazungumzia namna fulani ya uchumi uliojikita zaidi kwenye kukamilika na kujikamilisha kwa mambo madogomadogo katika small scale katika kila familia. Na inakuwa ni katika uzalishaji yaani kakiwanda kidogo.

Imagine upo kwako una eneo kuuubwa unafuga ngombe na kuku labda. Badala ya kuishia kuuza maziwa katika chupa na bili tu. Bali unaenda na mbele kidogo unakuwa na tuvifungashio flani twa plastiki na vikopo maalumu unasindika maziwa na kuyabrand unauza hata hapo wilayani kwako tu...... hicho tayari ni kiwanda cha maziwa! Ukipata hela yako unaingia online unawasiliana na mjasiriamali wa chakula cha mifugo anakudeliver mzigo wa pumba. Jioni unapumzika zako unaandika kablogu uchwara 'How to make super delicious yoghurt' unachill siku imeisha.

Mwingine amenunua mashine ndogo anatengeneza mafuta ya kupikia, mafuta ya nazi au [kama mimi hivi]mafuta ya nyonyo nayabrand na nayauza.Unaweza kuuza; Mkaa, Vitabu, Sabuni, Losheni/mkorogo, Ubuyu, dagaa wa kukaanga, popcorn, huduma za kufua/usafi au kutoa elimu tu/blog. Any service or entrepreneurship product kwa ajili ya kitaa wilaya na nchi nzima.

Ukiangalia kila mtu anaweza kujizalishia kakitu fulani nyumbani kwake na akauza, na yeye akanunua kitu amezalisha mwingine nyumbani kwake. Aidha kwa kutumia hizo mashine sahili au ujuzi tu mdogomdogo tu. Kama hujaajiriwa unakuwa unafanyia kazi zako home tu, unatoka kupeleka oda [uliyopokea online], na kununua malighafi. Tena ikifikia wanafanya delivery ndio poa zaidi. Kuna watu [hususani introverts] wanaweza wasitoke kabisa nyumbani - kila kitu online tu.

Katika kuwaza [Na kufanya actually] hilo nikaona kuna changamoto moja ya ku-coordinate mambo kufanya mfumo fulani watu wanaweza kupata masoko. Kujua mjasiriamali gani/wapi nitapata bidhaa fulani na nani atanunua bidhaa yangu. Kiufupi ni soko la hizo bidhaa ndogondogo za kijasiriamali Tanzania/wilayani kwako/mtaani kwako hasa online. Naamini tukiwa/[tukitumia maana zipo] na online platform moja ya kuwakutanisha wajasiriamali wooote wazo la watu kujiajiri litakuwa tamu zaidi. -HOME BASED ECONOMY

Hata wazungu walifanya sana hii kitu na hadi wameendelea kiviwanda. Ukisikia akina Smith, akina Tailor, akina Baker jua wote hawa zilikuwaga ndo biashara za familia na ukoo wao. Hadi sasa wakulima wa kizungu wanakuwaga na kakiwanda hukohuko shambani. Wewe una wazo gani la kujenga uchumi binafsi wa nyumbani kwako, familly home based economy na taifa kwa ujumla?
 
You killed and nailed it man! Na hili ndilo changamoto kubwa hapa nchini. Tanzania ya viwanda inapaswa kuanza chini, sio juu.
Kabisa, na tukilifanikisha hilo mzee. Afrika patakuwa 'heaven on earth' kabisa. Mazingira yetu yanatupendelea kabisa.

Nawazaga hata kama familia ni ndogo zaidi basi tuanze na makanisa/madhehebu.....mfano tu hata kila kanisa likaamua kujichanga kuunda miradi/viwanda kuajiri waumini wake wahitaji asee. Watu wanaenda kazini wanapokea neno na hela/mahitaji at the same spot, kwa upendo na ushirikiano......... difinisheni ya ufalme wa kimbingu
 
Wazo sahihi na ndivyo ukipita maeneo flani huko mbeya hasa rungwe , wakazi wake wanaishi maisha hayo, analima ndizi na kahawa shambani kwake, then anafuga mifugo (karibu kila familia ina ngombe wa maziwa) so anauza maziwa, anavuna ndizi anauza, anachkua samadi aliyozalisha shambani kwake anaisambaza shambani, so haendi mbali kufanya shuguli zake, lakini wanajenga , wanasomesha nk , niliga huo mfumo naona unalipa kwa hapa njombe
 
Wazo sahihi na ndivyo ukipita maeneo flani huko mbeya hasa rungwe , wakazi wake wanaishi maisha hayo, analima ndizi na kahawa shambani kwake, then anafuga mifugo (karibu kila familia ina ngombe wa maziwa) so anauza maziwa, anavuna ndizi anauza, anachkua samadi aliyozalisha shambani kwake anaisambaza shambani, so haendi mbali kufanya shuguli zake, lakini wanajenga , wanasomesha nk , niliga huo mfumo naona unalipa kwa hapa njombe
Yaani mi mwenyewe naitamani sana hii kitu

Ntafanikisha kuishi namna hiyo tu Inshallah, bado naipangilia mipango
 
Back
Top Bottom