Ujasusi Kwenye Ushindani wa Kibiashara

Ujasusi Kwenye Ushindani wa Kibiashara

Joined
Jun 21, 2021
Posts
6
Reaction score
12
1736787896758.png

Uandaaji wa Mpango Mkakati yaani “Strategic Planning” unahusisha ukusanyaji na ufanyaji wa tathmini wa taarifa juu ya mazingira ya nje yanayoizunguka kampuni yaani “external environment”. Mazingira haya yamehawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni’​
  • Fursa. Haya ni mazingira chanya yanoyoizunguka kampuni, na ikiwa kampuni itaamua kuyatumia kikamilifu, basi itafanikiwa katika biashara zake. Mfano wake ni; ushindani, ongezeko la kipato cha watu, uboreshaji wa miundo mbinu, utungwaji wa sera na sheria rafiki kwa biashara n.k​
  • Changamoto. Haya ni mazingira hasi yanayoizunguka kampuni, na yanaweza kuhatarisha biashara za kampuni husika. Kimsingi kampuni haina uwezo wa kuyaepuka, ila tu inaweza kupunguza athari zake.​
Ukusanyaji wa taarifa juu ya mazingira ya nje, mara nyingi haufanyiki kwa njia rasmi, taarifa zinaweza kukusanywa kutoka kwa wateja, kwenye machapisho mbalimbali ya sekta husika, kutoka kwa wafanyakazi, n.k. Ukusanyaji wa taarifa hizi hauwezi kufanikiwa bila kufanya Ujasusi wa Kiushindani.
Ujasusi wa Kiushindani ni programu maalumu inayoanzishwa na kampuni kwa lengo la kukusanya taarifa za washindani wa kampuni husika. Kitaalamu inaitwa “Competitive Intelligence” au “Business Intelligence”. Tafiti zinaonyesha kwamba kuna mahusiano makubwa kati ya utendaji mzuri wa kampuni na kuwa na programu ya ujasusi wa kiushindani.
Asilimia 78 ya kampuni kubwa ulimwenguni zimeanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya kushughulika na ujasusi wa kiushindani, kampuni zingine zinaunganisha programu hii nia idara za masoko, zingine idara za utafiti na maendeleo.

Vyanzo vya Taarifa za Ujasusi kwenye Ushindani wa Biashara
Kuna vyanzo mbalimabli ambavyo vinatumika kukusanya taarifa za kijasusi juu ya ushindani na mazingira ya nje ya kampuni kiujumla.​
  • Kuna kampuni maalumu zimeanzishwa kwa ajili ya kutoa huduma hii, lakini mara nyingi kampuni hizi zinatoa huduma ya ukusanyaji na wakati mwingine tathmini ya mazingira ya nje kiujumla, kama vile ushindani kwenye sekta, ukuaji wa soko n.k.​
  • Kutumia wafanyakazi wa zamani wa kampuni shindani ili kupata taarifa za siri. Mfano utafiti uliofanywa na PricewaterhouseCoopers unaonyehsa kwamba kwa mwaka kampuni zinapoteza kiasi cha shilingi dola za kimarekani bilioni 59 kwa wizi wa siri za biashara.​
  • Intaneti pia imekuwa ni suluhisho kubwa kwenye upatikanaji wa taarifa za kijasusi kwenye ushindani. Hivyo watendaji wanaohusika na masuala ya mipango mikakati kwenye kampuni za kibiashara hawana budi kutumia fursa itokanayo na intaneti. Ijapokuwa tahadhari inapaswa kuwepo kwenye matumizi ya taarifa zitokanazo na intaneti, hii ni kwa sababu, sio taarifa zote zinazopatikana kwenye intaneti ni sahihi, zingine ni za uongo.
  • N.k
Article By;

HEINZ Management Consulting
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
P.O Box 12119
Dar es Salaam
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: heinzconsultancy@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania​
 
Unapata taarifa Comoro wanahitaji mbuzi kwa wingi, hapo unaanza kuandika taarifa za mshindani ili iweje? Hapo kupima nguvu zako baasi.

Tazama azam TV kakuta tamthilia za nje dstv , yeye kaja kuzitafsiri.

Somo: Tengeneza niche yako , refer kitabu: Blue ocean strategy
 
Back
Top Bottom